Nasaha Kwa Wale Wanaofanya Na Kufanyiwa Ruqyah

´Allaamah al-Fawzaan: Hivyo inatakiwa kwa yule ambaye amesibiwa na anataka kufanyiwa ruqyah, asimuendee kila mtu - mtu ni mtu akamuendea. Bali asimuendee ila yule ambaye ni maarufu anapopita na kutoa [vitu vyake], Na awe maarufu kwa ´Aqiydah yake, awe na ´Aqiydah sahihi. Na awe ni maarufu kwa elimu yake pia. Hafanyi mambo ambayo yanakhalifu Shari´ah. Ni sharti kwa mwenye kusoma Ruqyah ashikamane na sharti hizi. Ama [wasomaji] wakiwa ni wajinga, [hakujulikani] wanapita wapi na wametokea wapi. Au kunajulikana wanapopita lakini hawana elimu wala ujuzi wa Ruqyah na hukumu zake, au anajulikana kuwa ana mambo yanayokwenda kinyume na ´Aqiydah. Watu wote hawa haijuzu kuwaendea. Baya zaidi ikiwa ni katika wachawi na makuhani na wanaotumia majini.Amesema Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam: "Atakayemwendea kuhani akamsadikisha kwa alichosema, amekufuru kwa yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)." Na kasema tena Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam: "Atakayemwendea kuhani, hatokubaliwa Swalah zake kwa siku arubaini." (Swahiyh Muslim)

´Allaamah al-Fawzaan:

Hivyo inatakiwa kwa yule ambaye amesibiwa na anataka kufanyiwa ruqyah, asimuendee kila mtu – mtu ni mtu akamuendea. Bali asimuendee ila yule ambaye ni maarufu anapopita na kutoa [vitu vyake], Na awe maarufu kwa ´Aqiydah yake, awe na ´Aqiydah sahihi. Na awe ni maarufu kwa elimu yake pia. Hafanyi mambo ambayo yanakhalifu Shari´ah. Ni sharti kwa mwenye kusoma Ruqyah ashikamane na sharti hizi. Ama [wasomaji] wakiwa ni wajinga, [hakujulikani] wanapita wapi na wametokea wapi. Au kunajulikana wanapopita lakini hawana elimu wala ujuzi wa Ruqyah na hukumu zake, au anajulikana kuwa ana mambo yanayokwenda kinyume na ´Aqiydah. Watu wote hawa haijuzu kuwaendea. Baya zaidi ikiwa ni katika wachawi na makuhani na wanaotumia majini.Amesema Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam:

“Atakayemwendea kuhani akamsadikisha kwa alichosema, amekufuru kwa yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Na kasema tena Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam:

“Atakayemwendea kuhani, hatokubaliwa Swalah zake kwa siku arubaini.” (Swahiyh Muslim)