Mwanafunzi Hamtangulii Mwanachuoni

Katika usiku huu wa 15 Shawwaal mwaka wa 1435 nitazungumzia kuhusu mkataba kati ya Shaykh Muhammad al-Imaam na ´Abdul-Maalik al-Hawthiy. Nina baadhi ya nasaha na maelekezo. Kwanza ninawanasihi wanafunzi na watu wa kawaida kutowatangulia wanachuoni. Fanyeni hilo kuwa ni kanuni ya jumla katika majanga yote. Wasitanguliwe wanachuoni. Wajipambe kwa adabu za Kishari´ah. Wanyamaze na wasubiri maneno ya wanachuoni wao wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ “Enyi mlioamini! Msitangulie mbele ya Allaah na Mtume Wake. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima - Mjuzi wa yote daima).” (49:01) Wanachuoni ndio warithi wa Mitume. Kama jinsi Maswahabah walivyokatazwa kutangulia mbele ya Allaah na Mtume Wake hali kadhalika linawahusu waliokuja baada ya Maswahabah wamekatazwa kutangulia mbele ya wanachuoni. Wanachuoni ndio wanatakiwa kuwa wa kwanza kuzungumza na sio wanafunzi wala watu wa kawaida. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amesema: وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا “Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Mtume na kwa wenye madaraka kati yao, wale (Wanavyuoni) wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua. Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na Rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan (nyote) ila wachache tu.” (04:83) Allaah Amewakataza kueneza uvumi na kuwaamrisha kurejea kwa wanachuoni: لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا “... wale (Wanavyuoni) wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua. Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na Rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan (nyote) ila wachache tu.” (04:83) Wakati wanandugu wawili walipokuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mdogo katika wao akataka kuzungumza, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamnyamazisha na kusema: “Anza na yule mkubwa! Anza na yule mkubwa!” Bi maana mwache kwanza mkubwa wako azungumze. Ni katika adabu za Kishari´ah kwamba wanafunzi wasitangulie kwanza. Wakati wa fitina za Abul-Hasan na al-Hajuuriy ilikuwa ni wanafunzi ndio walianza kuzungumza. Abul-Hasan aliwachochea wanafunzi dhidi ya wanachuoni. Kadhalika al-Hajuuriy alifanya hivo. Jazaa yake wanafunzi na wanachuoni wakaanza kuzungumza dhidi yao: وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ “Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa.” (16:126) Asli ni kwamba wanafunzi hawazungumzi mbele ya wanachuoni wao. Hata kama Shaykh atamuomba mwanafunzi wake kuandika makala, Shaykh ni mwanaadamu. Hakukingwa na kukosea. Katika hali hii mwanafunzi atake udhuru kwa heshima. Huu sio uwanja wa wanafunzi au watu wa kawaida. Huu ni uwanja wa wanachuoni. Anza na yule mkubwa! Anza na yule mkubwa. Akumbushe kwa Hadiyth na Aayah. Ikiwa Shaykh anataka mwanafunzi aandike na Shaykh aipitie, mwanafunzi aombe uandishi usambazwe kwa jina lake na sio jina lake [yeye mwanafunzi]. Ni bora yule mwanachuoni akazungumza kuliko mwanafunzi. Sizungumzii suala hili peke yake. Nazungumzia kuhusu Manhaj. Ni katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanachuoni peke yake, na sio vijana, kuingia katika masuala haya. Hadiyth inasema: “Baraka iko kwa wakubwa wenu.” Vijana wanaweza kusababisha ghasia tofauti na mkubwa atapomuomba Allaah msaada na akaingia kwenye maudhui na akamuomba Allaah Tawfiyq na uongofu. Huenda akawafikishwa. Haya ndio ninayowaomba ndugu zetu ambao ni wanafunzi na watu wa kawaida. Wasiwatangulie wanachuoni. Wajipambe kwa adabu. Wasiwe na papara ya kwenda kila mara kwa Shaykh au mwanachuoni na kumuomba aandike au azungumze. Huyu ni Shaykh. Sio mtoto wako wala kaka yako. Wala sio mwanafunzi wako uwezae kumuamrisha. Ni katika utovu wa adabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Katu hakukuwi uzuri katika kitu isipokuwa unakipamba na katu haukosi kwenye kitu isipokuwa unakifanya kuwa kibaya.” “Allaah ni mlaini na Anapenda ulaini na Anatoa kwa ajili yake Hatoi kwa vurugu.” Tunafuata Qur-aan na Sunnah na Manhaj ya Salaf ilio safi kabisa. Tunashikamana na Qur-aan na Sunnah. Kila kheri inapatikana kwa kufuata Qur-aan na Sunnah. Wanafunzi, pasina kujali daraja, wajipambe kwa adabu. Haijalishi kitu wale wanaoanza, shule ya kati na kati au chuo kikuu. Wote wawe na adabu kwa Mashaykh na wanachuoni wao.

Katika usiku huu wa 15 Shawwaal mwaka wa 1435 nitazungumzia kuhusu mkataba kati ya Shaykh Muhammad al-Imaam na ´Abdul-Maalik al-Hawthiy. Nina baadhi ya nasaha na maelekezo.

Kwanza ninawanasihi wanafunzi na watu wa kawaida kutowatangulia wanachuoni. Fanyeni hilo kuwa ni kanuni ya jumla katika majanga yote. Wasitanguliwe wanachuoni. Wajipambe kwa adabu za Kishari´ah. Wanyamaze na wasubiri maneno ya wanachuoni wao wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Enyi mlioamini! Msitangulie mbele ya Allaah na Mtume Wake. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).” (49:01)

Wanachuoni ndio warithi wa Mitume. Kama jinsi Maswahabah walivyokatazwa kutangulia mbele ya Allaah na Mtume Wake hali kadhalika linawahusu waliokuja baada ya Maswahabah wamekatazwa kutangulia mbele ya wanachuoni. Wanachuoni ndio wanatakiwa kuwa wa kwanza kuzungumza na sio wanafunzi wala watu wa kawaida. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amesema:

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا
“Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Mtume na kwa wenye madaraka kati yao, wale (Wanavyuoni) wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua. Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na Rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan (nyote) ila wachache tu.” (04:83)

Allaah Amewakataza kueneza uvumi na kuwaamrisha kurejea kwa wanachuoni:

لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا
“… wale (Wanavyuoni) wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua. Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na Rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan (nyote) ila wachache tu.” (04:83)

Wakati wanandugu wawili walipokuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mdogo katika wao akataka kuzungumza, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamnyamazisha na kusema:

“Anza na yule mkubwa! Anza na yule mkubwa!”

Bi maana mwache kwanza mkubwa wako azungumze. Ni katika adabu za Kishari´ah kwamba wanafunzi wasitangulie kwanza.

Wakati wa fitina za Abul-Hasan na al-Hajuuriy ilikuwa ni wanafunzi ndio walianza kuzungumza. Abul-Hasan aliwachochea wanafunzi dhidi ya wanachuoni. Kadhalika al-Hajuuriy alifanya hivo. Jazaa yake wanafunzi na wanachuoni wakaanza kuzungumza dhidi yao:

وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ
“Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa.” (16:126)

Asli ni kwamba wanafunzi hawazungumzi mbele ya wanachuoni wao. Hata kama Shaykh atamuomba mwanafunzi wake kuandika makala, Shaykh ni mwanaadamu. Hakukingwa na kukosea. Katika hali hii mwanafunzi atake udhuru kwa heshima. Huu sio uwanja wa wanafunzi au watu wa kawaida. Huu ni uwanja wa wanachuoni. Anza na yule mkubwa! Anza na yule mkubwa. Akumbushe kwa Hadiyth na Aayah. Ikiwa Shaykh anataka mwanafunzi aandike na Shaykh aipitie, mwanafunzi aombe uandishi usambazwe kwa jina lake na sio jina lake [yeye mwanafunzi]. Ni bora yule mwanachuoni akazungumza kuliko mwanafunzi. Sizungumzii suala hili peke yake. Nazungumzia kuhusu Manhaj. Ni katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanachuoni peke yake, na sio vijana, kuingia katika masuala haya. Hadiyth inasema:

“Baraka iko kwa wakubwa wenu.”

Vijana wanaweza kusababisha ghasia tofauti na mkubwa atapomuomba Allaah msaada na akaingia kwenye maudhui na akamuomba Allaah Tawfiyq na uongofu. Huenda akawafikishwa. Haya ndio ninayowaomba ndugu zetu ambao ni wanafunzi na watu wa kawaida. Wasiwatangulie wanachuoni. Wajipambe kwa adabu. Wasiwe na papara ya kwenda kila mara kwa Shaykh au mwanachuoni na kumuomba aandike au azungumze. Huyu ni Shaykh. Sio mtoto wako wala kaka yako. Wala sio mwanafunzi wako uwezae kumuamrisha. Ni katika utovu wa adabu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Katu hakukuwi uzuri katika kitu isipokuwa unakipamba na katu haukosi kwenye kitu isipokuwa unakifanya kuwa kibaya.”

“Allaah ni mlaini na Anapenda ulaini na Anatoa kwa ajili yake Hatoi kwa vurugu.”

Tunafuata Qur-aan na Sunnah na Manhaj ya Salaf ilio safi kabisa. Tunashikamana na Qur-aan na Sunnah. Kila kheri inapatikana kwa kufuata Qur-aan na Sunnah. Wanafunzi, pasina kujali daraja, wajipambe kwa adabu. Haijalishi kitu wale wanaoanza, shule ya kati na kati au chuo kikuu. Wote wawe na adabu kwa Mashaykh na wanachuoni wao.