´Mna Msimamo Mkali` – Kisha Baadae Yawa Hivi…

Qadhiya hii na utata huu ambao mmesikia karibuni ndio ambayo yanawakata Salafiyyuun leo. Ni kana kwamba hawakusoma vitabu vya ´Aqiydah. Kwa ajili hiyo wameanza kuwaona wale wenye kushikamana bara bara na Manhaj hii kuwa ni “wenye msimamo mkali”, “wavuka mipaka”, kwamba “anajiona yeye mwenyewe” na kadhalika. Ninaapa kwa Allaah kuwa ni ajabu. Tazama huyu aliyepinda kutoka katika njia iliyonyooka alivyokuwa akisema jana. Linganisha maneno yake ya jana na leo. Je, yeye ndiye alikuwa na Ahl-us-Sunnah au ni yeye ndio amebadilika na sio Ahl-us-Sunnah? Yale waliyokuwa wakishikamana nayo jana bado ni yale yale waliyoshikamana nayo leo. Hawakubadilika. Wewe ndio umebadilika. Hivi sasa unawasifu al-Ikhwaan al-Muslimuun. Hivi sasa unawasifu Jamaa´at-ut-Tabliygh. Hivi sasa unamsifu Hasan al-Bannaa. Hivi sasa unamsifu Sayyid Qutwub. Kisha unaanza kuchukulia sahali al-Ikhwaan al-Muslimuun, Jamaa´at-ut-Tabliyg na Suruuriyyuun. Unaanza kusema kuwa Sayyid Qutwub alikuwa na Ikhlaasw, lakini Ikhlaasw ni kitu cha moyoni na hakijui yeyote isipokuwa Allaah (Jallawa ´Alaa). Isitoshe unawahujumu Ahl-us-Sunnah.

Qadhiya hii na utata huu ambao mmesikia karibuni ndio ambayo yanawakata Salafiyyuun leo. Ni kana kwamba hawakusoma vitabu vya ´Aqiydah. Kwa ajili hiyo wameanza kuwaona wale wenye kushikamana bara bara na Manhaj hii kuwa ni “wenye msimamo mkali”, “wavuka mipaka”, kwamba “anajiona yeye mwenyewe” na kadhalika.

Ninaapa kwa Allaah kuwa ni ajabu. Tazama huyu aliyepinda kutoka katika njia iliyonyooka alivyokuwa akisema jana. Linganisha maneno yake ya jana na leo. Je, yeye ndiye alikuwa na Ahl-us-Sunnah au ni yeye ndio amebadilika na sio Ahl-us-Sunnah? Yale waliyokuwa wakishikamana nayo jana bado ni yale yale waliyoshikamana nayo leo. Hawakubadilika. Wewe ndio umebadilika. Hivi sasa unawasifu al-Ikhwaan al-Muslimuun. Hivi sasa unawasifu Jamaa´at-ut-Tabliygh. Hivi sasa unamsifu Hasan al-Bannaa. Hivi sasa unamsifu Sayyid Qutwub.

Kisha unaanza kuchukulia sahali al-Ikhwaan al-Muslimuun, Jamaa´at-ut-Tabliyg na Suruuriyyuun. Unaanza kusema kuwa Sayyid Qutwub alikuwa na Ikhlaasw, lakini Ikhlaasw ni kitu cha moyoni na hakijui yeyote isipokuwa Allaah (Jallawa ´Alaa). Isitoshe unawahujumu Ahl-us-Sunnah.