Mwanamke Wa Hedhi Kuoga Kwa Ajili Ya Hadathi Ya Janaba

Ikiwa mwanamke mwenye hedhi ana hadathi ya janaba, haimlazimikii kuoga (Ghusl) mpaka kipindi chake kiishe. Hili limesemwa na Ahmad na ni rai ya Ishaaq. Kauli hii imejengeka juu ya kwamba kuoga ni bure katika hali hii. Lakini ikiwa ataoga kwa kuwa yuko na janaba wakati wa kipindi chake, inachukuliwa kuoga kwake ni sahihi na ni sawa. Vilevile hazingatiwi kuwa yuko na hadathi ya janaba tena. Hili limesemwa na Ahmad. Kasema: "Janaba yake inapungua tofauti na kipindi chake ambacho kinaendelea mpaka pale damu itakapokatika. Sijui kama kuna mtu mwingine zaidi ya ´Atwaa´ aliyesema ya kwamba hatakiwi kuoga. Alisema kwamba hedhi ni kubwa. Kisha baadaye akajirudi kwa kauli hii na kusema ya kwamba anatakiwa kuoga." Kwa ajili tu yuko na hadathi mbili [kubwa], haimaanishi ya kwamba [hadathi] moja haiwezi kusitishwa. Mfano wa hilo ni pale ambapo mtu ataoga kwa sababu ya hadathi ndogo.

Ikiwa mwanamke mwenye hedhi ana hadathi ya janaba, haimlazimikii kuoga (Ghusl) mpaka kipindi chake kiishe. Hili limesemwa na Ahmad na ni rai ya Ishaaq. Kauli hii imejengeka juu ya kwamba kuoga ni bure katika hali hii. Lakini ikiwa ataoga kwa kuwa yuko na janaba wakati wa kipindi chake, inachukuliwa kuoga kwake ni sahihi na ni sawa. Vilevile hazingatiwi kuwa yuko na hadathi ya janaba tena. Hili limesemwa na Ahmad. Kasema:

“Janaba yake inapungua tofauti na kipindi chake ambacho kinaendelea mpaka pale damu itakapokatika. Sijui kama kuna mtu mwingine zaidi ya ´Atwaa´ aliyesema ya kwamba hatakiwi kuoga. Alisema kwamba hedhi ni kubwa. Kisha baadaye akajirudi kwa kauli hii na kusema ya kwamba anatakiwa kuoga.”

Kwa ajili tu yuko na hadathi mbili [kubwa], haimaanishi ya kwamba [hadathi] moja haiwezi kusitishwa. Mfano wa hilo ni pale ambapo mtu ataoga kwa sababu ya hadathi ndogo.


  • Author: Shaykh-ul-Islaam Ibn Qudaamah al-Maqdisiy. (al-Mughniy)
  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 9th, January 2014