Ndio Maana Ahl-ul-Bid´ah Wanapiga Kelele Juu Ya Da´wah Ya Salafiyyah

Kulingania katika Dini ya Allaah ndio kazi ya Mitume: يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا “Ee Nabii! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji. Na mlinganiaji kwa Allaah kwa Idhini Yake; na siraji yenye kun'gara.” (33:45-46” Ni kazi ya Mitume. Wewe, ndugu yangu kutoka Indonesia, unataka kulingania katika Dini ya Allaah bila ya kuudhiwa na kutukanywa kama jinsi walivyotukanywa Mitume na walinganiaji katika Dini ya Allaah (Ta´ala): الم أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ” Alif Laam Miym. Je, wanadhani watu kwamba wataachwa (bila ya misukosuko kwa kuwa) wanasema: “Tumeamini.” basi ndio wasijaribiwe? Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao, ili Allaah Awatambulishe wale walio wakweli na ili Awatambulishe waongo.” (29:2-3) Wanapiga kelele kwa sababu Da´wah yenu inapata nafasi imara. Kwa kuwa Da´wah ya Ahl-us-Sunnah wao wanalingania watu katika yale yanayowanufaisha: قُلْ مَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ “Sema: “Ujira wowote niliokuombeni (ikiwa nimekuombeni kweli), basi huo ni wenu; sina ujira ila kwa Allaah tu. Naye juu ya kila kitu niShahiyd (Mwenye kushuhudia yote daima).” (34:47) Hawawalinganii watu katika kuwafuata kichwa mchunga. Wao wanasema hawastahiki kufuatwa kichwa mchunga. Lau tungelikuwa tunawaita watu kutufuata kichwa mchunga basi tungeliwaita wamfuate kichwa mchunga Ahmad bin Hanbal, ´Aliy bin Abiy Twaalib au Abu Bakr asw-Swiddiyq. Lakini wao wanalingania katika Qur-aan na Sunnah. Tunawapa bishara njema ya kuwa Da´wah yenu itakuja kuizunguka Indonesia yote kwa idhini ya Allaah. Kwa nini? Kwa kuwa watu wanaona tofauti. Kuna tofauti kati ya Da´wah iliyojengaka juu ya maslahi na Da´wah inayotaka tu kuwanufaisha Waislanu.

Kulingania katika Dini ya Allaah ndio kazi ya Mitume:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا
“Ee Nabii! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji. Na mlinganiaji kwa Allaah kwa Idhini Yake; na siraji yenye kun’gara.” (33:45-46”

Ni kazi ya Mitume. Wewe, ndugu yangu kutoka Indonesia, unataka kulingania katika Dini ya Allaah bila ya kuudhiwa na kutukanywa kama jinsi walivyotukanywa Mitume na walinganiaji katika Dini ya Allaah (Ta´ala):

الم أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ
” Alif Laam Miym. Je, wanadhani watu kwamba wataachwa (bila ya misukosuko kwa kuwa) wanasema: “Tumeamini.” basi ndio wasijaribiwe? Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao, ili Allaah Awatambulishe wale walio wakweli na ili Awatambulishe waongo.” (29:2-3)

Wanapiga kelele kwa sababu Da´wah yenu inapata nafasi imara. Kwa kuwa Da´wah ya Ahl-us-Sunnah wao wanalingania watu katika yale yanayowanufaisha:

قُلْ مَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ
“Sema: “Ujira wowote niliokuombeni (ikiwa nimekuombeni kweli), basi huo ni wenu; sina ujira ila kwa Allaah tu. Naye juu ya kila kitu niShahiyd (Mwenye kushuhudia yote daima).” (34:47)

Hawawalinganii watu katika kuwafuata kichwa mchunga. Wao wanasema hawastahiki kufuatwa kichwa mchunga. Lau tungelikuwa tunawaita watu kutufuata kichwa mchunga basi tungeliwaita wamfuate kichwa mchunga Ahmad bin Hanbal, ´Aliy bin Abiy Twaalib au Abu Bakr asw-Swiddiyq. Lakini wao wanalingania katika Qur-aan na Sunnah.

Tunawapa bishara njema ya kuwa Da´wah yenu itakuja kuizunguka Indonesia yote kwa idhini ya Allaah. Kwa nini? Kwa kuwa watu wanaona tofauti. Kuna tofauti kati ya Da´wah iliyojengaka juu ya maslahi na Da´wah inayotaka tu kuwanufaisha Waislanu.