Msikiti Na Kaburi

´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy: Katika Uislamu haviwezi kukusanyika mahala pamoja Msikiti na kaburi. "Allaah Awalaani Mayahudi na Manaswara, wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa Misikiti." Uislamu umeharamisha kuweka mahala pamoja Msikiti na kaburi. "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msiyafanye makaburi kuwa Misikiti. Na niswalieni popote mlipo, kwa hakika Swalah zenu hunifikia." Kaburi na Msikiti, haviwezi kuwa mahala pamoja kamwe. Na Allaah Kawalaani Baniy Israaiyl kwa kuyafanya makaburi kuwa Misikiti wakiwaabudu Mitume, kwa kuwa ni viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Na magonjwa haya yamewaingilia Waislamu kupitia njia ya Mayahudi na Manaswara na waabudu masanamu. Na wamewasadikisha hawa wapotofu waabudu wa makaburi wameiweka Misikiti kwenye makaburi. Mpaka hali imefikia, unakuta katika baadhi ya miji Misikiti isiokuwa na kaburi haswali watu, Jamaa´ah ya watu wanaoswali humo ni wadogo sana. Na unaona Msikiti ulio na kaburi umejaa watu. Kwa hakika hawa ni waabudu wa makaburi na hawamuabudu Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Sahihi ni kwamba, Swalah katika Msikiti ambapo ndani yake kuna kaburi, Swalah hii ni batili na haisihi. Tunamuomba Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Awaponye Waislamu na maradhi haya machafu, ambayo sio ya kitabia wala kukosa kuwa na adabu, bali ni [maradhi ya] ´Aqiydah.

´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:

Katika Uislamu haviwezi kukusanyika mahala pamoja Msikiti na kaburi.

“Allaah Awalaani Mayahudi na Manaswara, wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa Misikiti.”

Uislamu umeharamisha kuweka mahala pamoja Msikiti na kaburi.

“Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msiyafanye makaburi kuwa Misikiti. Na niswalieni popote mlipo, kwa hakika Swalah zenu hunifikia.”

Kaburi na Msikiti, haviwezi kuwa mahala pamoja kamwe. Na Allaah Kawalaani Baniy Israaiyl kwa kuyafanya makaburi kuwa Misikiti wakiwaabudu Mitume, kwa kuwa ni viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Na magonjwa haya yamewaingilia Waislamu kupitia njia ya Mayahudi na Manaswara na waabudu masanamu. Na wamewasadikisha hawa wapotofu waabudu wa makaburi wameiweka Misikiti kwenye makaburi. Mpaka hali imefikia, unakuta katika baadhi ya miji Misikiti isiokuwa na kaburi haswali watu, Jamaa´ah ya watu wanaoswali humo ni wadogo sana. Na unaona Msikiti ulio na kaburi umejaa watu. Kwa hakika hawa ni waabudu wa makaburi na hawamuabudu Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Sahihi ni kwamba, Swalah katika Msikiti ambapo ndani yake kuna kaburi, Swalah hii ni batili na haisihi. Tunamuomba Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Awaponye Waislamu na maradhi haya machafu, ambayo sio ya kitabia wala kukosa kuwa na adabu, bali ni [maradhi ya] ´Aqiydah.