Radd Kwa Suufiyyah Waonao Kuwa Hawana Haja Ya Kumuabudu Allaah

Tazkiyah anayojisifu nayo mtu, ili afanye kitendo kizuri cha kujitakasa nafsi yake. Na Tazkiyah anayohukumiwa nayo mtu, ni pale anapomfahamisha Allaah kuhusu matendo yake na kujisifu. Ni kama vile anaona anamfanyia huduma Allaah. Anasema nimeswali, nimetoa Swadaqah, nimefunga, nimeenda Hajj, nimepigana Jihaad, nimewatendea wema wazazi na mfano wa hayo. Haijuzu kwa mtu kujisifia nafsi yake na kusema mimi mimi. Na kwa hili ni Radd kwa Suufiyyah wanaodai kuwa ni maimamu na wanajisifu nafsi zao. Na wanadai tumefikia katika kiwango ambacho hakitulazimi tena kumtii Allaah. Kuna watu wanaodai hivyo. Wanasema kuwa wao wamefikia kiwango cha Al-Malaquut na kuwa hawana uwajibu wa Swalah, Swadaqah, Swawm na kwamba hakuna kilichoharamu kwao. Watu kama hawa wametoka katika Dini kabisa. Hivyo wale wanaojisifu nafsi zao wenyewe ni watu walioko mbali kabisa na utakatifu.

  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (173 A)
  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 13th, January 2014