Mkataba Wa al-Imaam Na Raafidhwah Wa Yemen

Nimesoma aliyoandika Shaykh 'Arafaat bin Hasan al-Muhammadiy kuhusiana na Khutbah iliyosisitiza makubaliano kati ya Muhammad al-Imaam na maadui wa Allaah, Mtume Wake, Maswahabah zake na maadui wa Ahl-us-Sunnah Raafidhwah Huuthiyyah. Uadui huo unajulikana na wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah, wanafunzi na hata watu wengi wa kawaida wa Kiislamu. Hata Muhammad al-Imaam anaujua vizuri sana. Vitabu vya Raafidhwah vimejaa matusi mengi na Takfiyr kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Ahl-us-Sunnah, upotoshaji wa Qur-aan na ukanushaji wa Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zilizoandikwa kwenye al-Bukhaariy, Muslim na vitabu vingine vya Sunan. Miongoni mwa maneno ya maimamu wao ni pamoja na yale yaliyosemwa na Zindiyq na Raafidhwiy Ni'matullah al-Jazaairiy kuhusu Raafidhwah: "Hatuna mungu mmoja, mtume au kiongozi kama wao (Ahl-us-Sunnah). Kwa sababu wanasema Mola Wao ana Mtume aitwaye Muhammad ambaye ana Khaliyfah aitwaye Abu Bakr. Hatumuamini Mola wala Mtume kama huo. Sisi kwa hakika tunasema Mola ambaye Khaliyfah wa Mtume Wake ni Abu Bakr sio Mola Wetu na Mtume huyo sio Mtume wetu." Muhammad al-Imaam anayajua haya kikamilifu. Yeye mwenyewe aliyaandika kwenye kitabu chake dhidi ya Raafidhwah Huuthiyyah kiitwacho "al-Nusrah Yamaaniyyah". Ana ujuzi wa upotevu wao mwingi. Nafikiria kuwa anatambua jinsi makubaliano ambayo yameipiga Sunnah na Ahl-us-Sunnah, yalivo. Wamekasirikishwa sana kwa hilo na wamelikemea kwa njia kali sana. Mkataba huo umewafurahisha maadui na kuutumia kuwatukana Salafiyyuun na ´Aqiydah na mfumo wao. Matokeo yake, wamewatuhumu kuwa wana udugu na Raafidhwah na wamefikia mpaka kumkufurisha Muhammad al-Imaam. Wameitakasa Takfiyr yao juu ya Salafiyyuun kwa sababu ya mkataba huu. Ni wajibu kwa Muhammad al-Imaam kusitisha mkataba huu wa batili ambao unaingia katika maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Kila sharti isiyokuwepo katika Kitabu cha Allaah ni batili hata kama itakuwa ni sharti mia.” Salafiyyuun wanasubiri kwa hamu kubwa kutangazwa huku. Hivyo ni lazima kwa al-Imaam haraka atangaze yale ambayo Uislamu umemlazimu na kumuokoa na kosa lake na Khasira za Mwingi wa Rahmah. Mwandishi: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy Chanzo: at-Ta'kiyd li Ghalat-il-Wathiyqah wa ma ihtawathu Khutbat-ul-´Iyd, uk. 1 Toleo la: 15-08-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Nimesoma aliyoandika Shaykh ‘Arafaat bin Hasan al-Muhammadiy kuhusiana na Khutbah iliyosisitiza makubaliano kati ya Muhammad al-Imaam na maadui wa Allaah, Mtume Wake, Maswahabah zake na maadui wa Ahl-us-Sunnah Raafidhwah Huuthiyyah. Uadui huo unajulikana na wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah, wanafunzi na hata watu wengi wa kawaida wa Kiislamu. Hata Muhammad al-Imaam anaujua vizuri sana. Vitabu vya Raafidhwah vimejaa matusi mengi na Takfiyr kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Ahl-us-Sunnah, upotoshaji wa Qur-aan na ukanushaji wa Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zilizoandikwa kwenye al-Bukhaariy, Muslim na vitabu vingine vya Sunan.

Miongoni mwa maneno ya maimamu wao ni pamoja na yale yaliyosemwa na Zindiyq na Raafidhwiy Ni’matullah al-Jazaairiy kuhusu Raafidhwah:

“Hatuna mungu mmoja, mtume au kiongozi kama wao (Ahl-us-Sunnah). Kwa sababu wanasema Mola Wao ana Mtume aitwaye Muhammad ambaye ana Khaliyfah aitwaye Abu Bakr. Hatumuamini Mola wala Mtume kama huo. Sisi kwa hakika tunasema Mola ambaye Khaliyfah wa Mtume Wake ni Abu Bakr sio Mola Wetu na Mtume huyo sio Mtume wetu.”

Muhammad al-Imaam anayajua haya kikamilifu. Yeye mwenyewe aliyaandika kwenye kitabu chake dhidi ya Raafidhwah Huuthiyyah kiitwacho “al-Nusrah Yamaaniyyah”. Ana ujuzi wa upotevu wao mwingi. Nafikiria kuwa anatambua jinsi makubaliano ambayo yameipiga Sunnah na Ahl-us-Sunnah, yalivo. Wamekasirikishwa sana kwa hilo na wamelikemea kwa njia kali sana. Mkataba huo umewafurahisha maadui na kuutumia kuwatukana Salafiyyuun na ´Aqiydah na mfumo wao. Matokeo yake, wamewatuhumu kuwa wana udugu na Raafidhwah na wamefikia mpaka kumkufurisha Muhammad al-Imaam. Wameitakasa Takfiyr yao juu ya Salafiyyuun kwa sababu ya mkataba huu. Ni wajibu kwa Muhammad al-Imaam kusitisha mkataba huu wa batili ambao unaingia katika maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kila sharti isiyokuwepo katika Kitabu cha Allaah ni batili hata kama itakuwa ni sharti mia.”

Salafiyyuun wanasubiri kwa hamu kubwa kutangazwa huku. Hivyo ni lazima kwa al-Imaam haraka atangaze yale ambayo Uislamu umemlazimu na kumuokoa na kosa lake na Khasira za Mwingi wa Rahmah.

Mwandishi: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Chanzo: at-Ta’kiyd li Ghalat-il-Wathiyqah wa ma ihtawathu Khutbat-ul-´Iyd, uk. 1
Toleo la: 15-08-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Imaam, Muhammad bin ´Abdillaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 14th, August 2014