Ni Nani Mwenye Kubaki Na Mtoto Wakati Wa Talaka?

Nilimwambia Ahmad bin Hanbal kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Muache mvulana achague kati ya wazazi wao." Inakuweje? Akajibu: "Wakati anapokuwa na umri wa miaka saba, anachagua. Aidha anachagua kubakia na baba au mama." Nikamuuliza inakuweje ikiwa mtoto ni mdogo? Akajibu: "Atakuwa na mama mpaka pale anapokuwa na umri wa miaka saba." Hivyo nikawa nimemuuliza ikiwa mtoto ni msichana. Akajibu: "Msichana anabaki na mama mpaka pale anapoweza kuolewa. Kisha ataenda kwa baba." Nikamuuliza ikiwa itatokea wakati yeye yuko na umri wa miaka sita. Akajibu: "Sita au saba." Nilimuuliza Ishaaq kuhusu ni muda gani mvulana na msichana watakuwa kwa mama yake mtalikiwa. Akasema: "Ninaonelea watakuwa kwa mama mpaka pale watapokuwa na umri wa miaka saba. Kisha watachagua wenyewe. " Nikamuuliza kama anaonelea kuwa wao wenyewe wachague. Akajibu: "Ndiyo, kwa ngazi ya juu." Nikamuuliza iwapo wanaweza kuchagua kabla ya kufikisha umri wa miaka saba. Akajibu: "Baadhi wanasema kuwa wanaweza kufanya hivyo wakati wako na miaka mitano. Lakini ninaoenelea wanapaswa kuwa (na umri wa miaka) saba." ´Abdur-Rahmaan bin Ghanm kasema: "Nilishuhudia jinsi 'Umar bin al-Khattwaab alimuacha kijana achague kati ya wazazi wao." al-Waliyd bin Muslim kasema: "Walizozana juu ya mvulana mbele ya Umar bin al-Khattwaab. Hivyo akamuacha mtoto achague na hivyo mtoto akachagua mama mbele ya mjomba wake. Kisha ´Umar akasema: "Wema wa mama yako ni bora zaidi kuliko utajiri wa mjomba wako."

Nilimwambia Ahmad bin Hanbal kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Muache mvulana achague kati ya wazazi wao.”

Inakuweje? Akajibu:

“Wakati anapokuwa na umri wa miaka saba, anachagua. Aidha anachagua kubakia na baba au mama.”

Nikamuuliza inakuweje ikiwa mtoto ni mdogo? Akajibu:

“Atakuwa na mama mpaka pale anapokuwa na umri wa miaka saba.”

Hivyo nikawa nimemuuliza ikiwa mtoto ni msichana. Akajibu:

“Msichana anabaki na mama mpaka pale anapoweza kuolewa. Kisha ataenda kwa baba.”

Nikamuuliza ikiwa itatokea wakati yeye yuko na umri wa miaka sita. Akajibu:

“Sita au saba.”

Nilimuuliza Ishaaq kuhusu ni muda gani mvulana na msichana watakuwa kwa mama yake mtalikiwa. Akasema:

“Ninaonelea watakuwa kwa mama mpaka pale watapokuwa na umri wa miaka saba. Kisha watachagua wenyewe. ”

Nikamuuliza kama anaonelea kuwa wao wenyewe wachague. Akajibu:

“Ndiyo, kwa ngazi ya juu.”

Nikamuuliza iwapo wanaweza kuchagua kabla ya kufikisha umri wa miaka saba. Akajibu:

“Baadhi wanasema kuwa wanaweza kufanya hivyo wakati wako na miaka mitano. Lakini ninaoenelea wanapaswa kuwa (na umri wa miaka) saba.”

´Abdur-Rahmaan bin Ghanm kasema:

“Nilishuhudia jinsi ‘Umar bin al-Khattwaab alimuacha kijana achague kati ya wazazi wao.”

al-Waliyd bin Muslim kasema:

“Walizozana juu ya mvulana mbele ya Umar bin al-Khattwaab. Hivyo akamuacha mtoto achague na hivyo mtoto akachagua mama mbele ya mjomba wake. Kisha ´Umar akasema:

“Wema wa mama yako ni bora zaidi kuliko utajiri wa mjomba wako.”


  • Author: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy. Masaail-ul-Imaam Ahmad bin Hanbal wa Ishaaq bin Raahuuyah, uk. 240
  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 31st, December 2013