Mkutano Wa Shaykh al-Albaaniy Na Shaykh Ibn ´Uthamiyn

Swali: Mmeshawahi kukutana na Shaykh Muhammad bin ´Uthaymiyn katika mkutano wa kielimu au wa kawaida? Imaam al-Albaaniy: Nilipata heshima kwa kupata mgeni wake nyumbani kwa mkwe wangu Dr. Ridhwaa Na´saan Makkah. Nadhani ilikuwa wakati wa Hajj. Muulizaji: Hamjawahi kukutana wakati mwingine tena? Imaam al-Albaaniy: Siwezi kukumbuka zaidi ya mara hii. Muulizaji: Kama kwamba nadhani alinambia ni wakati ulipita ´Unayzah na Buraydah... Imaam al-Albaaniy: Ni kweli. Ila sidhani kama nilikutana nae. Muulizaji: Nadhani hata mlikunywa kahawa nyumbani kwake. Imaam al-Albaaniy: Sikumbuki. Yeye ndiye aliyekwambia? Muulizaji: Ndio na alinambia kuwa ulikuwa na Zuhayr ash-Shaawaysh. Imaam al-Albaaniy: Ndio ni kweli nilikuwa kule na Zuhayr ash-Shaawaysh. Inawezekana ilikuwa ni wakati ilikuwa sijamjui Shaykh vizuri. Inawezekana ndio maana sikuweza kumkumbuka, tofauti wakati alinizuru Makkah. Mimi nakumbuka hilo vizuri. Alikuwa na wanafunzi wawili. Mmoja wao aliniuliza swali kuhusiana na elimu ya Hadiyth. Kwa kweli napenda tabia ya Shaykh, urafiki wake, maadili yake na jinsi anavyofanya awezavyo kwa kuepuka Taqliyd [kufuata kichwa mchunga] tofauti na maulamaa wengi katika miji yote.

Swali:
Mmeshawahi kukutana na Shaykh Muhammad bin ´Uthaymiyn katika mkutano wa kielimu au wa kawaida?

Imaam al-Albaaniy:
Nilipata heshima kwa kupata mgeni wake nyumbani kwa mkwe wangu Dr. Ridhwaa Na´saan Makkah. Nadhani ilikuwa wakati wa Hajj.

Muulizaji:
Hamjawahi kukutana wakati mwingine tena?

Imaam al-Albaaniy:
Siwezi kukumbuka zaidi ya mara hii.

Muulizaji:
Kama kwamba nadhani alinambia ni wakati ulipita ´Unayzah na Buraydah…

Imaam al-Albaaniy:
Ni kweli. Ila sidhani kama nilikutana nae.

Muulizaji:
Nadhani hata mlikunywa kahawa nyumbani kwake.

Imaam al-Albaaniy:
Sikumbuki. Yeye ndiye aliyekwambia?

Muulizaji:
Ndio na alinambia kuwa ulikuwa na Zuhayr ash-Shaawaysh.

Imaam al-Albaaniy:
Ndio ni kweli nilikuwa kule na Zuhayr ash-Shaawaysh. Inawezekana ilikuwa ni wakati ilikuwa sijamjui Shaykh vizuri. Inawezekana ndio maana sikuweza kumkumbuka, tofauti wakati alinizuru Makkah. Mimi nakumbuka hilo vizuri.

Alikuwa na wanafunzi wawili. Mmoja wao aliniuliza swali kuhusiana na elimu ya Hadiyth. Kwa kweli napenda tabia ya Shaykh, urafiki wake, maadili yake na jinsi anavyofanya awezavyo kwa kuepuka Taqliyd [kufuata kichwa mchunga] tofauti na maulamaa wengi katika miji yote.


  • Author: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (301)
  • Kitengo: Uncategorized , Mchanganyiko
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 18th, October 2013