Mkono Wa Kulia Wa Allaah

Mkono wa Allaah wa kulia ni Sifa iliyothibitishwa. Ana Mikono miwili halisi. Katika moja ya upokezi wa Muslim kumethibitishwa yote miwili Mkono wa Allaah wa kulia na wa kushoto. Kuna wanachuoni wanaosema kwamba khabari hii haijathibitishwa na kwamba khabari iliyothibitishwa ni "Mkono Wake mwingine" badala ya "wa kulia". Kwa hali yoyote, khabari hii haipingani na khabari hii: "Mikono yote ya Mola Wangu ni ya kulia." Wanachuoni wamefafanua makusudio ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa Hadiyth hii, yaani ili mtu asifikirie ya kwamba kuna upungufu katika Hadiyth hiyo nyingine. Baadhi ya watu wanaweza kufikiria ya kwamba huyo Mkono wa kushoto au mwingine sio mkamilifu kama wa kulia. Mkono wa Allaah wa kulia umethibitishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala) Kasema: وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ “Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’ala (Ametakasika na Ametukuka kwa ‘Uluwwa) kutokana na yale (yote) wanayomshirikisha.” Katika Aayah hii wanaradiwa Mu'attwilah ambao wanasema kuwa Mkono wa kuthibitishwa unapelekea katika kufananisha na viumbe. Vipi mtu wa busara ambaye atazingatia Aayah hii na kusoma jinsi Mkono wa Allaah umeelezwa kwa njia hii kubwa na kamilifu (anaweza) kusema kwamba maana yake ni kufananisha na viumbe mtu akithibitisha Mkono wa Allaah kama mkono halisi? Isitoshe, jina zinazoendana sambamba kwa mambo mawili haina maana kuwa uhakika wake ni sawa. Ikiwa hali ni hivyo kati ya viumbe, tofauti ni kubwa zaidi kati ya Muumba na kiumbe. Mwandishi: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad Chanzo: at-Tuhfah as-Saniyyah, uk. 41-42

Mkono wa Allaah wa kulia ni Sifa iliyothibitishwa. Ana Mikono miwili halisi. Katika moja ya upokezi wa Muslim kumethibitishwa yote miwili Mkono wa Allaah wa kulia na wa kushoto. Kuna wanachuoni wanaosema kwamba khabari hii haijathibitishwa na kwamba khabari iliyothibitishwa ni “Mkono Wake mwingine” badala ya “wa kulia”.

Kwa hali yoyote, khabari hii haipingani na khabari hii:
“Mikono yote ya Mola Wangu ni ya kulia.”

Wanachuoni wamefafanua makusudio ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwa Hadiyth hii, yaani ili mtu asifikirie ya kwamba kuna upungufu katika Hadiyth hiyo nyingine. Baadhi ya watu wanaweza kufikiria ya kwamba huyo Mkono wa kushoto au mwingine sio mkamilifu kama wa kulia.

Mkono wa Allaah wa kulia umethibitishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala) Kasema:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
“Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’ala (Ametakasika na Ametukuka kwa ‘Uluwwa) kutokana na yale (yote) wanayomshirikisha.”

Katika Aayah hii wanaradiwa Mu’attwilah ambao wanasema kuwa Mkono wa kuthibitishwa unapelekea katika kufananisha na viumbe. Vipi mtu wa busara ambaye atazingatia Aayah hii na kusoma jinsi Mkono wa Allaah umeelezwa kwa njia hii kubwa na kamilifu (anaweza) kusema kwamba maana yake ni kufananisha na viumbe mtu akithibitisha Mkono wa Allaah kama mkono halisi?

Isitoshe, jina zinazoendana sambamba kwa mambo mawili haina maana kuwa uhakika wake ni sawa. Ikiwa hali ni hivyo kati ya viumbe, tofauti ni kubwa zaidi kati ya Muumba na kiumbe.

Mwandishi: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
Chanzo: at-Tuhfah as-Saniyyah, uk. 41-42


  • Kitengo: Uncategorized , Mikono ya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013