Mwanamke Kufunua Sehemu Ya Chini Wakati Wa Jimaa

137- Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema: "Wakati mwanamke wa kiyahudi alipokuwa anapata hedhi, mayahudi walikuwa wakiacha kula naye." Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa amesema: "Fanya kila kitu isipokuwa jimaa." Imepokelewa na Muslim. Maana yake ni kwamba inajuzu kustarehe na mwanamke wakati ana hedhi maadamu mtu hafanyi naye jimaa. Anaweza kumbusu, kumkumbatia na kuingiza uume wake kati ya mapaja yake. Anaweza kufanya kila kitu maadamu hafanyi naye jimaa. Je, ni lazima kwake mke kujifunika mwili wake ikiwa mume anataka kusugua mwili wake kwake? Hapana, sio lazima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitaja tendo hili pasina kizuizi. Anaweza kusugua mwili wake kwake bila ya yeye (mke) kufunika mwili wake. Hata hivyo ni bora kwake kufunika (maeneo ya uke wake) kutokana na sababu mbili: 1- Pengine akashindwa kuimiliki nafsi yake ikiwa hakufunika sehemu ya siri na hivyo akafanya naye jimaa kwenye uke wake. 2- Ili asione atakayoyadharau kutoka kwenye damu yake.

137- Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

“Wakati mwanamke wa kiyahudi alipokuwa anapata hedhi, mayahudi walikuwa wakiacha kula naye.” Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa amesema: “Fanya kila kitu isipokuwa jimaa.”

Imepokelewa na Muslim.

Maana yake ni kwamba inajuzu kustarehe na mwanamke wakati ana hedhi maadamu mtu hafanyi naye jimaa. Anaweza kumbusu, kumkumbatia na kuingiza uume wake kati ya mapaja yake. Anaweza kufanya kila kitu maadamu hafanyi naye jimaa.

Je, ni lazima kwake mke kujifunika mwili wake ikiwa mume anataka kusugua mwili wake kwake? Hapana, sio lazima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitaja tendo hili pasina kizuizi. Anaweza kusugua mwili wake kwake bila ya yeye (mke) kufunika mwili wake. Hata hivyo ni bora kwake kufunika (maeneo ya uke wake) kutokana na sababu mbili:

1- Pengine akashindwa kuimiliki nafsi yake ikiwa hakufunika sehemu ya siri na hivyo akafanya naye jimaa kwenye uke wake.

2- Ili asione atakayoyadharau kutoka kwenye damu yake.


  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. Fath Dhiyl-Jalaal wal-Ikraam (1/712)
  • Kitengo: Uncategorized , Familia
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 7th, January 2014