Msingi Wa Pili – Sunnah

Hapa tunapata kujua kwamba ni lazima kuitumia Sunnah baada ya Qur-aan. Sunnah ndio chanzo cha pili katika vyanzo vya Kiislamu baada ya Qur-aan Tukufu. Misingi ya kutumia kama dalili kwa Usuwliyyuun, katika hayo kuko ambayo wamekubaliana juu yake na mengine wametofautiana juu yake. Lakini yale ambayo wamekubaliana juu yake ni misingi mitatu: 1- Msingi wa kwanza: Qur-aan Tukufu. 2- Msingi wa pili: Sunnah ya Mtume. Kwa kuwa ni Wahyi wa pili baada ya Qur-aan. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema: وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا “Na lolote (lile) analokupeni Mtume (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na (lolote lile) analokukatazeni, basi acheni.” (al-Hashr:07) Anasema tena (Jalla wa ´Alaa): فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ “Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.” (an-Nuur:63) Huu ndio msingi wa pili ambao ni Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Naye ni kama Alivyomsifu Mola Wake: وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ “Na wala hatamki kwa matamanio (yake). Hayo (ayasemayo) si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa (kwake).” (an-Najm:03-04) Kwa ajili hii wanachuoni wanaita – yaani Sunnah zake – Wahyi wa pili baada ya Qur-aan Tukufu. Yaliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wajibu kuyachukua, kuyafuata na kuyatendea kazi, sawa ikiwa ni Mutawaatir au Ahaad, tofauti na Mubtadi´ah, wazushi ambao wanapinga Sunnah na wanasema tumetoshelezwa na kuitendea kazi Qur-aan. Ni jambo linalojulikana vyema kwamba kuitendea kazi Sunnah ndio kuitendea kazi vilevile Qur-aan. Kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema: وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا “Na lolote (lile) analokupeni Mtume (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na (lolote lile) analokukatazeni, basi acheni.” (al-Hashr:07) na watu hawa wanasema tumetoshelezwa na Qur-aan. Anasema tena (Jalla wa ´Alaa): مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ “Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah.” (an-Nisaa:80) وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ “Na mfuateni ili mpate kuongoka.” (al-A´raaf:158) وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ “Na mtiini Mtume ili mpate kurehemewa.” (an-Nuur:56) Watu hawa wamesema uongo kwa kusema kwao kwamba wanaitendea kazi Qur-aan. Kwa kule kuikanusha kwao Sunnah, hawakuitendea kazi Qur-aan. Isitoshe katika Qur-aan kuna (Aayah za) Mujmal, Sunnah ndio inaibainisha na kuifasiri. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema kumwambia Mtume Wake: وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ “Na Tumekuteremshia Adh-Dhikra (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwabainishie watu (kwa Sunnah) yaliyoteremshwa.” (an-Nahl:44) Sunnah ndio ina uwiano wa nguvu na Qur-aan. Kwa kuwa inabainisha, kuiweka wazi, kufafanua (Aayah za) Mujmal na kuipa nguvu (Aayah za) Muttwlaq. Vilevile Qur-aan inaweza kufutwa na Sunnah kama jinsi Qur-aan pia inaweza kuifuta Sunnah, Qur-aan ikaifuta Qur-aan na Sunnah ikaifuta Sunnah. Ni lazima kupatikane mambo haya makubwa. Kwa haya kunapata kujulikana manzila ya Sunnah katika Qur-aan na nafasi yake katika Uislamu. Hawa watu ambao wanapinga (au kiupuuza) Sunnah Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alielezea juu yao na akathadharisha nao kwa kusema: “Tanabahini! Kunakaribia kuja mtu aliyeshiba ajitupe juu ya kitanda chake. Aelezwe Hadiyth katika Hadiyth zangu. Aseme: “Baina yetu sisi na nyinyi kuna Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jalla). Tutayoyapata humo katika halali basi tutayahalalisha na tutayoyapata humo ya haramu basi tuyaharamishe. Tanabahini! Yale aliyoharamisha Mtume wa Allaah ndio mfano wa Aliyoharamisha Allaah.” Kadhalika kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nimepewa Qur-aan na mfano wake pamoja.” yaani Sunnah. Kauli yake (Ta´ala): وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ “Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah.” (an-Nisaa:113) وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ “Anawafunza Kitabu na Hikmah.” (al-´Imraan:164) Kitaabu ni Qur-aan na Hikmah ni Sunnah. Sunnah ni lazima na ndio msingi wa pili katika misingi ya dalili ambao wamekubaliana. Haizingatiwi tofauti ya watu hawa ambao wanapinga Sunnah. Kwa kuwa ima ni Khawaarij, wajinga, wanaoanza kusoma au watu wenye malengo mabaya wanachotaka ni kuiharibu Dini kidogo kidogo. Tofauti yao haizingatiwi na wala maneno yao hayatazamwi. Sunnah sahihi inatendewa kazi, sawa ikiwa ni katika mambo madogo madogo au mambo ya msingi. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 59-61

Hapa tunapata kujua kwamba ni lazima kuitumia Sunnah baada ya Qur-aan. Sunnah ndio chanzo cha pili katika vyanzo vya Kiislamu baada ya Qur-aan Tukufu. Misingi ya kutumia kama dalili kwa Usuwliyyuun, katika hayo kuko ambayo wamekubaliana juu yake na mengine wametofautiana juu yake. Lakini yale ambayo wamekubaliana juu yake ni misingi mitatu:

1- Msingi wa kwanza: Qur-aan Tukufu.
2- Msingi wa pili: Sunnah ya Mtume. Kwa kuwa ni Wahyi wa pili baada ya Qur-aan. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا
“Na lolote (lile) analokupeni Mtume (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na (lolote lile) analokukatazeni, basi acheni.” (al-Hashr:07)

Anasema tena (Jalla wa ´Alaa):

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
“Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.” (an-Nuur:63)

Huu ndio msingi wa pili ambao ni Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Naye ni kama Alivyomsifu Mola Wake:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ
“Na wala hatamki kwa matamanio (yake). Hayo (ayasemayo) si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa (kwake).” (an-Najm:03-04)

Kwa ajili hii wanachuoni wanaita – yaani Sunnah zake – Wahyi wa pili baada ya Qur-aan Tukufu.

Yaliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wajibu kuyachukua, kuyafuata na kuyatendea kazi, sawa ikiwa ni Mutawaatir au Ahaad, tofauti na Mubtadi´ah, wazushi ambao wanapinga Sunnah na wanasema tumetoshelezwa na kuitendea kazi Qur-aan.

Ni jambo linalojulikana vyema kwamba kuitendea kazi Sunnah ndio kuitendea kazi vilevile Qur-aan. Kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا
“Na lolote (lile) analokupeni Mtume (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na (lolote lile) analokukatazeni, basi acheni.” (al-Hashr:07)

na watu hawa wanasema tumetoshelezwa na Qur-aan. Anasema tena (Jalla wa ´Alaa):

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ
“Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah.” (an-Nisaa:80)

وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
“Na mfuateni ili mpate kuongoka.” (al-A´raaf:158)

وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
“Na mtiini Mtume ili mpate kurehemewa.” (an-Nuur:56)

Watu hawa wamesema uongo kwa kusema kwao kwamba wanaitendea kazi Qur-aan. Kwa kule kuikanusha kwao Sunnah, hawakuitendea kazi Qur-aan.

Isitoshe katika Qur-aan kuna (Aayah za) Mujmal, Sunnah ndio inaibainisha na kuifasiri. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema kumwambia Mtume Wake:

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ
“Na Tumekuteremshia Adh-Dhikra (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwabainishie watu (kwa Sunnah) yaliyoteremshwa.” (an-Nahl:44)

Sunnah ndio ina uwiano wa nguvu na Qur-aan. Kwa kuwa inabainisha, kuiweka wazi, kufafanua (Aayah za) Mujmal na kuipa nguvu (Aayah za) Muttwlaq. Vilevile Qur-aan inaweza kufutwa na Sunnah kama jinsi Qur-aan pia inaweza kuifuta Sunnah, Qur-aan ikaifuta Qur-aan na Sunnah ikaifuta Sunnah. Ni lazima kupatikane mambo haya makubwa. Kwa haya kunapata kujulikana manzila ya Sunnah katika Qur-aan na nafasi yake katika Uislamu.

Hawa watu ambao wanapinga (au kiupuuza) Sunnah Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alielezea juu yao na akathadharisha nao kwa kusema:

“Tanabahini! Kunakaribia kuja mtu aliyeshiba ajitupe juu ya kitanda chake. Aelezwe Hadiyth katika Hadiyth zangu. Aseme: “Baina yetu sisi na nyinyi kuna Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jalla). Tutayoyapata humo katika halali basi tutayahalalisha na tutayoyapata humo ya haramu basi tuyaharamishe. Tanabahini! Yale aliyoharamisha Mtume wa Allaah ndio mfano wa Aliyoharamisha Allaah.”

Kadhalika kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nimepewa Qur-aan na mfano wake pamoja.”

yaani Sunnah.

Kauli yake (Ta´ala):

وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ
“Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah.” (an-Nisaa:113)

وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ
“Anawafunza Kitabu na Hikmah.” (al-´Imraan:164)

Kitaabu ni Qur-aan na Hikmah ni Sunnah.

Sunnah ni lazima na ndio msingi wa pili katika misingi ya dalili ambao wamekubaliana. Haizingatiwi tofauti ya watu hawa ambao wanapinga Sunnah. Kwa kuwa ima ni Khawaarij, wajinga, wanaoanza kusoma au watu wenye malengo mabaya wanachotaka ni kuiharibu Dini kidogo kidogo. Tofauti yao haizingatiwi na wala maneno yao hayatazamwi. Sunnah sahihi inatendewa kazi, sawa ikiwa ni katika mambo madogo madogo au mambo ya msingi.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 59-61


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 11th, February 2014