Radd Ya ´Allaamah an-Najmiy Kwa Abu Bakr al-Jazaairiy Kuwasifu Jamaa´at-ut-Tabliygh

Baadhi ya ndugu Salafiyyuun wamenionesha maneno ya Shaykh Abu Bakr al-Jazaairiy ambapo amesema: ”Ninaapa kwa Allaah kuwa hakuna kundi lolote katika ulimwengu wa Kiislamu ambalo linalingania katika Uislamu na kuwafanya watu kuwa bora kuliko Jamaa´at-ut-Tabliygh.” Namna hii ndivo anavyoapa Abu Bakr kiapo hichi cha dhambi na kwamba hakuna kundi lolote katika ulimwengu wa Kiislamu ambalo ni bora kuliko Jamaa´at-ut-Tabliygh. Sikudhani kamwe kuwa wewe, Abu Bakr, utakuwa namna hiyo mwenye kuachwa. Unapendekeza Jamaa´at-ut-Tabliygh ambao ni Suufiyyah, waabudu makaburi, makhurafi, Deobandiyyah na washirikina mbele ya madhehebu ya Salafiyyah. Je, hujui kuwa kaburi la mwanzilishi wa kundi hili liko Msikitini? Je, hujui kuwa wanakaa kwenye makaburi ya Suufiyyah na kuwaomba msukumo? Je, hujui kuwa Jamaa´at-ut-Tabliyh imejengeka juu ya maneno mane ya ki-Suufiy? Je, hujui kuwa wanawachukia watu wa Tawhiyd? Hukumsikia Mola Wako Akisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ “Kwa yakini umeletewa Wahy na kwa wale walio kabla yako (kwamba): “Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako (zote), na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”? (39:65) Hukumsikia Mola Wako Akisema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ “Basi usiombe (au kuabudu) pamoja na Allaah mungu mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa.”? (26:213) Jaabir! Je, wewe humchi Allaah wakati unapodai kitu kama hicho? Isitoshe unaapa juu ya hilo pia wakati wewe unapiga vita madhehebu ya Tawhiyd na mji wa Tawhiyd katika nchi ya Tawhiyd ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alihamia ndani yake na Tawhiyd ya Mtume. Unadai kuwa umefasiri Kitabu cha Allaah. Je, hukuchuma mafunzo yoyote ya utahadharisho wa Qur-aan dhidi ya Shirki na ulinganio wake katika Tawhiyd? Je, hutubii, Jaabir? Ukifa katika hali hiyo basi ninakudhamini kwamba mkutano wako na Allaah utakuwa mgumu. Tubu kwa Allaah kabla hakujachelewa. Ukifanya kiburi na ukakataa kutubia ninaonelea kuwa umekwenda na maji. Imeandikwa na mtu anayekutakia kheri Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy Mwandishi: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy Chanzo: al-Fataawaa al-Jaliyyah (2/138)7 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Baadhi ya ndugu Salafiyyuun wamenionesha maneno ya Shaykh Abu Bakr al-Jazaairiy ambapo amesema:

”Ninaapa kwa Allaah kuwa hakuna kundi lolote katika ulimwengu wa Kiislamu ambalo linalingania katika Uislamu na kuwafanya watu kuwa bora kuliko Jamaa´at-ut-Tabliygh.”

Namna hii ndivo anavyoapa Abu Bakr kiapo hichi cha dhambi na kwamba hakuna kundi lolote katika ulimwengu wa Kiislamu ambalo ni bora kuliko Jamaa´at-ut-Tabliygh.

Sikudhani kamwe kuwa wewe, Abu Bakr, utakuwa namna hiyo mwenye kuachwa. Unapendekeza Jamaa´at-ut-Tabliygh ambao ni Suufiyyah, waabudu makaburi, makhurafi, Deobandiyyah na washirikina mbele ya madhehebu ya Salafiyyah. Je, hujui kuwa kaburi la mwanzilishi wa kundi hili liko Msikitini? Je, hujui kuwa wanakaa kwenye makaburi ya Suufiyyah na kuwaomba msukumo? Je, hujui kuwa Jamaa´at-ut-Tabliyh imejengeka juu ya maneno mane ya ki-Suufiy? Je, hujui kuwa wanawachukia watu wa Tawhiyd? Hukumsikia Mola Wako Akisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ
“Kwa yakini umeletewa Wahy na kwa wale walio kabla yako (kwamba): “Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako (zote), na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”? (39:65)

Hukumsikia Mola Wako Akisema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ
“Basi usiombe (au kuabudu) pamoja na Allaah mungu mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa.”? (26:213)

Jaabir! Je, wewe humchi Allaah wakati unapodai kitu kama hicho? Isitoshe unaapa juu ya hilo pia wakati wewe unapiga vita madhehebu ya Tawhiyd na mji wa Tawhiyd katika nchi ya Tawhiyd ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alihamia ndani yake na Tawhiyd ya Mtume. Unadai kuwa umefasiri Kitabu cha Allaah. Je, hukuchuma mafunzo yoyote ya utahadharisho wa Qur-aan dhidi ya Shirki na ulinganio wake katika Tawhiyd? Je, hutubii, Jaabir? Ukifa katika hali hiyo basi ninakudhamini kwamba mkutano wako na Allaah utakuwa mgumu. Tubu kwa Allaah kabla hakujachelewa. Ukifanya kiburi na ukakataa kutubia ninaonelea kuwa umekwenda na maji.

Imeandikwa na mtu anayekutakia kheri

Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy

Mwandishi: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Chanzo: al-Fataawaa al-Jaliyyah (2/138)7
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Jazaairiy, Abu Bakr
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 15th, April 2014