Ndio Maana Hutaki Kusema Haki

Wakati ambapo njia tofauti na walinganizi wa upotevu ni wengi, basi inakuwa ni wajibu kwa Ahl-us-Sunnah kuzidisha juhudi mara mbili katika kuibainisha haki na kuwawekea nayo wazi watu na kuwapa nasaha. Waepuke fujo. Jambo hili ni kubwa. Watu wanahitajia nasaha. Leo – na ninasema kwa ukweli kabisa – ni wachache wanaonasihi kwa ubainifu na uwazi kabisa. Fujo ndio zimekuwa nyingi na hilo linatokana na sababu kuu tatu: 1- Mzungumzaji anakhofia juu ya nafsi yake. Hataki akaja kusemwa vibaya. 2- Mzungumzaji anakhofia maslahi yake. Akizungumza haki huenda akakosa maslahi yake. 3- Mzungumzaji anataka watu wengi wamkusanyikie. Anaonelea kuwa athari yake itasibiwa ikiwa atazungumza. Sasa inajalisha nini? Umeamrishwa kubainisa haki, sio kuwakusanya watu hata kama itakuwa ni kwa batili. Pata mazingatio kwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mayahudi wamegawanyika makundi sabini na moja. Manaswara wamegawanyika makundi sabini na mbili. Na Dini hii itakuja kugawanyika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni lipi hilo, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni lile litakalofuata yale ambayo mimi na Maswahabah wangu waliyomo hivi leo.” Haya ni mapokezi mengine. Yamekuja “Dini”. Hii ni Radd kubwa kwa wapotevu wanaosema kuwa mgawanyiko inahusiana na watu wote ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumwa kwao na sio wale walioitikia. Wanachotaka ni kuyatetea mapote potevu na hivyo waweze kuyaingiza katika Uislamu na Ahl-us-Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Na Dini hii itakuja kugawanyika katika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Bi maana Ummah wake. Katika mapokezi mengine imekuja: “Mayahudi wamegawanyika katika makundi sabini na moja. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja. Manaswara wamegawanyika katika makundi sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja. Na Ummah huu utakuja kugawanyika katika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Ni wachache ndio wataokoka na ni wengi ndio wataangamia. Hii ni Radd bora kwa yule anayesema ikiwa atazungumza watu watakuja kumuacha. Wana faida gani na wewe sasa ikiwa kama hawafaidiki na elimu yako na kuwaelekeza katika Dini ya Allaah?

Wakati ambapo njia tofauti na walinganizi wa upotevu ni wengi, basi inakuwa ni wajibu kwa Ahl-us-Sunnah kuzidisha juhudi mara mbili katika kuibainisha haki na kuwawekea nayo wazi watu na kuwapa nasaha. Waepuke fujo. Jambo hili ni kubwa. Watu wanahitajia nasaha.

Leo – na ninasema kwa ukweli kabisa – ni wachache wanaonasihi kwa ubainifu na uwazi kabisa. Fujo ndio zimekuwa nyingi na hilo linatokana na sababu kuu tatu:

1- Mzungumzaji anakhofia juu ya nafsi yake. Hataki akaja kusemwa vibaya.

2- Mzungumzaji anakhofia maslahi yake. Akizungumza haki huenda akakosa maslahi yake.

3- Mzungumzaji anataka watu wengi wamkusanyikie. Anaonelea kuwa athari yake itasibiwa ikiwa atazungumza. Sasa inajalisha nini? Umeamrishwa kubainisa haki, sio kuwakusanya watu hata kama itakuwa ni kwa batili. Pata mazingatio kwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mayahudi wamegawanyika makundi sabini na moja. Manaswara wamegawanyika makundi sabini na mbili. Na Dini hii itakuja kugawanyika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni lipi hilo, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni lile litakalofuata yale ambayo mimi na Maswahabah wangu waliyomo hivi leo.”

Haya ni mapokezi mengine. Yamekuja “Dini”. Hii ni Radd kubwa kwa wapotevu wanaosema kuwa mgawanyiko inahusiana na watu wote ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumwa kwao na sio wale walioitikia. Wanachotaka ni kuyatetea mapote potevu na hivyo waweze kuyaingiza katika Uislamu na Ahl-us-Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Na Dini hii itakuja kugawanyika katika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.”
Bi maana Ummah wake. Katika mapokezi mengine imekuja:

“Mayahudi wamegawanyika katika makundi sabini na moja. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja. Manaswara wamegawanyika katika makundi sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja. Na Ummah huu utakuja kugawanyika katika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.”

Ni wachache ndio wataokoka na ni wengi ndio wataangamia. Hii ni Radd bora kwa yule anayesema ikiwa atazungumza watu watakuja kumuacha. Wana faida gani na wewe sasa ikiwa kama hawafaidiki na elimu yako na kuwaelekeza katika Dini ya Allaah?