Mwanamke Anatakiwa Kupaka Mikono Yake Hina

Muhammad bin Muhammad as-Sawriy ametuhadithia: Khaalid bin 'Abdir-Rahmaan ametuhadithia: Mutiy' bin Maymuun ametuhadithia, kutoka kwa Safiyyah bint 'Ismah, kutoka kwa 'Aaishah ambaye amesema: "Mwanamke aliashiria kwa mkono wake nyuma ya pazia. Mkononi alikuwa na barua ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akaichukua na kusema: "Je, huu ni mkono wa mwanaume au mkono wa mwanamke?" Akasema (mwanamke yule): "Ni mkono wa mwanamke." Hivyo akasema (Mtume): "Kama ungelikuwa mwanamke, ungelibadili makucha yako" - bi maana kwa hina." UFAFANUZI "Kama ungelikuwa mwanamke..." - Bi maana kama ungetilia uzito juu ya tabia ya mwanamke. "... ungelibadili makucha yako... " - Bi maana kuyatia rangi. "... bi maana kwa hina." - Haya aidha ni maneno ya Aaishah au mtu mwingine miongoni mwa wapokezi. Katika Hadiyth hii kuna dalili ya kwamba ni imependekezwa [mustahab] sana kwa wanawake kutumia hina. Mwandishi: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy (d. 275) Chanzo: as-Sunan (4160) Mfafanuaji: Imaam Shams-ul-Haqq al-´Adhiymaabaadiy Chanzo: ´Awn-ul-Ma´buud (11/149)

Muhammad bin Muhammad as-Sawriy ametuhadithia: Khaalid bin ‘Abdir-Rahmaan ametuhadithia: Mutiy’ bin Maymuun ametuhadithia, kutoka kwa Safiyyah bint ‘Ismah, kutoka kwa ‘Aaishah ambaye amesema:

“Mwanamke aliashiria kwa mkono wake nyuma ya pazia. Mkononi alikuwa na barua ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akaichukua na kusema: “Je, huu ni mkono wa mwanaume au mkono wa mwanamke?” Akasema (mwanamke yule): “Ni mkono wa mwanamke.” Hivyo akasema (Mtume): “Kama ungelikuwa mwanamke, ungelibadili makucha yako” – bi maana kwa hina.”

UFAFANUZI

“Kama ungelikuwa mwanamke…” – Bi maana kama ungetilia uzito juu ya tabia ya mwanamke.

“… ungelibadili makucha yako… ” – Bi maana kuyatia rangi.

“… bi maana kwa hina.” – Haya aidha ni maneno ya Aaishah au mtu mwingine miongoni mwa wapokezi. Katika Hadiyth hii kuna dalili ya kwamba ni imependekezwa [mustahab] sana kwa wanawake kutumia hina.

Mwandishi: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy (d. 275)
Chanzo: as-Sunan (4160)
Mfafanuaji: Imaam Shams-ul-Haqq al-´Adhiymaabaadiy
Chanzo: ´Awn-ul-Ma´buud (11/149)


  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 6th, January 2014