Mwanafunzi Mwenye Maendeleo

Usisababishe maradhi ya moyo wako. Jiweke mbali na mtu ambaye anataka kuzungumza na wewe na kusababisha maradhi ya moyo wako. Mwambie mimi nimekuja huku kwa ajili ya kuusafisha moyo wangu na hukuja kwa ajili ya kuuchafua. Tazama baadhi ya watu Dammaaj! Tazama kulipitika nini wakati walipoanza kusikiliza usengenyaji. Walisikiliza usengenyaji mpaka wakatumbukia katika chuki, vifundo na kujigawa vikundikundi na Dammaaj ikaangamia. Itakuja kurudi – in shaa Allaah – wakati kheri na neema itarudi. Mimi ninawanasihi wasimamizi wa Maraakiz – sawa ikiwa ni Shaykh ´Abdur-Rahmaan [al-´Adniy], Shaykh [Muhammad] al-Imaam, Shaykh [´Abdul-´Aziyz] al-Bura´iy, Shaykh ´Abdullaah bin Mar´iy [al-´Adniy] Shihr na wasimamizi wengine wote wa Maraakiz kama ndugu yetu Abu ´Ammaar kwetu Hudaydah, Ahmad bin Saalim Husayniyyah, Shaykh Hasan ´Ilyaawah Shabwah na wengine – kuzihifadhi Maraakiz zao na kamwe wasikubali vurugu kwa mwanachuoni yeyote. Sisi tunawaheshimu wanachuoni wote. Tunawaheshimu wanachuoni wa Hijaaz, Najd na wanachuoni wengine wote duniani maadamu wameshikamana na Qur-aan na Sunnah. Tunawaheshimu, tunawapa hadhi na stahi yao. Kadhalika wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah Yemen. Tunawachukua kwa furaha. Hatukubali mwanachuoni yeyote akapondwa au kutukanywa. Haijalishi ikiwa anatoka Yemen, Hijaaz, Najd, Misri, Sudan au sehemu nyingine yoyote. Vipi tutakubali wanachuoni wakapondwa na kutukanywa wakati haturuhusu hata ´Awwaam kutukanywa na kupondwa? Tukimuona mtu anamponda na kumfanyia mzaha mwengine tunamwambia amche Allaah na anyamaze. Wewe ni mwanafunzi. Hivyo jipambe kama jinsi elimu inavosema. Ama kuhusu walinganizi na wanachuoni, wao ni aula zaidi. Ama kuhusiana na Hizbiyyuun, nimeshawaambia kwamba sisi tunajiweka mbali kwa Allaah kutokana na kila mwenye kwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Kila mmoja kwa kiasi cha upindaji wake. Hatukubali katika safu zetu isipokuwa watu walio na adabu ambao hawashtaki na hakuna yeyote anayemshtaki. Huyu ana tabia na adabu nzuri. Amejishughulisha na duruus zake, kuhifadhi, kuandika, kupangilia masomo yake, kufanya marudilio, analingania katika Dini ya Allaah, anashirikiana katika kulingania katika Dini ya Allaah na kuwafunza ndugu zake. Huyu ni mtu mwenye maendeleo. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy Chanzo: Dammaaj - Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 6-7 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Usisababishe maradhi ya moyo wako. Jiweke mbali na mtu ambaye anataka kuzungumza na wewe na kusababisha maradhi ya moyo wako. Mwambie mimi nimekuja huku kwa ajili ya kuusafisha moyo wangu na hukuja kwa ajili ya kuuchafua. Tazama baadhi ya watu Dammaaj! Tazama kulipitika nini wakati walipoanza kusikiliza usengenyaji. Walisikiliza usengenyaji mpaka wakatumbukia katika chuki, vifundo na kujigawa vikundikundi na Dammaaj ikaangamia. Itakuja kurudi – in shaa Allaah – wakati kheri na neema itarudi.

Mimi ninawanasihi wasimamizi wa Maraakiz – sawa ikiwa ni Shaykh ´Abdur-Rahmaan [al-´Adniy], Shaykh [Muhammad] al-Imaam, Shaykh [´Abdul-´Aziyz] al-Bura´iy, Shaykh ´Abdullaah bin Mar´iy [al-´Adniy] Shihr na wasimamizi wengine wote wa Maraakiz kama ndugu yetu Abu ´Ammaar kwetu Hudaydah, Ahmad bin Saalim Husayniyyah, Shaykh Hasan ´Ilyaawah Shabwah na wengine – kuzihifadhi Maraakiz zao na kamwe wasikubali vurugu kwa mwanachuoni yeyote.

Sisi tunawaheshimu wanachuoni wote. Tunawaheshimu wanachuoni wa Hijaaz, Najd na wanachuoni wengine wote duniani maadamu wameshikamana na Qur-aan na Sunnah. Tunawaheshimu, tunawapa hadhi na stahi yao. Kadhalika wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah Yemen. Tunawachukua kwa furaha. Hatukubali mwanachuoni yeyote akapondwa au kutukanywa. Haijalishi ikiwa anatoka Yemen, Hijaaz, Najd, Misri, Sudan au sehemu nyingine yoyote. Vipi tutakubali wanachuoni wakapondwa na kutukanywa wakati haturuhusu hata ´Awwaam kutukanywa na kupondwa? Tukimuona mtu anamponda na kumfanyia mzaha mwengine tunamwambia amche Allaah na anyamaze. Wewe ni mwanafunzi. Hivyo jipambe kama jinsi elimu inavosema. Ama kuhusu walinganizi na wanachuoni, wao ni aula zaidi.

Ama kuhusiana na Hizbiyyuun, nimeshawaambia kwamba sisi tunajiweka mbali kwa Allaah kutokana na kila mwenye kwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Kila mmoja kwa kiasi cha upindaji wake. Hatukubali katika safu zetu isipokuwa watu walio na adabu ambao hawashtaki na hakuna yeyote anayemshtaki. Huyu ana tabia na adabu nzuri. Amejishughulisha na duruus zake, kuhifadhi, kuandika, kupangilia masomo yake, kufanya marudilio, analingania katika Dini ya Allaah, anashirikiana katika kulingania katika Dini ya Allaah na kuwafunza ndugu zake. Huyu ni mtu mwenye maendeleo.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
Chanzo: Dammaaj – Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 6-7
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Hajuuriy, Yahyaa
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 12th, April 2014