Msimamo Wa Salaf Kwa Wenye Kuwatetea Ahl-ul-Bid´ah

Wanasema kuwa Muhammad bin Haadiy anasema hili na lile. Sisi na nyinyi tuhukumiwe kwa vitabu vilivyopokelewa kwa minyororo. Mkikuta ninaenda kinyume na herufi moja tu, basi mnionyeshe. Nitawatajia mfano mmoja juu ya suala hili. Ni kitu ambacho Mumayyi´ah leo hawataki kukisikia. al-Lalakaa´iy ametaja hilo katika mjaladi wa kwanza [wa Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah] wakati alipokuwa anataja ´Aqiydah ya Abu Haatim ar-Raaziy na Abu Zur´ah ar-Raaziy. Wakati alipoingia kwenye ´Aqiydah ya Abu Haatim ar-Raaziy akataja matahadharisho ya Ahl-ul-Hadiyth was-Sunnah juu ya al-Karaabiysiy. al-Karaabiysiy alikuwa ni Faqiyh mkubwa. Alikuwa anajulikana. Pindi alipoandika kitabu kuhusu porojo na watu wa porojo na akamuonesha nacho Imaam Ahmad, akamkemea kwayo. Walimweleza kuwa Abu ´Abdillaah [Ahmad bin Hanbal] alifikiwa na kitabu hichi na akamuomba kujirudi, lakini akakataa. Ndipo Abu Haatim akaomba aelezwe hali ya al-Karaabiysiy ambapo akaanza kumkemea na kutahadharisha rafiki yake na kukaa naye. Abu Haatim akatahadharisha al-Karaabiysiy na mwenye kumtetea kama Daawuud bin ´Aliy al-Asbahaaniy. Daawuud bin ´Aliy al-Asbahaaniy alikuwa ni kiongozi wa Dhwaahiriyyah. Cheo chake kilikuwa kikubwa. Alikuja kwa Imaam Ahmad na akakataa kumpokea. Abu Haatim akazungumza juu yake maneno makali sana kwa sababu anamtetea al-Karaabiysiy. Wakati al-Karaabiysiy alipopata taarifa ya ukosoaji wa Ahmad na akakataa kuukubali, akaanza kumsema vibaya Ahmad. Ninakuelezeni jambo hili lenye kuchoma, lakini limetajwa kwenye vitabu vya Salaf wetu ili mtu aweze kujua ni nani mwenye kufumbia macho na kujifanya ni kiziwi wa haki. Yahyaa bin Ma´iyn alifikiwa na khabari jinsi al-Karaabiysiy anavomsema vibaya Imaam Ahmad ambapo akasema: "Allaah Amlaani." Hatuzungumzi kuwa ni sawa au si sawa. Tunazungumzia ukali wa Yahyaa kwa al-Karaabiysiy. Alisema: "Allaah Amlaani. Anastahiki kutiwa adabu." Ahmad hakudhurika kwa hili. al-Karaabiysiy alikufa. al-Khatwiyb al-Baghdaadiy ametaja jinsi alivyopokea Hadiyth lakini ilikuwa karibu hakuna yeyote anayesimulia kutoka kwake. Wanafunzi wakamkimbia. Tazama jinsi wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah walivyokuwa wananusuriana. Wakati Daawuud bin ´Aliy alivyomtetea al-Karaabiysiy, Ahmad akamtimua na hakumuacha aingie. Abu Haatim na wengi katika wanachuoni Ahl-us-Sunnah katika zama hizo wakatahadharisha naye. Je, hawa wa leo wanaweza kulinganishwa na wale? Ni kama tone kwenye bahari ukilinganisha na wale. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba yule atakayeenda kinyume na njia ya wale tutatahadharisha naye hata kama tutakuwa ndege wa mawindo. Je, mnafikiria kuwa Dini hii imetufikia bila ya malezi? Ninaapa kwa Allaah ya kuwa sivyo. Baadhi walifungwa. Wengine walipigwa. Kuko ambao walidhulumiwa. Wengine wakafukuzwa. Pamoja na hivyo vitabu vyao viko mbele yetu. Kurasa zao zenye kung´ara ziko mbele yetu. Watu hawa ambao wanataka kuchukua wepesi juu ya suala la watu wa Bid´ah, ni lazima waepukwe. Khatari yao kwa Ahl-us-Sunnah na Salafiyyuun ni kubwa kuliko khatari ya Ahl-ul-Bid´ah. Mzungumzaji: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy Chanzo: sahab.net Toleo la: 05-12-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Wanasema kuwa Muhammad bin Haadiy anasema hili na lile. Sisi na nyinyi tuhukumiwe kwa vitabu vilivyopokelewa kwa minyororo. Mkikuta ninaenda kinyume na herufi moja tu, basi mnionyeshe.

Nitawatajia mfano mmoja juu ya suala hili. Ni kitu ambacho Mumayyi´ah leo hawataki kukisikia.

al-Lalakaa´iy ametaja hilo katika mjaladi wa kwanza [wa Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah] wakati alipokuwa anataja ´Aqiydah ya Abu Haatim ar-Raaziy na Abu Zur´ah ar-Raaziy. Wakati alipoingia kwenye ´Aqiydah ya Abu Haatim ar-Raaziy akataja matahadharisho ya Ahl-ul-Hadiyth was-Sunnah juu ya al-Karaabiysiy. al-Karaabiysiy alikuwa ni Faqiyh mkubwa. Alikuwa anajulikana. Pindi alipoandika kitabu kuhusu porojo na watu wa porojo na akamuonesha nacho Imaam Ahmad, akamkemea kwayo. Walimweleza kuwa Abu ´Abdillaah [Ahmad bin Hanbal] alifikiwa na kitabu hichi na akamuomba kujirudi, lakini akakataa. Ndipo Abu Haatim akaomba aelezwe hali ya al-Karaabiysiy ambapo akaanza kumkemea na kutahadharisha rafiki yake na kukaa naye. Abu Haatim akatahadharisha al-Karaabiysiy na mwenye kumtetea kama Daawuud bin ´Aliy al-Asbahaaniy. Daawuud bin ´Aliy al-Asbahaaniy alikuwa ni kiongozi wa Dhwaahiriyyah. Cheo chake kilikuwa kikubwa. Alikuja kwa Imaam Ahmad na akakataa kumpokea. Abu Haatim akazungumza juu yake maneno makali sana kwa sababu anamtetea al-Karaabiysiy. Wakati al-Karaabiysiy alipopata taarifa ya ukosoaji wa Ahmad na akakataa kuukubali, akaanza kumsema vibaya Ahmad.

Ninakuelezeni jambo hili lenye kuchoma, lakini limetajwa kwenye vitabu vya Salaf wetu ili mtu aweze kujua ni nani mwenye kufumbia macho na kujifanya ni kiziwi wa haki.

Yahyaa bin Ma´iyn alifikiwa na khabari jinsi al-Karaabiysiy anavomsema vibaya Imaam Ahmad ambapo akasema:

“Allaah Amlaani.”

Hatuzungumzi kuwa ni sawa au si sawa. Tunazungumzia ukali wa Yahyaa kwa al-Karaabiysiy. Alisema:

“Allaah Amlaani. Anastahiki kutiwa adabu.”

Ahmad hakudhurika kwa hili. al-Karaabiysiy alikufa. al-Khatwiyb al-Baghdaadiy ametaja jinsi alivyopokea Hadiyth lakini ilikuwa karibu hakuna yeyote anayesimulia kutoka kwake. Wanafunzi wakamkimbia. Tazama jinsi wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah walivyokuwa wananusuriana. Wakati Daawuud bin ´Aliy alivyomtetea al-Karaabiysiy, Ahmad akamtimua na hakumuacha aingie. Abu Haatim na wengi katika wanachuoni Ahl-us-Sunnah katika zama hizo wakatahadharisha naye.

Je, hawa wa leo wanaweza kulinganishwa na wale? Ni kama tone kwenye bahari ukilinganisha na wale. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba yule atakayeenda kinyume na njia ya wale tutatahadharisha naye hata kama tutakuwa ndege wa mawindo. Je, mnafikiria kuwa Dini hii imetufikia bila ya malezi? Ninaapa kwa Allaah ya kuwa sivyo. Baadhi walifungwa. Wengine walipigwa. Kuko ambao walidhulumiwa. Wengine wakafukuzwa. Pamoja na hivyo vitabu vyao viko mbele yetu. Kurasa zao zenye kung´ara ziko mbele yetu. Watu hawa ambao wanataka kuchukua wepesi juu ya suala la watu wa Bid´ah, ni lazima waepukwe. Khatari yao kwa Ahl-us-Sunnah na Salafiyyuun ni kubwa kuliko khatari ya Ahl-ul-Bid´ah.

Mzungumzaji: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
Chanzo: sahab.net
Toleo la: 05-12-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 5th, December 2014