Ni Kweli Shaykh al-Fawzaan Anawapa Udhuru Wanaoabudu Makaburi?

Swali: Baadhi ya watu wanasema kwamba wewe unawapa udhuru wale ambao hawajafikiwa na Qur-aan wala Sunnah kama wanaoabudu makaburi kwa ujinga wao. Na je wanaoabudu makaburi wanaambiwa ni washirikina wote? al-Fawzaan: Nimesema nini? Swali: Kwamba wewe unawapa udhuru wanaoabudu makaburi... al-Fawzaan: Huu ni uongo, huu ni uongo. Mimi ninasema "Hapana", hawapewi udhuru kwa kuwa wanaishi katika mji wa Waislamu, wanasoma Qur-aan asubuhi na jioni na wanasikiliza Qur-aan. Wako na Duruus mbalimbali na idhaa na barnamiji za dini, wao sio wajinga. Lakini wao wanapuuzia. Na wanasema "sisi tupo katika yale waliyokuwemo baba zetu", hatuachi yale waliyokuwemo baba zetu na wananchi wetu. Haya ndio wanayosema. Kisha wapewe udhuru kwa ujinga?! Hapana! Mimi sikusema hivyo, huo ni uongo. Swali: Je, waambiwe kuwa ni Washirikina? Jibu: Ndio. Yule anayeabudu badala ya Allaah anaambiwa kuwa ni mshirikina. Je kuna Shirki mbali na hii kuomba badala ya Allaah?! Yule mwenye kuomba, kuchinja, kutazamia au kutaka msaada badala ya Allaah - huyu ni Mshirikina.

Swali: Baadhi ya watu wanasema kwamba wewe unawapa udhuru wale ambao hawajafikiwa na Qur-aan wala Sunnah kama wanaoabudu makaburi kwa ujinga wao. Na je wanaoabudu makaburi wanaambiwa ni washirikina wote?

al-Fawzaan: Nimesema nini?

Swali: Kwamba wewe unawapa udhuru wanaoabudu makaburi…

al-Fawzaan: Huu ni uongo, huu ni uongo. Mimi ninasema “Hapana”, hawapewi udhuru kwa kuwa wanaishi katika mji wa Waislamu, wanasoma Qur-aan asubuhi na jioni na wanasikiliza Qur-aan. Wako na Duruus mbalimbali na idhaa na barnamiji za dini, wao sio wajinga. Lakini wao wanapuuzia. Na wanasema “sisi tupo katika yale waliyokuwemo baba zetu”, hatuachi yale waliyokuwemo baba zetu na wananchi wetu. Haya ndio wanayosema. Kisha wapewe udhuru kwa ujinga?! Hapana! Mimi sikusema hivyo, huo ni uongo.

Swali: Je, waambiwe kuwa ni Washirikina?

Jibu: Ndio. Yule anayeabudu badala ya Allaah anaambiwa kuwa ni mshirikina. Je kuna Shirki mbali na hii kuomba badala ya Allaah?! Yule mwenye kuomba, kuchinja, kutazamia au kutaka msaada badala ya Allaah – huyu ni Mshirikina.