Ni Wajibu Kwa Baba Kumuoza Kijana Wake

Kama baba anaweza kumuozesha mtoto wake wa kiume, basi analazimika kufanya hivyo kwa njia hiyo hiyo kama jinsi ni wajibu kwake kumpa nguo, chakula, kinywaji na makazi. Ni ajabu kwamba wakati mtoto wa kiume anamuomba baba yake tajiri kumuozesha, baba anajibu: "Hapana. Fanya kazi na ujifanyie mwenyewe." Subhaana Allaah! Je, ni juu ya mtoto? Je, yeye na pesa za kufanya hivyo? Kwa hiyo ndio maana mimi naona kuwa ni lazima kwa yule baba ambaye ana uwezo kumuoza mwanawe. Kama hafanyi hivyo, ni dhalimu na ni mwenye dhambi. Hili si kwangu mwenyewe. Wanachuoni wanasema namna hii. Wanasema: "Ni lazima kwa baba kuchunga heshima ya watoto vile vile kama jinsi ni wajibu kwake kupoza njaa na kiu chao." Kwa hakika ni kwamba suala la ndoa linaweza kuwa khatari. Linaweza kuathiri wengine na kuwaharibu. Kama tulivyosema, ni lazima kwa wale baba wenye uwezo kuwaoza vijana wao.

Kama baba anaweza kumuozesha mtoto wake wa kiume, basi analazimika kufanya hivyo kwa njia hiyo hiyo kama jinsi ni wajibu kwake kumpa nguo, chakula, kinywaji na makazi.

Ni ajabu kwamba wakati mtoto wa kiume anamuomba baba yake tajiri kumuozesha, baba anajibu:

“Hapana. Fanya kazi na ujifanyie mwenyewe.”

Subhaana Allaah! Je, ni juu ya mtoto? Je, yeye na pesa za kufanya hivyo? Kwa hiyo ndio maana mimi naona kuwa ni lazima kwa yule baba ambaye ana uwezo kumuoza mwanawe. Kama hafanyi hivyo, ni dhalimu na ni mwenye dhambi. Hili si kwangu mwenyewe. Wanachuoni wanasema namna hii. Wanasema:

“Ni lazima kwa baba kuchunga heshima ya watoto vile vile kama jinsi ni wajibu kwake kupoza njaa na kiu chao.”

Kwa hakika ni kwamba suala la ndoa linaweza kuwa khatari. Linaweza kuathiri wengine na kuwaharibu. Kama tulivyosema, ni lazima kwa wale baba wenye uwezo kuwaoza vijana wao.


  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. al-Liqaa' ash-Shahriy (28)
  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 17th, December 2013