Qur-aaniyyuun Ni Kundi Gani?

´Allaamah al-Fawzaan: Qur-aaniyuun ni wale wanaopinga Sunnah, wanapinga kuzifanyia kazi Hadiyth na wanasema hatutaki kitu isipokuwa Qur-aan tu. Watu watu ni waongo, hakika hawakuifanyia kazi Qur-aan. Kwa kuwa Allaah kasema katika Qur-aan: إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ “Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu.” (59:07) Na Akasema Allaah kumwambia Mtume Wake: وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ “Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao.” (16:44) Ikiachwa Sunnah vipi angeliweza kuibainisha Qur-aan? Nani ambaye angeliibainisha Qur-aan? Ikiachwa Sunnah vipi angeliweza kuibainisha Qur-aan? Nani ambaye angeliifasiri Qur-aan? Ni Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hizo ndio zinaibainisha Qur-aan na zinaifasiri Qur-aan. Ni Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hizo ndio zinaibainisha Qur-aan na zinaifasiri Qur-aan. Wale ambao wanapinga Sunnah, ikiwa wamekusudia hili huku ni kumkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii inakuwa kufuru na kuritadi. Ama ikiwa ni wajinga na wanafuata kichwa mchunga wabainishiwe na kuwekewa wazi jambo hili. Walikuja kwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) na wakamwambia hivi, akasema (Radhiya Allaahu ´anhu): وَأَقِيمُواْ الصَّلاَةَ “Na shikeni Swalah.” (02:43) Ni idadi ngapi za Rakaa? Ni wakati upi wa Swalah? (Hali kadhalika Allaah Anasema): وَآتُواْ الزَّكَاةَ “Na toeni Zakaah.” (02:43) Ni nisaab ngapi? Na ni kipimo gani cha Zakaah kitatolewa? Wakakwama hapo na hawakuweza kumjibu, akawasimamisha (Rahimahu Allaah). Hii ni dalili kuwa Qur-aan lazima iambatane na Sunnah. Na Sunnah ndio Wahyi wa pili baada ya Qur-aan. Inaifasiri Qur-aan, kuibainisha, kuiweka wazi, kuitolea dalili. Na kunaweza kuja hukumu ambayo haipo ndani ya Qur-aan. Kwa mfano (uharamu) wa mwanamke kuoana na mjomba wake, mwanamke kuoana na khalat yake - haya hayapo katika Qur-aan. Bali haya yapo katika Sunnah. Unyonyeshaji. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa): وَأُمَّهَاتُكُمُ اللاَّتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ “Na mama zenu waliokunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya.” (04:23) Ni kunyonya mara ngapi? Na lini kunyonya inahesabika kuwa ni Haramu? Haya yamekuja katika Sunnah za Mtume. Haya yamekuja katika Sunnah za Mtume, kayabainisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akasema: "Ni haramu kwa unyonyaji yale ambayo ni Haramu kwa nasabu." Hadiyth ikaweka wazi zaidi kuliko jinsi ilivyokuja katika Aayah. وَأُمَّهَاتُكُمُ اللاَّتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ “Na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya.” (04:23) Imekuja namna hii tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: "Ni haramu kwa unyonyaji yale ambayo ni Haramu kwa nasabu." Mama mdogo, khalati, mtoto wa kaka, mtoto wa dada n,k. Haya hayakuja katika Qur-aan. Yamekuja katika Sunnah. "Ni haramu kwa unyonyaji yale ambayo ni Haramu kwa nasabu."

´Allaamah al-Fawzaan:

Qur-aaniyuun ni wale wanaopinga Sunnah, wanapinga kuzifanyia kazi Hadiyth na wanasema hatutaki kitu isipokuwa Qur-aan tu. Watu watu ni waongo, hakika hawakuifanyia kazi Qur-aan. Kwa kuwa Allaah kasema katika Qur-aan:

إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ
“Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu.” (59:07)

Na Akasema Allaah kumwambia Mtume Wake:

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ
“Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao.” (16:44)

Ikiachwa Sunnah vipi angeliweza kuibainisha Qur-aan? Nani ambaye angeliibainisha Qur-aan? Ikiachwa Sunnah vipi angeliweza kuibainisha Qur-aan? Nani ambaye angeliifasiri Qur-aan? Ni Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hizo ndio zinaibainisha Qur-aan na zinaifasiri Qur-aan. Ni Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hizo ndio zinaibainisha Qur-aan na zinaifasiri Qur-aan.
Wale ambao wanapinga Sunnah, ikiwa wamekusudia hili huku ni kumkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii inakuwa kufuru na kuritadi. Ama ikiwa ni wajinga na wanafuata kichwa mchunga wabainishiwe na kuwekewa wazi jambo hili. Walikuja kwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) na wakamwambia hivi, akasema (Radhiya Allaahu ´anhu):

وَأَقِيمُواْ الصَّلاَةَ
“Na shikeni Swalah.” (02:43)

Ni idadi ngapi za Rakaa? Ni wakati upi wa Swalah? (Hali kadhalika Allaah Anasema):
وَآتُواْ الزَّكَاةَ
“Na toeni Zakaah.” (02:43)

Ni nisaab ngapi? Na ni kipimo gani cha Zakaah kitatolewa? Wakakwama hapo na hawakuweza kumjibu, akawasimamisha (Rahimahu Allaah). Hii ni dalili kuwa Qur-aan lazima iambatane na Sunnah. Na Sunnah ndio Wahyi wa pili baada ya Qur-aan. Inaifasiri Qur-aan, kuibainisha, kuiweka wazi, kuitolea dalili. Na kunaweza kuja hukumu ambayo haipo ndani ya Qur-aan. Kwa mfano (uharamu) wa mwanamke kuoana na mjomba wake, mwanamke kuoana na khalat yake – haya hayapo katika Qur-aan. Bali haya yapo katika Sunnah. Unyonyeshaji. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

وَأُمَّهَاتُكُمُ اللاَّتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ
“Na mama zenu waliokunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya.” (04:23)

Ni kunyonya mara ngapi? Na lini kunyonya inahesabika kuwa ni Haramu? Haya yamekuja katika Sunnah za Mtume. Haya yamekuja katika Sunnah za Mtume, kayabainisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akasema:

“Ni haramu kwa unyonyaji yale ambayo ni Haramu kwa nasabu.”

Hadiyth ikaweka wazi zaidi kuliko jinsi ilivyokuja katika Aayah.

وَأُمَّهَاتُكُمُ اللاَّتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ
“Na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya.” (04:23)

Imekuja namna hii tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Ni haramu kwa unyonyaji yale ambayo ni Haramu kwa nasabu.”

Mama mdogo, khalati, mtoto wa kaka, mtoto wa dada n,k. Haya hayakuja katika Qur-aan. Yamekuja katika Sunnah.

“Ni haramu kwa unyonyaji yale ambayo ni Haramu kwa nasabu.”