Mlinganizi Mtukufu Anayependwa Na Watu Wote

Ni jambo lenye kusitikisha jinsi leo wanavosema: "Mlinganizi huyu na huyu ana tabia nzuri kweli! Kila mtu anampenda!" Ukiona mtu anayependwa na kila mtu basi ujue kuwa ni mpakanaji mafuta. Hata Mitume hawakupendwa na watu wote. Allaah Aliwafanya wakawa na maadui. Kwa msemo mwingine hii ina maana ya kwamba mtu huyo haamrishi mema na hakatazi maovu. Hamgusi yeyote. Kila mtu anampenda. Hii ina maana ya kwamba ni mpakanaji mafuta. Vinginevyo ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Aliwafanya Mitume kuwa na maadui kati ya watu na majini. Hivyo basi, unapowasikia watu wanasema kuwa kuna mtu asiyechukiwa na yeyote na kila mtu anampenda, basi utambue kuwa ni mpakanaji mafuta. Kwa sababu hatekelezi maamrisho ya Allaah. Ikiwa kweli ametimiza maamrisho ya Allaah basi ungeliona jinsi watu wa batili, washirikina na Ahl-ul-Bid´ah wangelivomchukia na huku anapendwa tu na watu wema Ahl-ut-Tawhiyd na Ahl-us-Sunnah. Ama kupendwa na watu wote na hakuna yeyote wa kumchukia ni dalili tosha kuonyesha ya kwamba ni mpakanaji mafuta. Mzungumzaji: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=148340 Toleo la: 10-12-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Ni jambo lenye kusitikisha jinsi leo wanavosema:

“Mlinganizi huyu na huyu ana tabia nzuri kweli! Kila mtu anampenda!”

Ukiona mtu anayependwa na kila mtu basi ujue kuwa ni mpakanaji mafuta. Hata Mitume hawakupendwa na watu wote. Allaah Aliwafanya wakawa na maadui. Kwa msemo mwingine hii ina maana ya kwamba mtu huyo haamrishi mema na hakatazi maovu. Hamgusi yeyote. Kila mtu anampenda. Hii ina maana ya kwamba ni mpakanaji mafuta. Vinginevyo ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Aliwafanya Mitume kuwa na maadui kati ya watu na majini. Hivyo basi, unapowasikia watu wanasema kuwa kuna mtu asiyechukiwa na yeyote na kila mtu anampenda, basi utambue kuwa ni mpakanaji mafuta. Kwa sababu hatekelezi maamrisho ya Allaah. Ikiwa kweli ametimiza maamrisho ya Allaah basi ungeliona jinsi watu wa batili, washirikina na Ahl-ul-Bid´ah wangelivomchukia na huku anapendwa tu na watu wema Ahl-ut-Tawhiyd na Ahl-us-Sunnah. Ama kupendwa na watu wote na hakuna yeyote wa kumchukia ni dalili tosha kuonyesha ya kwamba ni mpakanaji mafuta.

Mzungumzaji: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=148340
Toleo la: 10-12-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Da´wah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 10th, December 2014