Picha Na Video Zinazochukuliwa Harusini

Katika mambo ya munkari wanawake wanakuwa na ala za kupicha picha ili wasajili hafla na kuhifadhi picha zao, na sijui nani kawaruhusu wanawake hawa kuchukua picha za hafla ili wasambaze baina ya watu sawa kwa kukusudia au kwa kutokukusudia. Je, mnadhani wanawake hawa wanaokamatwa picha za kwenye hafla kuna anaeridhia kuchukuliwa picha ya ahli wake - mke wake, au binti yake, au dadake au mamake? Ienezwe kwenye mikono ya watu hawa waovu waifanye watakavyo wamtakaye. Ataridhia yeyote kati yenu picha ya Mahram wake kuwa baina ya mikono ya watu, ifanyiziwe maskhara ikiwa [mwanamke huyo] ni mbaya na athari ya fitina ikiwa [mwanamke huyo] ni mzuri. Baya zaidi waliopigwa picha ikiwa ni wajane wamechanganyika na wanawake au wako wenyewe. Wala hawezi kupinga yeyote anayejua Shari´ah inavyosema kuwa hili ni katika mambo ya maovu na ni kufuata kichwa mchunga makafiri na wanaojifananisha nao. Baya zaidi ni baadhi ya watu waovu wanakuwa na ala ya video wakamate picha za wajane, wanaziona wao na wasiyokuwa wao kila wanapotaka kuburudika kumwangalia mjane huyu. Dawa ya hilo ni sisi kurejea katika Imani yetu, akili zetu, muruwa wetu, tabia yetu nzuri, turejea kwa waliokuwemo Salaf-us-Swaalih (wema wetu waliotangulia). Tuachane na mambo kama haya maovu, tuachane na kufuata vichwa mchunga. Hakika sisi ni Ummah wa Kiislamu Ummah bora... Tuzifanye hafla zetu kuwa za Kishari´ah za Kiislamu kwa waliokuwemo Salaf-us-Swaalih. Hakika kufanya hivi ni katika kushukuru neema za Allaah juu yetu...

Katika mambo ya munkari wanawake wanakuwa na ala za kupicha picha ili wasajili hafla na kuhifadhi picha zao, na sijui nani kawaruhusu wanawake hawa kuchukua picha za hafla ili wasambaze baina ya watu sawa kwa kukusudia au kwa kutokukusudia.

Je, mnadhani wanawake hawa wanaokamatwa picha za kwenye hafla kuna anaeridhia kuchukuliwa picha ya ahli wake – mke wake, au binti yake, au dadake au mamake? Ienezwe kwenye mikono ya watu hawa waovu waifanye watakavyo wamtakaye. Ataridhia yeyote kati yenu picha ya Mahram wake kuwa baina ya mikono ya watu, ifanyiziwe maskhara ikiwa [mwanamke huyo] ni mbaya na athari ya fitina ikiwa [mwanamke huyo] ni mzuri. Baya zaidi waliopigwa picha ikiwa ni wajane wamechanganyika na wanawake au wako wenyewe. Wala hawezi kupinga yeyote anayejua Shari´ah inavyosema kuwa hili ni katika mambo ya maovu na ni kufuata kichwa mchunga makafiri na wanaojifananisha nao.

Baya zaidi ni baadhi ya watu waovu wanakuwa na ala ya video wakamate picha za wajane, wanaziona wao na wasiyokuwa wao kila wanapotaka kuburudika kumwangalia mjane huyu. Dawa ya hilo ni sisi kurejea katika Imani yetu, akili zetu, muruwa wetu, tabia yetu nzuri, turejea kwa waliokuwemo Salaf-us-Swaalih (wema wetu waliotangulia). Tuachane na mambo kama haya maovu, tuachane na kufuata vichwa mchunga. Hakika sisi ni Ummah wa Kiislamu Ummah bora… Tuzifanye hafla zetu kuwa za Kishari´ah za Kiislamu kwa waliokuwemo Salaf-us-Swaalih. Hakika kufanya hivi ni katika kushukuru neema za Allaah juu yetu…