Msafiri Anayeishi Pembezoni Mwa Msikiti Na Anasikia Adhaana

Swali La Kwanza: Tukiwa ni wasafiri katika mji, akaadhini muadhini Swalah ya Dhuhr. Je, ni wajibu kwetu kuswali Msikitini? ´Allaamah al-Fawzaan: Ndio, mkiwa karibu na Msikiti mnasikia adhaana ni wajibu kwenu kuhudhuria na mswali pamoja na Waislamu. Swali La Pili: Na tukiswali Msikitini Swalah ya Dhuhr pamoja na watu, inajuzu kwetu kuswali baada yake Swalah ya ´Aswr Jamaa´ah? ´Allaamah al-Fawzaan: Hakuna ubaya kufanya hivyo. Ukiwa mnataka kuendelea na safari yenu, jumuisheni. Ama ikiwa mnataka kubaki kwenye mji, hapana. al-Muqiym [Ataebaki mjini siku zaidi ya 3] anaswali Swalah zote kwa wakati wake na wala hajumuishi.

Swali La Kwanza:
Tukiwa ni wasafiri katika mji, akaadhini muadhini Swalah ya Dhuhr. Je, ni wajibu kwetu kuswali Msikitini?

´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, mkiwa karibu na Msikiti mnasikia adhaana ni wajibu kwenu kuhudhuria na mswali pamoja na Waislamu.

Swali La Pili:
Na tukiswali Msikitini Swalah ya Dhuhr pamoja na watu, inajuzu kwetu kuswali baada yake Swalah ya ´Aswr Jamaa´ah?

´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna ubaya kufanya hivyo. Ukiwa mnataka kuendelea na safari yenu, jumuisheni. Ama ikiwa mnataka kubaki kwenye mji, hapana. al-Muqiym [Ataebaki mjini siku zaidi ya 3] anaswali Swalah zote kwa wakati wake na wala hajumuishi.