Radd Kwa Jabriyyah Na Qadariyyah

Shaykh Abu ´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy: Na kawaradi Allaah (Jalla wa ´Alaa) makundi mawili kwa kauli Yake (Jalla wa ´Alaa): لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ "Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona." (42:11) Anawaradi Mushabbihah kwa kauli Yake Allaah (Ta´ala): لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ "Hapana kitu kama mfano wake." (42:11) Hapa anawaradi Mushabbihah. Na kauli Yake Allaah: وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ "Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona." (42:11) Hapa Anawaradi al-Muattwilah , Watu wahaki ndio wanathibitisha Sifa za Allaah (Jalla wa ´Alaa) uthibitisho usiokuwa na mfano, na hawazifananishi na sifa za viumbe kwa kutegemea Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa): لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ “Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” (42:11) Wao wako kati kwa kati, katika mlango vitendo vya Allaah baina ya Jabriyyah na al-Qadariyyah. Jabriyyah wamechupa mipaka katika Qadar, wakapinga matendo ya waja na wakasema: "Binaadamu kafungwa katika matendo yake, hana khiari wala matakwa." Ni mwenye kuzini na wakati huohuo si yeye mwenye kuzini, anaiba na si yeye mwenye kuiba - wanathibisha kuwa matendo haya ni majawaliwa, na [wanasema] kwa uhakika mtendaji ni Allaah (´Azza wa ´Alaa). Na haya ni madhehebu batili, madhehebu ya Jabriyyah, na ndio madhehebu ya Jahmiy bin Safwaan (muasisi wa Jahmiyyah).

Shaykh Abu ´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy:

Na kawaradi Allaah (Jalla wa ´Alaa) makundi mawili kwa kauli Yake (Jalla wa ´Alaa):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ
“Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” (42:11)

Anawaradi Mushabbihah kwa kauli Yake Allaah (Ta´ala):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hapana kitu kama mfano wake.” (42:11)

Hapa anawaradi Mushabbihah. Na kauli Yake Allaah:

وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ
“Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” (42:11)

Hapa Anawaradi al-Muattwilah , Watu wahaki ndio wanathibitisha Sifa za Allaah (Jalla wa ´Alaa) uthibitisho usiokuwa na mfano, na hawazifananishi na sifa za viumbe kwa kutegemea Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ
“Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” (42:11)

Wao wako kati kwa kati, katika mlango vitendo vya Allaah baina ya Jabriyyah na al-Qadariyyah. Jabriyyah wamechupa mipaka katika Qadar, wakapinga matendo ya waja na wakasema:

“Binaadamu kafungwa katika matendo yake, hana khiari wala matakwa.”

Ni mwenye kuzini na wakati huohuo si yeye mwenye kuzini, anaiba na si yeye mwenye kuiba – wanathibisha kuwa matendo haya ni majawaliwa, na [wanasema] kwa uhakika mtendaji ni Allaah (´Azza wa ´Alaa). Na haya ni madhehebu batili, madhehebu ya Jabriyyah, na ndio madhehebu ya Jahmiy bin Safwaan (muasisi wa Jahmiyyah).