Mlango Wa 61: Yaliyokuja Kuhusu Watengeneza Picha

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: “Allaah Kasema: “Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule ambaye anajaribu kuumba mfano wa viumbe Vyangu? Waache waumbe chembe, au waumbe nafaka, au waache waumbe nafaka ya shayiri.'" (Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim) Wamepokea pia kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wanaoiga uumbaji wa Allaah.” Wamepokea pia kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalia kila picha aliyoitengeneza nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake katika Moto wa Jahannam.” Wamepokea (al-Bukhaariy na Muslim) tena kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allahu ´anhumaa) Hadiyth ya Marfuu´: “Atakayetengeneza picha duniani atakalifishwa kuitia roho na hatoweza kufanya hivyo.” Muslim kapokea kutoka kwa Abu Hayyaaj (al-Asadiy) ya kwamba ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) alimwambia: “Hivi nikutumie ujumbe kama vile alivyonituma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Nao ni kuwa usiache picha hata moja isipokuwa umeifutilia mbali wala kaburi lililoinuka isipokuwa ulisawazishe.” MAELEZO Mlango huu ni kuhusu matishio makali yaliyokuja kuhusu wetengeneza picha na makatazo ya picha. Hilo, ni kwa sababu picha ni katika njia zinazopelekea katika Shirki. Ikiadhimishwa picha na kutundikwa – na khaswa picha za wakuu na watu wema – zikatundikwa, hakika ni katika njia zinazopelekea katika Shirki, kama ilivyokuwa katika watu wa Nuuh. Hakika mwanzo wa Shirki kabisa ilivoanza katika ardhi ni kwa sababu ya picha. Hapo ilikuwa pindi walipokufa watu wema katika watu wa Nuuh ambao walikuwa wameshikamana na ´Ibaadah, elimu na Da´wah katika Dini ya Allaah, watu hawa walipokufa wakawa na huzuni kubwa juu yao. Walikufa katika mwaka mmoja. Akawajia Shaytwaan na kuwaambia: “Tengenezeni sura (picha) zao ili muweze kukumbuka hali zao, na ziweze kuwasaidia katika ´Ibaadah.” Alikuja kwa njia ya kuwapa nasaha kwa madai yake. Hawakuwaambia: “Tengenezeni ili muwaabudu”, isipokuwa aliwaambia kwa sababu ziweze kuwasaidia katika ´Ibaadah na kukumbuka hali zao pindi mtapoona picha zao kisha mzitundike katika vikao vyenu. Yeye alikuwa anakusudia Mustaqbal (huko mbeleni) kwa kujua kwake kuwa kizazi hichi hakiwezi kuabudu picha, ndani yake kulikuwemo wanachuoni. Lakini huko mbele kutakuja kizazi cha wajinga, hapo ndipo akawajia Shaytwaan na kuwaambia: “Hakika baba zenu hawakutengeneza picha haya isipokuwa ni kwa sababu ziko na baraka, zinaathiri na kunufaisha.” Akawa amewadanganya namna hii ya kuwa picha hizi zinanufaisha na kudhuru, kwa kuwa zimenasibishwa kwa ajili ya ´Ibaadah. Hivyo, wakawa wameziabudu badala ya Allaah. Hapa ndio Shirki ikawa imeanza. Allaah Akamtuma Mtume Wake Nuuh (´alayhis-Salaam) awalinganie katika kumuabudu Allaah Pekee asiyekuwa na mshirika na kuacha Shirki. Wakakataa. وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ ”Wakasema: “Msiwaache miungu yenu.” (Nuuh 71:23) yaani msiache picha hizi. وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا ”Na wala msimwache Waddaa, na wala Su’waa’a, na wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa.” (Nuuh 71:23) Haya ni majina ya watu wema ambao zilitengenezwa picha zao na wakaabudiwa badala ya Allaah. Na wakausiana kutoacha kuwaabudu na kumuasi Nuuh (´alayhis-Salaam). Shirki ikawa imezuka kwa ajili ya picha na kuadhimisha picha. Kwa ajili hiyo, ndio maana mwandishi akawa ametenga mlango huu katika kitabu cha Tawhiyd. Kwa kuwa kitabu hichi kinabainisha Tawhiyd na Shirki, sababu za Shirki na njia zake. Hii ndio sababu, ya kwamba picha ni katika njia za Shirki, kwa kuwa ni kuiga viumbe vya Allaah (´Azza wa Jalla). Kwa kuwa mtengeneza picha anataka kupatikane sura inayofanana na sura Aliyoiumba Allaah. Anajaribu kufanya hivi. Kuna ushirikisho wa Allaah katika jambo ambalo ni maalum Kwake Pekee ambalo ni Kuumba. Kwa kuwa hakuna awezae kuumba isipokuwa Allaah (´Azza wa Jalla). Huyu mtengeneza picha anajaribu kushirikiana na Allaah katika Kuumba Kwake na kupatikane picha inayofanana na Aliyoumba Allaah. Hili ni jambo la khatari. Na wala haijuzu kufanya picha kwa viumbe vyenye roho. Ama kufanya picha ya viumbe visivyokuwa na roho, kama miti, nyumba, gari na kadhalika hakuna ubaya. Kwa kuwa hakuna kipingamizi. Makatazo ni kufanya picha ya kiumbe chenye roho katika wanaadamu, minyama na kila kiumbe chenye roho. Haya ndio yamekatazwa. Hii ndio sababu ya kutajwa mlango huu katika kitabu cha Tawhiyd kwa kuwa picha ni katika njia zinazopelekea katika Shirki, kama ilivokuwa katika watu wa Nuuh. Hadiyth “Allaah Kasema: “Ni nani dhalimu...”, yaani hakuna yeyote ambaye ni dhalimu mkubwa kama mtu huyu. Kwa kuwa Shirki ndio aina kubwa ya dhuluma. إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ”Hakika shirki ni dhulma kubwa mno!” (Luqmaan 31:13) Na hii ni katika njia ya Shirki. Yaani mtu huyu anatengeneza picha na anataka kutoka katika picha hiyo kufananisha na viumbe vya Allaah (´Azza wa Jalla). Picha hiyo anaifanya kuwa na kiwiliwili, uso, macho, mdomo n.k. kama kilivo kiumbe cha Allaah (´Azza wa Jalla). Namna hii. Yaani anaumba sura, anataka kuumba kama kiumbe cha Allaah. Huyu ndiye dhalimu mkubwa. Mtengeneza picha ndiye dhalimu mkubwa. Allaah Atukinge. Allaah Kawapa changamoto na Kuwaambia: “Waache waumbe chembe, au waumbe nafaka, au waache waumbe nafaka ya shayiri.'" Pengine wakatengeneza picha, lakini hawawezi kuipulizia roho na kuifanya ikawa kama kiumbe cha Allaah, kinatembea, kinachukua kitu, kinaongea. Hawawezi kufanya hivi. Wanachoweza ni kuigiza tu. Hawawezi hilo. “Watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wanaoiga uumbaji wa Allaah.” Na haya ni matishio mengine. Ya kwanza ilikuwa kwamba wao ndio madhalimu wakubwa, na haya ya pili ni kwamba ndio watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah. Mtengeneza picha. Huyu ndiye atakayekuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah, kwa kuwa kitendo chake hichi ni njia inayopelekea katika Shirki na kutaka kushirikiana pamoja na Allaah katika kuumba Kwake. “Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalie kila picha aliyoitengeneza nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam.” Haya ni matishio ya tatu kwa wale wenye kutengeneza picha. Kasema kila mtengeneza picha, sawa ikiwa katengeneza (kafanya picha hiyo) kwa kunakili, au katengeneza picha kwa kuchora na mkono, au kwa kifaa cha Camera. Kila mtengeneza picha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuvua kitu katika hayo, ni yeyote katika wanaotengeneza picha, sawa ikiwa katumia njia yoyote ile ya kufanya picha. Wale wanaosema kuwa picha za Digital Camera hazina ubaya, inawafedhehesha Hadiyth hii. Kwa kuwa Mtume hapa hakuvua kitu. Kasema “kila mtengeneza picha”, kila mwenye kufanya picha bila kujali katumia njia ipi. Kapewa tishio la Moto. “Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalia kila picha aliyoitengeneza nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam.” Hili ni tishio la nne. Ataijaalia kila picha aliyoitengeneza kuipa nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam. Ataadhibiwa kwa kila picha aliyoitengeneza. Ikiwa alitengeneza picha mia, atazijaalia nafsi mia. Ikiwa alitengeneza picha milioni, atazijaalia nafsi milioni. Kwa kila picha ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam. Allaah Atukinge. Je, hivi kweli kuna matishio makali zaidi ya haya? Mtu yuko katika afya, Alhamdulillaah, asiingize nafsi yake katika yaharamu. Mtu aache mambo ya picha. Hili ni jambo la khatari sana. Kadiri ya idadi ya wingi wa picha ndio jinsi adhabu itakuwa kubwa. “Atakayetengeneza picha duniani atakalifishwa kuitia roho na hatoweza kufanya hivyo.” Hili ni tishio la tano. Ya kwamba mpiga picha siku ya Qiyaamah ataambiwa: “Kitie roho ulichokiumba, kipulizie roho.” Na hatoweza kufanya hivi kwa kuwa roho. وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي ”Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: “Roho ni katika amri ya Mola wangu.” (al-Israa 17:85) Hakuna yeyote awazae kupulizia picha roho, akaifanya ikatembea. Hata hivyo, ataamrishwa kufanya hivyo kwa ajili ya kutaka kumuadhibu. “Hivi nikutumie ujumbe kama vile alivyonituma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Nao ni kuwa usiache picha hata moja isipokuwa umeifutilia mbali wala kaburi lililoinuka isipokuwa ulisawazishe.” Hapa kuna ubainisho wa nini kinachofanywa na picha, ya kwamba ni wajibu kuichana chana. Huku ni katika kuondosha munkari. Huu ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtuma ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu), akamuamrisha na kumuusia asiache picha hata moja isipokuwa aifutilie mbali. Hapa kamwambia “usiache picha hata moja” hakukuvuliwa kitu hata kimoja. Hali kadhalika kaburi lililoinuka, yaani kujengewa na kuadhimishwa isipokuwa alisawazishe, yaani aliweke sawa na alifanye kama makaburi mengine ya Waislamu. Isijengewe, isiandikwe kitu, isipambwe na kadhalika. Kwa kuwa hii ni njia inayopelekea katika Shirki. Wakati Shiy´ah waliposhika utawala Misri na katika miji mingi ya Waislamu ndio kukazushwa kuyajengea makaburi na likaenea hili katika miji ya Waislamu kwa sababu ya Shiy´ah al-Faatwimiyyuun, vinginevyo hili lilikuwa ni jambo lisilojulikana mwanzo wa Uislamu katika karne bora. Na Shiy´ah bila ya shaka ni kampeni katika kampeni za mayahudi wanaotaka kuuharibu Uislamu kwa madai ya kutumia jina la Uislamu, wanasema ni kuwapenda Waislamu na kuhifadhi athari zao na mfano wa madai kama hayo katika shubuha za Kishaytwaan. Na anayewakataza wanasema huyu ni Wahhaabiy. Hii ndio Dini ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sio Dini ya Wahhaabiyyah bali ni Dini ya Muhammad na yeye ndiye kaamrisha hili. Hizi zote ni nususi kuhusu picha, na Hadiyth hizi zipo katika Swahiyh al-Bukhaariy na Muslim. Hakuna njia ya kuwekea shaka (Hadiyth hizi), ni Hadiyth maana yake iko wazi kabisa. Lakini wanachuoni wa sasa wahakiki wamevua zile picha ambazo ni za dharurah, itakuwa inaruhusiwa kwa dharurah, kama kwa mfano picha ya kitambulisho n.k. Hizi ni za dharurah kiasi cha dharurah itavyokuwa. Ama picha za kumbukumbu, kuadhimisha wapigwa picha n.k., hizi hazijuzu kwa hali yoyote ile. Picha hupigwa wakati wa dharurah tu.

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kapokea ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:
“Allaah Kasema: “Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule ambaye anajaribu kuumba mfano wa viumbe Vyangu? Waache waumbe chembe, au waumbe nafaka, au waache waumbe nafaka ya shayiri.'” (Kaipokea al-Bukhaariy na Muslim)

Wamepokea pia kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wanaoiga uumbaji wa Allaah.”

Wamepokea pia kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalia kila picha aliyoitengeneza nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake katika Moto wa Jahannam.”

Wamepokea (al-Bukhaariy na Muslim) tena kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allahu ´anhumaa) Hadiyth ya Marfuu´:
“Atakayetengeneza picha duniani atakalifishwa kuitia roho na hatoweza kufanya hivyo.”

Muslim kapokea kutoka kwa Abu Hayyaaj (al-Asadiy) ya kwamba ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) alimwambia:
“Hivi nikutumie ujumbe kama vile alivyonituma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Nao ni kuwa usiache picha hata moja isipokuwa umeifutilia mbali wala kaburi lililoinuka isipokuwa ulisawazishe.”

MAELEZO

Mlango huu ni kuhusu matishio makali yaliyokuja kuhusu wetengeneza picha na makatazo ya picha. Hilo, ni kwa sababu picha ni katika njia zinazopelekea katika Shirki. Ikiadhimishwa picha na kutundikwa – na khaswa picha za wakuu na watu wema – zikatundikwa, hakika ni katika njia zinazopelekea katika Shirki, kama ilivyokuwa katika watu wa Nuuh.

Hakika mwanzo wa Shirki kabisa ilivoanza katika ardhi ni kwa sababu ya picha. Hapo ilikuwa pindi walipokufa watu wema katika watu wa Nuuh ambao walikuwa wameshikamana na ´Ibaadah, elimu na Da´wah katika Dini ya Allaah, watu hawa walipokufa wakawa na huzuni kubwa juu yao. Walikufa katika mwaka mmoja. Akawajia Shaytwaan na kuwaambia: “Tengenezeni sura (picha) zao ili muweze kukumbuka hali zao, na ziweze kuwasaidia katika ´Ibaadah.” Alikuja kwa njia ya kuwapa nasaha kwa madai yake. Hawakuwaambia: “Tengenezeni ili muwaabudu”, isipokuwa aliwaambia kwa sababu ziweze kuwasaidia katika ´Ibaadah na kukumbuka hali zao pindi mtapoona picha zao kisha mzitundike katika vikao vyenu. Yeye alikuwa anakusudia Mustaqbal (huko mbeleni) kwa kujua kwake kuwa kizazi hichi hakiwezi kuabudu picha, ndani yake kulikuwemo wanachuoni. Lakini huko mbele kutakuja kizazi cha wajinga, hapo ndipo akawajia Shaytwaan na kuwaambia: “Hakika baba zenu hawakutengeneza picha haya isipokuwa ni kwa sababu ziko na baraka, zinaathiri na kunufaisha.” Akawa amewadanganya namna hii ya kuwa picha hizi zinanufaisha na kudhuru, kwa kuwa zimenasibishwa kwa ajili ya ´Ibaadah. Hivyo, wakawa wameziabudu badala ya Allaah. Hapa ndio Shirki ikawa imeanza.
Allaah Akamtuma Mtume Wake Nuuh (´alayhis-Salaam) awalinganie katika kumuabudu Allaah Pekee asiyekuwa na mshirika na kuacha Shirki. Wakakataa.

وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ
”Wakasema: “Msiwaache miungu yenu.” (Nuuh 71:23)

yaani msiache picha hizi.

وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا
”Na wala msimwache Waddaa, na wala Su’waa’a, na wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa.” (Nuuh 71:23)

Haya ni majina ya watu wema ambao zilitengenezwa picha zao na wakaabudiwa badala ya Allaah. Na wakausiana kutoacha kuwaabudu na kumuasi Nuuh (´alayhis-Salaam).

Shirki ikawa imezuka kwa ajili ya picha na kuadhimisha picha. Kwa ajili hiyo, ndio maana mwandishi akawa ametenga mlango huu katika kitabu cha Tawhiyd. Kwa kuwa kitabu hichi kinabainisha Tawhiyd na Shirki, sababu za Shirki na njia zake. Hii ndio sababu, ya kwamba picha ni katika njia za Shirki, kwa kuwa ni kuiga viumbe vya Allaah (´Azza wa Jalla). Kwa kuwa mtengeneza picha anataka kupatikane sura inayofanana na sura Aliyoiumba Allaah. Anajaribu kufanya hivi. Kuna ushirikisho wa Allaah katika jambo ambalo ni maalum Kwake Pekee ambalo ni Kuumba. Kwa kuwa hakuna awezae kuumba isipokuwa Allaah (´Azza wa Jalla). Huyu mtengeneza picha anajaribu kushirikiana na Allaah katika Kuumba Kwake na kupatikane picha inayofanana na Aliyoumba Allaah. Hili ni jambo la khatari.

Na wala haijuzu kufanya picha kwa viumbe vyenye roho. Ama kufanya picha ya viumbe visivyokuwa na roho, kama miti, nyumba, gari na kadhalika hakuna ubaya. Kwa kuwa hakuna kipingamizi. Makatazo ni kufanya picha ya kiumbe chenye roho katika wanaadamu, minyama na kila kiumbe chenye roho. Haya ndio yamekatazwa. Hii ndio sababu ya kutajwa mlango huu katika kitabu cha Tawhiyd kwa kuwa picha ni katika njia zinazopelekea katika Shirki, kama ilivokuwa katika watu wa Nuuh.

Hadiyth “Allaah Kasema: “Ni nani dhalimu…”, yaani hakuna yeyote ambaye ni dhalimu mkubwa kama mtu huyu. Kwa kuwa Shirki ndio aina kubwa ya dhuluma.

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ
”Hakika shirki ni dhulma kubwa mno!” (Luqmaan 31:13)

Na hii ni katika njia ya Shirki. Yaani mtu huyu anatengeneza picha na anataka kutoka katika picha hiyo kufananisha na viumbe vya Allaah (´Azza wa Jalla). Picha hiyo anaifanya kuwa na kiwiliwili, uso, macho, mdomo n.k. kama kilivo kiumbe cha Allaah (´Azza wa Jalla). Namna hii. Yaani anaumba sura, anataka kuumba kama kiumbe cha Allaah. Huyu ndiye dhalimu mkubwa. Mtengeneza picha ndiye dhalimu mkubwa. Allaah Atukinge. Allaah Kawapa changamoto na Kuwaambia: “Waache waumbe chembe, au waumbe nafaka, au waache waumbe nafaka ya shayiri.'” Pengine wakatengeneza picha, lakini hawawezi kuipulizia roho na kuifanya ikawa kama kiumbe cha Allaah, kinatembea, kinachukua kitu, kinaongea. Hawawezi kufanya hivi. Wanachoweza ni kuigiza tu. Hawawezi hilo.

“Watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wanaoiga uumbaji wa Allaah.” Na haya ni matishio mengine. Ya kwanza ilikuwa kwamba wao ndio madhalimu wakubwa, na haya ya pili ni kwamba ndio watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah. Mtengeneza picha. Huyu ndiye atakayekuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah, kwa kuwa kitendo chake hichi ni njia inayopelekea katika Shirki na kutaka kushirikiana pamoja na Allaah katika kuumba Kwake.

“Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalie kila picha aliyoitengeneza nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam.” Haya ni matishio ya tatu kwa wale wenye kutengeneza picha. Kasema kila mtengeneza picha, sawa ikiwa katengeneza (kafanya picha hiyo) kwa kunakili, au katengeneza picha kwa kuchora na mkono, au kwa kifaa cha Camera. Kila mtengeneza picha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuvua kitu katika hayo, ni yeyote katika wanaotengeneza picha, sawa ikiwa katumia njia yoyote ile ya kufanya picha.

Wale wanaosema kuwa picha za Digital Camera hazina ubaya, inawafedhehesha Hadiyth hii. Kwa kuwa Mtume hapa hakuvua kitu. Kasema “kila mtengeneza picha”, kila mwenye kufanya picha bila kujali katumia njia ipi. Kapewa tishio la Moto.

“Kila mwenye kutengeneza picha atakuwa Motoni. Ataijaalia kila picha aliyoitengeneza nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam.” Hili ni tishio la nne. Ataijaalia kila picha aliyoitengeneza kuipa nafsi, ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam. Ataadhibiwa kwa kila picha aliyoitengeneza. Ikiwa alitengeneza picha mia, atazijaalia nafsi mia. Ikiwa alitengeneza picha milioni, atazijaalia nafsi milioni. Kwa kila picha ataadhibiwa kwa ajili yake kwenye Moto wa Jahannam. Allaah Atukinge. Je, hivi kweli kuna matishio makali zaidi ya haya? Mtu yuko katika afya, Alhamdulillaah, asiingize nafsi yake katika yaharamu. Mtu aache mambo ya picha. Hili ni jambo la khatari sana. Kadiri ya idadi ya wingi wa picha ndio jinsi adhabu itakuwa kubwa.

“Atakayetengeneza picha duniani atakalifishwa kuitia roho na hatoweza kufanya hivyo.” Hili ni tishio la tano. Ya kwamba mpiga picha siku ya Qiyaamah ataambiwa: “Kitie roho ulichokiumba, kipulizie roho.” Na hatoweza kufanya hivi kwa kuwa roho.

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي
”Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: “Roho ni katika amri ya Mola wangu.” (al-Israa 17:85)

Hakuna yeyote awazae kupulizia picha roho, akaifanya ikatembea. Hata hivyo, ataamrishwa kufanya hivyo kwa ajili ya kutaka kumuadhibu.

“Hivi nikutumie ujumbe kama vile alivyonituma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Nao ni kuwa usiache picha hata moja isipokuwa umeifutilia mbali wala kaburi lililoinuka isipokuwa ulisawazishe.” Hapa kuna ubainisho wa nini kinachofanywa na picha, ya kwamba ni wajibu kuichana chana. Huku ni katika kuondosha munkari. Huu ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtuma ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu), akamuamrisha na kumuusia asiache picha hata moja isipokuwa aifutilie mbali. Hapa kamwambia “usiache picha hata moja” hakukuvuliwa kitu hata kimoja. Hali kadhalika kaburi lililoinuka, yaani kujengewa na kuadhimishwa isipokuwa alisawazishe, yaani aliweke sawa na alifanye kama makaburi mengine ya Waislamu. Isijengewe, isiandikwe kitu, isipambwe na kadhalika. Kwa kuwa hii ni njia inayopelekea katika Shirki. Wakati Shiy´ah waliposhika utawala Misri na katika miji mingi ya Waislamu ndio kukazushwa kuyajengea makaburi na likaenea hili katika miji ya Waislamu kwa sababu ya Shiy´ah al-Faatwimiyyuun, vinginevyo hili lilikuwa ni jambo lisilojulikana mwanzo wa Uislamu katika karne bora. Na Shiy´ah bila ya shaka ni kampeni katika kampeni za mayahudi wanaotaka kuuharibu Uislamu kwa madai ya kutumia jina la Uislamu, wanasema ni kuwapenda Waislamu na kuhifadhi athari zao na mfano wa madai kama hayo katika shubuha za Kishaytwaan. Na anayewakataza wanasema huyu ni Wahhaabiy. Hii ndio Dini ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sio Dini ya Wahhaabiyyah bali ni Dini ya Muhammad na yeye ndiye kaamrisha hili.

Hizi zote ni nususi kuhusu picha, na Hadiyth hizi zipo katika Swahiyh al-Bukhaariy na Muslim. Hakuna njia ya kuwekea shaka (Hadiyth hizi), ni Hadiyth maana yake iko wazi kabisa. Lakini wanachuoni wa sasa wahakiki wamevua zile picha ambazo ni za dharurah, itakuwa inaruhusiwa kwa dharurah, kama kwa mfano picha ya kitambulisho n.k. Hizi ni za dharurah kiasi cha dharurah itavyokuwa. Ama picha za kumbukumbu, kuadhimisha wapigwa picha n.k., hizi hazijuzu kwa hali yoyote ile. Picha hupigwa wakati wa dharurah tu.


  • Author: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan. Sharh Kitaab-ut-Tawhiyd, uk. 253-257
  • Kitengo: Uncategorized , Picha
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 6th, November 2013