Nusu Ya Usiku Unaenda Kwenye Du´aa Dhidi Ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-´Adniy

Watu hawa wamejishughulisha na Shaykh ´Abdur-Rahmaan [al-´Adniy]. Allaah Amjaze kheri. Alikuwa ni mwenye subira na kimyaa. Allaah Hakumpotosha. Tazameni matunda ya kuwa na subira, adabu na utulivu. Wakati walipotumbukia kwenye vichwa vyao wakamvamia, lakini akasubiri tu. Lau wangelikuwa ni wenye kuzingatia. Ingelikuwa vizuri lau wangelipata mafunzo. Lakini wakati moyo unakuwa haupati mafunzo ina maana umegeuzwa. Kuna mtu amesema kuwa mimi ninaomba dhidi ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan [al-´Adniy] tokea 1428 (2008). Anasema kuwa yeye huugawa usiku mara mbili; nusu yake na nusu nyingine mke wake. Wanaomba dhidi ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan [al-´Adniy]. Du´aa yenu imepotea mchangani na imewasibu nyinyi wenyewe. Tokea mwaka wa 1428 usiku unagawiwa na kwa juhudi kubwa. Mwanaume na mwanamke wanaomba dhidi ya Shaykh anayelingania katika Tawhiyd, Sunnah, Fiqh na ´Aqiydah. Shaykh ni mtu wa amani. Allaah Amjaze kheri. Hataki fujo wala matatizo. Halikumdhuru na himdi zote ni Zake Allaah. Limewadhuru nyinyi wenyewe na watu mfano wenu. Kana kwamba uliomba dhidi ya mtu na Malaika akasema “Na wewe upate kadhalika”. Kila wakati ulipokuwa unaomba wewe na mke wako dhidi yake Malaika husema “Na wewe upate kadhalika”. Mkasibiwa. Kama wanavyosema uchawi umemrudilia mchawi mwenyewe. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy Chanzo: Dammaaj - Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 16 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Watu hawa wamejishughulisha na Shaykh ´Abdur-Rahmaan [al-´Adniy]. Allaah Amjaze kheri. Alikuwa ni mwenye subira na kimyaa. Allaah Hakumpotosha. Tazameni matunda ya kuwa na subira, adabu na utulivu. Wakati walipotumbukia kwenye vichwa vyao wakamvamia, lakini akasubiri tu. Lau wangelikuwa ni wenye kuzingatia. Ingelikuwa vizuri lau wangelipata mafunzo. Lakini wakati moyo unakuwa haupati mafunzo ina maana umegeuzwa.

Kuna mtu amesema kuwa mimi ninaomba dhidi ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan [al-´Adniy] tokea 1428 (2008). Anasema kuwa yeye huugawa usiku mara mbili; nusu yake na nusu nyingine mke wake. Wanaomba dhidi ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan [al-´Adniy]. Du´aa yenu imepotea mchangani na imewasibu nyinyi wenyewe. Tokea mwaka wa 1428 usiku unagawiwa na kwa juhudi kubwa. Mwanaume na mwanamke wanaomba dhidi ya Shaykh anayelingania katika Tawhiyd, Sunnah, Fiqh na ´Aqiydah. Shaykh ni mtu wa amani. Allaah Amjaze kheri. Hataki fujo wala matatizo. Halikumdhuru na himdi zote ni Zake Allaah. Limewadhuru nyinyi wenyewe na watu mfano wenu. Kana kwamba uliomba dhidi ya mtu na Malaika akasema “Na wewe upate kadhalika”. Kila wakati ulipokuwa unaomba wewe na mke wako dhidi yake Malaika husema “Na wewe upate kadhalika”. Mkasibiwa. Kama wanavyosema uchawi umemrudilia mchawi mwenyewe.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
Chanzo: Dammaaj – Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 16
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Hajuuriy, Yahyaa
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 13th, April 2014