Mtu Afanye Nini Kama Anataka Kufaulu?

Kama unataka kufaulu, ni juu yako (lazima) kushikamana na mambo matatu haya: 1- Shikamana na Kitabu cha Allaah. 2- Fuata uongofu. 3- Jiepushe na Bid´ah. Ukiacha moja kati ya mambo haya matatu, basi umekhasirika na hutofaulu kamwe. فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ “Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao.” (al-Muuminuun:102-103) Kinyume cha “kufaulu” ni kukhasirika na tunajikinga kwa Allaah. Hawakukhasirika mali zao bali wamekhasiri nafsi zao. Kule mtu kukhasirika nafsi yake hii ndio khasara kubwa na tunaomba kinga kwa Allaah. قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ “Hakika waliokhasirika ni wale waliokhasiri nafsi zao na ahli zao Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Huko ndiko kukhasirika dhahiri.” (az-Zumar:15) Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 57-58

Kama unataka kufaulu, ni juu yako (lazima) kushikamana na mambo matatu haya:

1- Shikamana na Kitabu cha Allaah.
2- Fuata uongofu.
3- Jiepushe na Bid´ah.

Ukiacha moja kati ya mambo haya matatu, basi umekhasirika na hutofaulu kamwe.

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ
“Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao.” (al-Muuminuun:102-103)

Kinyume cha “kufaulu” ni kukhasirika na tunajikinga kwa Allaah. Hawakukhasirika mali zao bali wamekhasiri nafsi zao. Kule mtu kukhasirika nafsi yake hii ndio khasara kubwa na tunaomba kinga kwa Allaah.

قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ
“Hakika waliokhasirika ni wale waliokhasiri nafsi zao na ahli zao Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Huko ndiko kukhasirika dhahiri.” (az-Zumar:15)

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 57-58


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 11th, February 2014