Namna Hii Wanatakiwa Wanafunzi Kuwa

Haijuzu kuwa shabaki wa watu wala kuwatukuza. Wanaume wanajulikana kwa haki. Haki haijulikani kwa wanaume. Nitawaeleza tukio na Shaykh wetu Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy (Rahimahu Allaah). Lilitokea wakati nilipomtembelea mwezi mmoja na nusu kabla ya kufa kwake. Baada ya kumsalimia baadhi ya watu wakaanza kunitambulisha kwake. Akasema: “Mnanitambulisha mtu anayejadili juu ya kufunga Jumamosi na kuswali Jamaa´ah ya pili [msikitini]?” Nikamwambia: “Natofautiana na wewe mimi bado nimeshikamana na rai hii kuwa inajuzu kuswali Jamaa´ah ya pili na kufunga Jumamosi ilimradi haifungwi pekee. Wewe ndio umetufunza hivi.” Akaufinya mkono wangu (Rahimahu Allaah) na sintosahau kunishika kwake kwa nguvu wakati ule. Akasema: “Namna hii ndio ninavyotaka wanafunzi wawe. Wasiwe na ushabiki kwangu wala kwa mwengine. Allaah Akujaze kheri.” Nilikuwepo wakati Shaykh wetu ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad alipojadiliana naye. Wote wawili walikuwa wakiheshimiana sana. Walijadiliana juu ya kukata chenye kuzidi juu ya kiganja. Hii ni rai aliokuwa nayo Shaykh [al-Albaaniy] kutokana na mapokezi kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar (Rahimahu Allaah). Tuliburudika kwa mjadala huu uliofanyika karibu saa mbili na ulikuwa kwa heshima ya hali ya juu. Shaykh Muhammad Naaswir-ur-Diyn al-Albaaniy na Shaykh wetu Hamuud at-Tuwayjiriy (Rahimahu Allaah) walipigana Radd za nguvu kuhusiana na masuala ya Hijaab. Pamoja na hivyo walikuwa wakitukuzana pindi wanapokutana na wakati mmoja anapopata jibu anamwomba mwengine alijibu. Wanachuoni hawa wamekufa. Kulitokea upenyo mkubwa walipofariki.

Haijuzu kuwa shabaki wa watu wala kuwatukuza. Wanaume wanajulikana kwa haki. Haki haijulikani kwa wanaume.

Nitawaeleza tukio na Shaykh wetu Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy (Rahimahu Allaah). Lilitokea wakati nilipomtembelea mwezi mmoja na nusu kabla ya kufa kwake. Baada ya kumsalimia baadhi ya watu wakaanza kunitambulisha kwake. Akasema:

“Mnanitambulisha mtu anayejadili juu ya kufunga Jumamosi na kuswali Jamaa´ah ya pili [msikitini]?”
Nikamwambia:

“Natofautiana na wewe mimi bado nimeshikamana na rai hii kuwa inajuzu kuswali Jamaa´ah ya pili na kufunga Jumamosi ilimradi haifungwi pekee. Wewe ndio umetufunza hivi.”

Akaufinya mkono wangu (Rahimahu Allaah) na sintosahau kunishika kwake kwa nguvu wakati ule. Akasema:

“Namna hii ndio ninavyotaka wanafunzi wawe. Wasiwe na ushabiki kwangu wala kwa mwengine. Allaah Akujaze kheri.”

Nilikuwepo wakati Shaykh wetu ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad alipojadiliana naye. Wote wawili walikuwa wakiheshimiana sana. Walijadiliana juu ya kukata chenye kuzidi juu ya kiganja. Hii ni rai aliokuwa nayo Shaykh [al-Albaaniy] kutokana na mapokezi kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar (Rahimahu Allaah). Tuliburudika kwa mjadala huu uliofanyika karibu saa mbili na ulikuwa kwa heshima ya hali ya juu.

Shaykh Muhammad Naaswir-ur-Diyn al-Albaaniy na Shaykh wetu Hamuud at-Tuwayjiriy (Rahimahu Allaah) walipigana Radd za nguvu kuhusiana na masuala ya Hijaab. Pamoja na hivyo walikuwa wakitukuzana pindi wanapokutana na wakati mmoja anapopata jibu anamwomba mwengine alijibu.

Wanachuoni hawa wamekufa. Kulitokea upenyo mkubwa walipofariki.