Miongoni Mwa Siasa Ni Kuachana Na Siasa

Tumeona leo jinsi ni miongoni mwa siasa kujitenga mbali na siasa. Sisemi ya kwamba siasa sio katika Dini, hili ni jambo lenye kujulikana [ya kwamba siasa ni katika Dini]. Nasema hivo kwa sababu sisi kwa njia fulani tunafanana na Waislamu Makkah. Katika wakati huo hawakuamrishwa kuhamasisha na kuhajiri na kufanya upinzani wa silaha dhidi ya makafiri washirikina. Kwa nini hawakuwa hivo? Kwa sababu hali zilikuwa hazikutimizwa na nyepesi. Haina maana ya kwamba walikuwa wazembe au hawakufanya ya wajibu kwao kwa kuinusuru Dini na kuifikisha kwa wengine. Hali zilikuwa hazijatimizwa. Kwa njia hii sisi angalau kwa uchache tuko kama wao. Kwa hivyo pindi tunapotaka kufikia lengo hili la haki ni kama jinsi tunavyojiuliza wenyewe ni kwa nini hatupigani Jihaad katika njia ya Allaah. Tokea karibu kila karne makundi mengi yamezungumzia Jihaad. Wamefanya nini? Hakuna. Sisi hatuwalaumu kwa kutokufanya lolote kwa sababu hawawezi kufanya lolote. Pamoja na hivyo kuna mambo mengi ambayo wanaweza kufanya na hawakuyafanya. Wameshughulisha ulimwengu wa Kiislamu na wao wenyewe kwa kitu wasichokiweza badala ya kitu wanachokiweza. Mzungumzaji: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy Chanzo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930) Tarehe: 1417-04-09/1996-08-24 Toleo la: 19-12-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Tumeona leo jinsi ni miongoni mwa siasa kujitenga mbali na siasa. Sisemi ya kwamba siasa sio katika Dini, hili ni jambo lenye kujulikana [ya kwamba siasa ni katika Dini]. Nasema hivo kwa sababu sisi kwa njia fulani tunafanana na Waislamu Makkah. Katika wakati huo hawakuamrishwa kuhamasisha na kuhajiri na kufanya upinzani wa silaha dhidi ya makafiri washirikina. Kwa nini hawakuwa hivo? Kwa sababu hali zilikuwa hazikutimizwa na nyepesi. Haina maana ya kwamba walikuwa wazembe au hawakufanya ya wajibu kwao kwa kuinusuru Dini na kuifikisha kwa wengine. Hali zilikuwa hazijatimizwa. Kwa njia hii sisi angalau kwa uchache tuko kama wao.

Kwa hivyo pindi tunapotaka kufikia lengo hili la haki ni kama jinsi tunavyojiuliza wenyewe ni kwa nini hatupigani Jihaad katika njia ya Allaah. Tokea karibu kila karne makundi mengi yamezungumzia Jihaad. Wamefanya nini? Hakuna. Sisi hatuwalaumu kwa kutokufanya lolote kwa sababu hawawezi kufanya lolote. Pamoja na hivyo kuna mambo mengi ambayo wanaweza kufanya na hawakuyafanya. Wameshughulisha ulimwengu wa Kiislamu na wao wenyewe kwa kitu wasichokiweza badala ya kitu wanachokiweza.

Mzungumzaji: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Chanzo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930)
Tarehe: 1417-04-09/1996-08-24
Toleo la: 19-12-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Jihaad
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 19th, December 2014