Mkutano Kati Ya Muqbil al-Waadi´iy, Raisi Wa Yemen Na az-Zindaaniy

Watu wengi wamedanganyika na baadhi ya Madu´aat. Wanaona hina kwenye ndevu, nguo nusu ya muundi na kilemba kimezungushwa na wanasema "Huyu ni mlinganiaji katika Uislamu". Nyinyi - majini - lazima muwe na aina hii ya watu. Siwezi kuwapa mfano kutoka kwenu, kwa kuwa sijui hali yenu. Nitawapa mfano wa Hizbiyyuun wanaopatikana huku kwetu na jinsi wanavyopotosha maneno. Mimi na ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy tulikuwa kwa raisi. Nikawaambia: "Ninawapa changamoto. Mnasema kuwa sisi, Ahl-us-Sunnah, tuna msimamo mkali. Ninawapa changamoto nyote wawili mthibitishe dalili ya kuwa tuko na msimamo mkali." Raisi akakaa kimya na apewe pongezi kwa hilo. Ama ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy, akasema: "Dalili yangu ni kwamba unazungumzia juu watu." Nikamwambia: "Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kumwambia Mu´aadh: "Mu´aadh! Wewe ni mtu unayewatia watu katika mtihani"? Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia kumwambia Abu Dharr: "Wewe ni mtu ambaye kunapatikana athari ya Jaahiliyyah kwako." Raisi akageuka kwa ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy ili apate jibu kwa hilo. ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy akajibu kwa kusema: "Dalili hizi zimefutwa." Nataka hii ichezwe ili wanachuoni wa Kiislamu ambao wanawatetea Hizbiyyuun wasikie hili na waone jinsi wanavyohukumu dalili. ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy! Ni nani amesema hili kabla yako? Kasema kuwa dalili hizi zimefutwa. Waulize wanachuoni hata kama ni mwenye kufanikiwa.

Watu wengi wamedanganyika na baadhi ya Madu´aat. Wanaona hina kwenye ndevu, nguo nusu ya muundi na kilemba kimezungushwa na wanasema “Huyu ni mlinganiaji katika Uislamu”. Nyinyi – majini – lazima muwe na aina hii ya watu. Siwezi kuwapa mfano kutoka kwenu, kwa kuwa sijui hali yenu. Nitawapa mfano wa Hizbiyyuun wanaopatikana huku kwetu na jinsi wanavyopotosha maneno.

Mimi na ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy tulikuwa kwa raisi. Nikawaambia:

“Ninawapa changamoto. Mnasema kuwa sisi, Ahl-us-Sunnah, tuna msimamo mkali. Ninawapa changamoto nyote wawili mthibitishe dalili ya kuwa tuko na msimamo mkali.”

Raisi akakaa kimya na apewe pongezi kwa hilo. Ama ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy, akasema:

“Dalili yangu ni kwamba unazungumzia juu watu.”

Nikamwambia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kumwambia Mu´aadh:

“Mu´aadh! Wewe ni mtu unayewatia watu katika mtihani”?

Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia kumwambia Abu Dharr:

“Wewe ni mtu ambaye kunapatikana athari ya Jaahiliyyah kwako.”

Raisi akageuka kwa ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy ili apate jibu kwa hilo. ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy akajibu kwa kusema:

“Dalili hizi zimefutwa.”

Nataka hii ichezwe ili wanachuoni wa Kiislamu ambao wanawatetea Hizbiyyuun wasikie hili na waone jinsi wanavyohukumu dalili. ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy! Ni nani amesema hili kabla yako? Kasema kuwa dalili hizi zimefutwa. Waulize wanachuoni hata kama ni mwenye kufanikiwa.