Na Akaja Mola Wako Na Malaika Safu Safu

Allaah (Subhanahu wa Ta'ala) Kasema: وجاء ربك والملك صفا صفا ”Na akaja Mola Wako na Malaika safu safu.” Yaani (Akaja) kuwahukumu viumbe Wake. Hili litafanyika baada ya viumbe kumuomba kiongozi wa wanaadamu, Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), kumuomba Allaah (asimamishe Qiyaamah). Kabla ya hapo, waliwaomba Mitume wengine wanne wakubwa. Wote wataomba radhi na kusema: "Sina haki ya hilo." Hatimaye, wataenda kwa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye atasema: "Mimi ndiye mwenye haki ya hilo! Nina haki ya hilo!" Atamuomba Allaah (Ta´ala) ili aje (ya'tiy) kuwahukumu [viumbe]. Namna hii ndivyo Allaah Atamruhusu suala hili. Hii ndio itakuwa Shafaa´ah (uombezi) ya kwanza na huitwa "cheo kinachosifika" (al-Maqaam al-Mahmuud). Hapo ndipo Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atakuja (yajiy') Kuhukumu vile Apendavyo. Wakati wa tukio hili, Malaika watakuja (yaji´uun) mbele Yake safu safu. Mwandishi: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (4/657-658) Mu’assasah ar-Risaalah, 1422/2001

Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Kasema:

وجاء ربك والملك صفا صفا
”Na akaja Mola Wako na Malaika safu safu.”

Yaani (Akaja) kuwahukumu viumbe Wake. Hili litafanyika baada ya viumbe kumuomba kiongozi wa wanaadamu, Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), kumuomba Allaah (asimamishe Qiyaamah). Kabla ya hapo, waliwaomba Mitume wengine wanne wakubwa. Wote wataomba radhi na kusema:

“Sina haki ya hilo.”

Hatimaye, wataenda kwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ambaye atasema:
“Mimi ndiye mwenye haki ya hilo! Nina haki ya hilo!”

Atamuomba Allaah (Ta´ala) ili aje (ya’tiy) kuwahukumu [viumbe]. Namna hii ndivyo Allaah Atamruhusu suala hili.

Hii ndio itakuwa Shafaa´ah (uombezi) ya kwanza na huitwa “cheo kinachosifika” (al-Maqaam al-Mahmuud). Hapo ndipo Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atakuja (yajiy’) Kuhukumu vile Apendavyo. Wakati wa tukio hili, Malaika watakuja (yaji´uun) mbele Yake safu safu.

Mwandishi: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (4/657-658)
Mu’assasah ar-Risaalah, 1422/2001


  • Kitengo: Uncategorized , Kuja kwa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013