Pata Mafunzo Kutoka Dammaaj

Ndugu! Da´wah yetu sio ya kuvimbisha mifupa. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba sisi tunampenda mwanafunzi aliye na adabu asiyekuwa na fujo. Tunampenda na kumkubali kwa furaha. Wakati huo huo tunamchukia yule mwenye kuleta vurugu. Dammaaj iko wapi? Hatutakiwi kuzingatia juu ya Dammaaj? Ina maana mazingatio yanatupitia pasina kuzingatia. Mawaidha yanatupitia pasina kuwaidhika. Tunamuomba Allaah kinga kutokana na kughafilika. Huku ni kughafilika, ujinga na upofu. Ni wajibu kwetu kupata mafunzo. Tazama wale waliosababisha vurugu Dammaaj! Wameifanya nini Dammaaj? Wameichoma Dammaaj na ardhi. Ni vurugu. Ni kuvimbisha mifupa. Ni upondaji wa wanachuoni. Kila mmoja anataka kujionyesha. Kila mmoja anataka kujulikana. Ninaapa kwa Allaah hili ni khatari. Ni khatari katika Da´wah, mtu mwenyewe, kundi na jamii. Hili hatulikubali. Mwanafunzi ni lazima ajilazimie kuwa na adabu kwa mwalimu wake, mwanachuoni, walinganizi na Waislamu. Mwenye kuonesha u-Hizbiyyah wake tunamalizana naye. Tumekwishamalizana na watu wa Hizbiyyah na Ahl-ul-Bid´ah. Hatujishughulishi na wao. Tumekwishamalizana nao. Ninakumbuka maneno ya Shaykh Muqbil (Rahimahu Allaah) amesema: “Ndugu! Ninapenda maneno ya Shaykh Abu Ibraahiym Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab “Hatupotezi wakati wetu na Hizbiyyuun. Tunasema yale tulio nayo ya kusema na kusonga mbele.” Maneno mazuri. Bainisha na songa mbele. Wewe kama mwanafunzi tilia umuhimu mkubwa wa kutafuta elimu na mhimdi Allaah Aliyekujaalia kuja katika Maraakiz hizi za Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hazikuwepo hapo kabla na mhimidi Allaah. Unatakiwa kuzihifadhi. Haitoshelezi Shaykh tu yeye mwenyewe ndiye akahifadhi nafasi hii. Shaykh wa Ma´bar, Mafraq Hubaysh, Fuyuush au Hudaydah hawezi kufanya yote. Nyote mnatakiwa kuchangia. Hii ni neema kubwa kuliko dunia nzima. Nyote mnatakiwa kuihifadhi. Moja ya njia ya kuzihifadhi ni kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maasi ni sababu ya kuwaharibu watu na miji: فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ “Basi nyooka kama ulivyoamrishwa na aliyetubia pamoja nawe, na wala msiruke mipaka. Hakika Yeye kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona yote daima).” (11:112-113) Ni lazima tushikamane bara bara na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tusifanye Daar-ul-Hadiyth kuwa ni mahala pa usengenyaji na uvumi na kuzungumzia kuhusu waliyosema na kufanya watu. Upotevu huanza namna hii. Tazama Dammaaj ilikuwa vipi? Kama taji. Dammaaj ilikuwa taji juu ya vichwa vya waumini. Lakini kulipitika nini wakati kulipokuja usengenyaji, uvumi, matusi, dharau na mzaha? Ilichomwa na ardhi. Ni lazima kwetu kumcha Allaah kwa ajili ya Da´wah hii. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy Chanzo: Dammaaj - Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 4-5 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Ndugu! Da´wah yetu sio ya kuvimbisha mifupa. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba sisi tunampenda mwanafunzi aliye na adabu asiyekuwa na fujo. Tunampenda na kumkubali kwa furaha. Wakati huo huo tunamchukia yule mwenye kuleta vurugu.

Dammaaj iko wapi? Hatutakiwi kuzingatia juu ya Dammaaj? Ina maana mazingatio yanatupitia pasina kuzingatia. Mawaidha yanatupitia pasina kuwaidhika. Tunamuomba Allaah kinga kutokana na kughafilika. Huku ni kughafilika, ujinga na upofu. Ni wajibu kwetu kupata mafunzo. Tazama wale waliosababisha vurugu Dammaaj! Wameifanya nini Dammaaj? Wameichoma Dammaaj na ardhi. Ni vurugu. Ni kuvimbisha mifupa. Ni upondaji wa wanachuoni. Kila mmoja anataka kujionyesha. Kila mmoja anataka kujulikana. Ninaapa kwa Allaah hili ni khatari. Ni khatari katika Da´wah, mtu mwenyewe, kundi na jamii. Hili hatulikubali. Mwanafunzi ni lazima ajilazimie kuwa na adabu kwa mwalimu wake, mwanachuoni, walinganizi na Waislamu.

Mwenye kuonesha u-Hizbiyyah wake tunamalizana naye. Tumekwishamalizana na watu wa Hizbiyyah na Ahl-ul-Bid´ah. Hatujishughulishi na wao. Tumekwishamalizana nao. Ninakumbuka maneno ya Shaykh Muqbil (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ndugu! Ninapenda maneno ya Shaykh Abu Ibraahiym Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab “Hatupotezi wakati wetu na Hizbiyyuun. Tunasema yale tulio nayo ya kusema na kusonga mbele.”

Maneno mazuri. Bainisha na songa mbele. Wewe kama mwanafunzi tilia umuhimu mkubwa wa kutafuta elimu na mhimdi Allaah Aliyekujaalia kuja katika Maraakiz hizi za Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hazikuwepo hapo kabla na mhimidi Allaah. Unatakiwa kuzihifadhi. Haitoshelezi Shaykh tu yeye mwenyewe ndiye akahifadhi nafasi hii. Shaykh wa Ma´bar, Mafraq Hubaysh, Fuyuush au Hudaydah hawezi kufanya yote. Nyote mnatakiwa kuchangia. Hii ni neema kubwa kuliko dunia nzima. Nyote mnatakiwa kuihifadhi. Moja ya njia ya kuzihifadhi ni kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maasi ni sababu ya kuwaharibu watu na miji:

فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ
“Basi nyooka kama ulivyoamrishwa na aliyetubia pamoja nawe, na wala msiruke mipaka. Hakika Yeye kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona yote daima).” (11:112-113)

Ni lazima tushikamane bara bara na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tusifanye Daar-ul-Hadiyth kuwa ni mahala pa usengenyaji na uvumi na kuzungumzia kuhusu waliyosema na kufanya watu. Upotevu huanza namna hii.

Tazama Dammaaj ilikuwa vipi? Kama taji. Dammaaj ilikuwa taji juu ya vichwa vya waumini. Lakini kulipitika nini wakati kulipokuja usengenyaji, uvumi, matusi, dharau na mzaha? Ilichomwa na ardhi. Ni lazima kwetu kumcha Allaah kwa ajili ya Da´wah hii.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
Chanzo: Dammaaj – Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 4-5
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Hajuuriy, Yahyaa
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 12th, April 2014