Radd Kwa Murji-ah al-Fuqahaa´ Wanaosema Imani Ni Kuamini Na Kutamka Tu

Kadhalika imani sio kama wanavyosema Murji-ah al-Fuqahaa´ kwamba imani ni kutamka kwa ulimi na kuamini moyoni. Kwa kuwa ingelikuwa ni hivyo maamrisho na makatazo yasingelikuwa na faida, ingelitosheleza kwa mtu kuamini moyoni mwake na akatamka kwa ulimi wake, hata kama hakufunga na kuswali. Haya ni madhehebu batili bila ya shaka. Kwa kuwa wanakanusha matendo yote. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ameambatanisha matendo na imani katika Aayah nyingi: “Walioamini na wakatenda mema.” Hakusema: “Walioamini” tu. au “Wakatenda mema.” tu. Ni lazima kuwepo mambo yote mawili, matendo hayatoshelezi bila ya kuamini kama jinsi kuamini hakutoshelezi bila ya matendo. Kuamini na matendo mema ni mambo mawili yanaenda sambamba. Hili lipo katika Aayah nyingi. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 190

Kadhalika imani sio kama wanavyosema Murji-ah al-Fuqahaa´ kwamba imani ni kutamka kwa ulimi na kuamini moyoni. Kwa kuwa ingelikuwa ni hivyo maamrisho na makatazo yasingelikuwa na faida, ingelitosheleza kwa mtu kuamini moyoni mwake na akatamka kwa ulimi wake, hata kama hakufunga na kuswali. Haya ni madhehebu batili bila ya shaka. Kwa kuwa wanakanusha matendo yote. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ameambatanisha matendo na imani katika Aayah nyingi:

“Walioamini na wakatenda mema.”

Hakusema: “Walioamini” tu.

au

“Wakatenda mema.” tu.

Ni lazima kuwepo mambo yote mawili, matendo hayatoshelezi bila ya kuamini kama jinsi kuamini hakutoshelezi bila ya matendo. Kuamini na matendo mema ni mambo mawili yanaenda sambamba. Hili lipo katika Aayah nyingi.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 190


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 27th, February 2014