Mwanamke Wa Kiislamu Anafanya Kazi Zaidi Ya Wanaume

Mashaytwaan wanasema kuwa nusu ya jamii itakuwa ni yenye kukosa kazi kwa kuwa mwanamke ni nusu ya jamii. Ikiwa mwanamke hatofanya kazi pamoja na wanaume nusu ya jamii itakosa kazi. Maneno yasiyokuwa na maana. Ni wasiwasi usiokuwa wa usalama na hoja ya kutupwa. Ni nani mwenye kusema ya kwamba mwanamke amekosa kazi? Wanawake wetu na wanawake katika jamii ya Kiislamu sio wenye kukosa kazi hata kidogo. Anafanya kazi zaidi kuliko wanaume. Anafanya mambo ambayo mwanaume hawezi. Ni nani mwenye kuijenga familia? Ni nani mwenye kuwalea watoto? Ni nani mwenye kupika chakula na kupanga na kusafisha nyumba? Ni nani mwenye kufanya mambo yote nyumbani? Ni nani atakayefanya kazi ya mwanamke ikiwa ataenda nje kwenye barabara na kuanza kufanya kazi pamoja na wanaume? Ni nani atakayefanya hayo ikiwa mwanaume na mwanamke wote wawili wanafanya kazi nje ya nyumba? Je, nyumbani sio nusu ya maisha na pengine hata ikawa zaidi ya hivyo? Kufanya kazi nje ya nyumba ndio uwanja wa kazi ya mwanaume. Kufanya kazi ndani ya nyumba ndio uwanja wa kazi ya mwanamke. Ina maana nusu ya jamii inashughulika na sio yenye kukosa kazi kabisa. Lakini watu hawa wanajaribu kudanganya na kuficha khatari. Mwanamke sio mwenye kukosa kazi kabisa. Mwanamke ana jukumu kubwa katika jamii ambayo hakuna mwingine yeyote anayeiweza. Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: Makaanat-ul-Mar'ah fiyl-Islaam, uk. 556-557 Majmuu´atu Rasaail Da´wiyyah wa Manhajiyyah

Mashaytwaan wanasema kuwa nusu ya jamii itakuwa ni yenye kukosa kazi kwa kuwa mwanamke ni nusu ya jamii. Ikiwa mwanamke hatofanya kazi pamoja na wanaume nusu ya jamii itakosa kazi. Maneno yasiyokuwa na maana. Ni wasiwasi usiokuwa wa usalama na hoja ya kutupwa. Ni nani mwenye kusema ya kwamba mwanamke amekosa kazi? Wanawake wetu na wanawake katika jamii ya Kiislamu sio wenye kukosa kazi hata kidogo. Anafanya kazi zaidi kuliko wanaume. Anafanya mambo ambayo mwanaume hawezi.

Ni nani mwenye kuijenga familia?

Ni nani mwenye kuwalea watoto?

Ni nani mwenye kupika chakula na kupanga na kusafisha nyumba?

Ni nani mwenye kufanya mambo yote nyumbani?

Ni nani atakayefanya kazi ya mwanamke ikiwa ataenda nje kwenye barabara na kuanza kufanya kazi pamoja na wanaume? Ni nani atakayefanya hayo ikiwa mwanaume na mwanamke wote wawili wanafanya kazi nje ya nyumba?

Je, nyumbani sio nusu ya maisha na pengine hata ikawa zaidi ya hivyo? Kufanya kazi nje ya nyumba ndio uwanja wa kazi ya mwanaume. Kufanya kazi ndani ya nyumba ndio uwanja wa kazi ya mwanamke. Ina maana nusu ya jamii inashughulika na sio yenye kukosa kazi kabisa. Lakini watu hawa wanajaribu kudanganya na kuficha khatari. Mwanamke sio mwenye kukosa kazi kabisa. Mwanamke ana jukumu kubwa katika jamii ambayo hakuna mwingine yeyote anayeiweza.

Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Makaanat-ul-Mar’ah fiyl-Islaam, uk. 556-557
Majmuu´atu Rasaail Da´wiyyah wa Manhajiyyah


  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 16th, January 2014