Ni Nani Ana Haki Ya Kusimamisha Hadd?

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema: “Kusimamisha huduud (adhabu).” Kusimamisha adhabu sio kazi ya watu wote isipokuwa mtawala tu ambaye anatawalia mambo ya Waislamu. Yeye ndiye ana haki ya kusimamisha adhabu. Atamuua mwenye kuua, atakata mkono wa mwenye kuiba, atampiga bakora mwenye kuzini ambaye ni bikira na atampiga mawe ambaye kishaoa, atampiga bakora mwenye kunywa pombe na kumuaziri hata kama itakuwa kwa kumuua, yote haya yanafanywa na mtawala. Hana mwingine - sawa ikiwa ni mwanachuoni, muftiy wala mtu mwingine - haki ya kusimamisha adhabu, sawa kujisimamishia yeye mwenyewe wala Ummah isipokuwa tu ikiwa kama ni mtu maalum ameteuliwa na mtawala. Atafanya kazi kwa yale ambayo amepewa kwayo idhini na mtawala wa watu wote. Mfano wa watu hawa ni kama ma-Qaadhiy wanaohukumu katika mahakama ya Kishari´ah, wafanyakazi wenye kuchunga usalama na kadhalika. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah inapokuja katika masuala haya ambayo ni katika mambo ya ´Aqiydah. Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy Chanzo: Usuul-us-Sunnah Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=999&size=2h&ext=.rm

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kusimamisha huduud (adhabu).”

Kusimamisha adhabu sio kazi ya watu wote isipokuwa mtawala tu ambaye anatawalia mambo ya Waislamu. Yeye ndiye ana haki ya kusimamisha adhabu. Atamuua mwenye kuua, atakata mkono wa mwenye kuiba, atampiga bakora mwenye kuzini ambaye ni bikira na atampiga mawe ambaye kishaoa, atampiga bakora mwenye kunywa pombe na kumuaziri hata kama itakuwa kwa kumuua, yote haya yanafanywa na mtawala. Hana mwingine – sawa ikiwa ni mwanachuoni, muftiy wala mtu mwingine – haki ya kusimamisha adhabu, sawa kujisimamishia yeye mwenyewe wala Ummah isipokuwa tu ikiwa kama ni mtu maalum ameteuliwa na mtawala. Atafanya kazi kwa yale ambayo amepewa kwayo idhini na mtawala wa watu wote. Mfano wa watu hawa ni kama ma-Qaadhiy wanaohukumu katika mahakama ya Kishari´ah, wafanyakazi wenye kuchunga usalama na kadhalika. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah inapokuja katika masuala haya ambayo ni katika mambo ya ´Aqiydah.

Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy
Chanzo: Usuul-us-Sunnah
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=999&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Kukufurisha na Kuhukumu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 29th, March 2014