Mkataba Kati Ya Muhammad al-Imaam Na Raafidhwah Wa Yemen

Himdi zote ni Zake Allaah: إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ “Hakika Waumini ni ndugu.” (49:10) Allaah Mtukufu Amesema kweli. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad na ukoo wake safi na awe radhi juu ya Maswahabah zake wazuri kati ya Muhaajiruun na Answaar na wale wenye kuwafuata kwa wema. Sote ni Waislamu. Mola wetu ni mmoja, kitabu chetu ni kimoja, Mtume wetu ni mmoja na adui yetu ni mmoja hata kama tuna tofauti kati ya mambo madogo madogo. Sisi kama Waislamu Uislamu umetukataza kukiuka maisha kati yetu, heshima na mali. Kutokana na haya, kumekhitimishwa mkataba kati ya msaidizi wa Allaah, akiwakilishwa kama ´Abdul-Maalik Badr-ud-Diyn al-Huuthiy, na Salafiyyuun katika markaz ya Nuur Ma´bar na markaz zingine zote zilizoko chini yake, zenye kuwakilishwa na Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam, kuhusiana na nukta zifuatazo: 1- Maisha ya amani baina ya pande zote mbili pasina magonvi, mapigano na fitina pasina kujali hali na sababu itakavokuwa pamoja na uhuru wa fikira na wa utamaduni kwa wote. 2- Pande zote mbili zisitukanane kwa kuchokozana na uadui pasina kujali njia na nafasi. Badala yake kufanyiwe kazi udugu na kushirikiana kati ya kila mtu. 3- Kuendelea na mchakato wa mawasiliano wa moja kwa moja kati ya pande zote mbili ili kukabiliana na aina yoyote ya janga, ajali, tatizo au mwenendo wa mtu au jaribio lolote kutoka kwa upande mwingine ili kuharibu uhusiano wa pande zote mbili. Mkataba huu umetimizwa 1435-08-28/2014-06-26 Upande wa kwanza: ´Abdul-Maalik Badr-ud-Diyn al-Huuthiy Upande wa pili: Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam

Himdi zote ni Zake Allaah:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ
“Hakika Waumini ni ndugu.” (49:10)

Allaah Mtukufu Amesema kweli. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad na ukoo wake safi na awe radhi juu ya Maswahabah zake wazuri kati ya Muhaajiruun na Answaar na wale wenye kuwafuata kwa wema.

Sote ni Waislamu. Mola wetu ni mmoja, kitabu chetu ni kimoja, Mtume wetu ni mmoja na adui yetu ni mmoja hata kama tuna tofauti kati ya mambo madogo madogo. Sisi kama Waislamu Uislamu umetukataza kukiuka maisha kati yetu, heshima na mali. Kutokana na haya, kumekhitimishwa mkataba kati ya msaidizi wa Allaah, akiwakilishwa kama ´Abdul-Maalik Badr-ud-Diyn al-Huuthiy, na Salafiyyuun katika markaz ya Nuur Ma´bar na markaz zingine zote zilizoko chini yake, zenye kuwakilishwa na Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam, kuhusiana na nukta zifuatazo:

1- Maisha ya amani baina ya pande zote mbili pasina magonvi, mapigano na fitina pasina kujali hali na sababu itakavokuwa pamoja na uhuru wa fikira na wa utamaduni kwa wote.

2- Pande zote mbili zisitukanane kwa kuchokozana na uadui pasina kujali njia na nafasi. Badala yake kufanyiwe kazi udugu na kushirikiana kati ya kila mtu.

3- Kuendelea na mchakato wa mawasiliano wa moja kwa moja kati ya pande zote mbili ili kukabiliana na aina yoyote ya janga, ajali, tatizo au mwenendo wa mtu au jaribio lolote kutoka kwa upande mwingine ili kuharibu uhusiano wa pande zote mbili.

Mkataba huu umetimizwa

1435-08-28/2014-06-26

Upande wa kwanza:

´Abdul-Maalik Badr-ud-Diyn al-Huuthiy

Upande wa pili:

Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam