Mioyo Ya Waja Kuwa Baina Ya Vidole Viwili Katika Vidole Vya Allaah Haihitajii Kugusana

Mfano mwingine wa pili ni Hadiyth: "Mioyo ya waja (binaadamu) iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Ar-Rahmaan." Hadiyth hii ni Swahiyh. Iko katika "Swahiyh Muslim" katika mlango "al-Qadr" na imesimuliwa na 'Abdullaah bin 'Amr bin al-´Aasw. Salaf, Ahl-us-Sunnah, wanaifahamu Hadiyth hii kwa udhahiri wake (Dhwaahir-ul-Hadiyth). Wanasema kwamba mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah (Ta´ala) kwa njia ya kweli (halisi). Tunathibitisha hilo kwa njia ile ile kama jinsi Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Alivyovithitisha Kwake. Kwamba mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah, haihitajii kwamba (mioyo) inavigusa (Vidole vya Allaah) mtu akaelewa kwamba Hadiyth ina pantheism (Huluul) na matukio yake ikaja kuwa ufahamu wa kimakosa. Mwezi uko baina ya mbingu na ardhi, bila ya kugusa chochote katika hivyo. (Mlima wa) Badr uko baina ya Makkah na al-Madiynah ilihali kuna umbali mrefu kati yavyo. Hali kadhalika mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili vya Mwingi wa Rahmah kwa njia ya ukweli (halisi) na haihitajii kugusana wala pantheism . Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn Chanzo: al-Qawaa´id al-Muthlaa, uk. 50-51 ´Aalam-ul-Kutub, 1406/1986

Mfano mwingine wa pili ni Hadiyth:

“Mioyo ya waja (binaadamu) iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Ar-Rahmaan.”

Hadiyth hii ni Swahiyh. Iko katika “Swahiyh Muslim” katika mlango “al-Qadr” na imesimuliwa na ‘Abdullaah bin ‘Amr bin al-´Aasw.

Salaf, Ahl-us-Sunnah, wanaifahamu Hadiyth hii kwa udhahiri wake (Dhwaahir-ul-Hadiyth). Wanasema kwamba mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah (Ta´ala) kwa njia ya kweli (halisi). Tunathibitisha hilo kwa njia ile ile kama jinsi Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) Alivyovithitisha Kwake. Kwamba mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah, haihitajii kwamba (mioyo) inavigusa (Vidole vya Allaah) mtu akaelewa kwamba Hadiyth ina pantheism (Huluul) na matukio yake ikaja kuwa ufahamu wa kimakosa. Mwezi uko baina ya mbingu na ardhi, bila ya kugusa chochote katika hivyo. (Mlima wa) Badr uko baina ya Makkah na al-Madiynah ilihali kuna umbali mrefu kati yavyo.

Hali kadhalika mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili vya Mwingi wa Rahmah kwa njia ya ukweli (halisi) na haihitajii kugusana wala pantheism .

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Chanzo: al-Qawaa´id al-Muthlaa, uk. 50-51
´Aalam-ul-Kutub, 1406/1986


  • Kitengo: Uncategorized , Vidole vya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013