Radd Kwa Karaamiyyah Wanaosema Imani Ni Kutamka Tu

Imani sio kutamka kwa ulimi tu bila ya kuamini moyoni, kama wanavosema Karraamiyyah. Kwa kuwa kutokana na kauli hii wanafiki wanakuwa waumini. Kwa kuwa wanatamka kwa ndimi zao lakini wanapinga kwa mioyo yao. Allaah Amewahukumu kuwa wako katika tabaka ya chini kabisa Motoni chini ya washirikina. Anasema: وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ “Na miongoni mwa watu wako wasemao... “ yaani wanatamka: آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho” hali ya kuwa si wenye kuamini.” (al-Baqarah:08) yaani wanatamka kwa ndimi zao. Katika Aayah nyingine Anasema: يَقُولُونَ بِأَفْوَاهِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ “Wanasema kwa midomo yao, yale yasiyokuwemo katika nyoyo zao.” (al-´Imraan:167) Kule kutamka tu hakutoshelezi. Bali Allaah Amesema kuhusu wao: اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً “Wamefanya viapo vyao (vya uongo) kuwa ni kinga (ya ‘amali zao ovu).” (al-Munaafiquun:02) yaani sitara: اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا “Wamefanya viapo vyao (vya uongo) kuwa ni kinga (ya ‘amali zao ovu). Hivyo wakazuia (watu) njia ya Allaah, hakika ni uovu mbaya mno waliokuwa wakitenda. Hiyo ni kwa kuwa wao waliamini, kisha wakakufuru.” (al-Munaafiquun:02-03) “wao waliamini... ”, wameamini kwa ndimi zao: “... kisha wakakufuru”, kwa mioyo yao. Kutamka kwa ulimi hakutoshelezi, hata kama mtu atajua hilo, hata kama atapigana vita na akapigana Jihaad pamoja na Waislamu, lau ataswali na kufunga, haya hayatoshelezi mpaka aamini kwa moyo wake yaliyotamkwa na ulimi wake. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 189-190

Imani sio kutamka kwa ulimi tu bila ya kuamini moyoni, kama wanavosema Karraamiyyah. Kwa kuwa kutokana na kauli hii wanafiki wanakuwa waumini. Kwa kuwa wanatamka kwa ndimi zao lakini wanapinga kwa mioyo yao. Allaah Amewahukumu kuwa wako katika tabaka ya chini kabisa Motoni chini ya washirikina. Anasema:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ

“Na miongoni mwa watu wako wasemao… “

yaani wanatamka:

آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ
”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho” hali ya kuwa si wenye kuamini.” (al-Baqarah:08)

yaani wanatamka kwa ndimi zao.

Katika Aayah nyingine Anasema:

يَقُولُونَ بِأَفْوَاهِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ
“Wanasema kwa midomo yao, yale yasiyokuwemo katika nyoyo zao.” (al-´Imraan:167)

Kule kutamka tu hakutoshelezi. Bali Allaah Amesema kuhusu wao:

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً
“Wamefanya viapo vyao (vya uongo) kuwa ni kinga (ya ‘amali zao ovu).” (al-Munaafiquun:02)

yaani sitara:

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا
“Wamefanya viapo vyao (vya uongo) kuwa ni kinga (ya ‘amali zao ovu). Hivyo wakazuia (watu) njia ya Allaah, hakika ni uovu mbaya mno waliokuwa wakitenda. Hiyo ni kwa kuwa wao waliamini, kisha wakakufuru.” (al-Munaafiquun:02-03)

“wao waliamini… ”, wameamini kwa ndimi zao:

“… kisha wakakufuru”, kwa mioyo yao.

Kutamka kwa ulimi hakutoshelezi, hata kama mtu atajua hilo, hata kama atapigana vita na akapigana Jihaad pamoja na Waislamu, lau ataswali na kufunga, haya hayatoshelezi mpaka aamini kwa moyo wake yaliyotamkwa na ulimi wake.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 189-190


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 27th, February 2014