Mimi Sio ´Allaamah – Hawa Ndio ´Allaamah!

Napenda kumkumbusha ndugu yangu, na nyinyi mnasikia, kujiepusha na kusifu. Ninasema haya na wallaahi naapa kwamba sipendi hilo na Allaah Anajua yaliyomo ndani mwangu. Mtu husifiwa kwa matendo yake. Mbele ya Allaah kutajitokeza yote ambayo mtu alikuwa akificha. Mimi sio ´Allaamah. Neno hili limeanza kupewa kila mtu leo. ´Allaamah ni Imaam na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz (Rahimahu Allaah) ambaye ni mwalimu wangu na mwalimu wa baadhi ya waliimu zangu. Allaah Amrahamu. ´Allaamah na Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthyamiyn. Allaah Amrahamu. ´Allaamah na Shaykh Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy. Allaah Amrahamu. Kadhalika Shaykh Swaalih al-Fawzaan, Shaykh Rabiy´ bin Haadiy, Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy na Muftiy [´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh]. Hawa ndio wanaitwa “´Allaamah”. Ama mimi, mimi ni mwanafunzi tu. Nilisoma na kunufaisha na bado twaendelea kunufaika. Tunamuomba Allaah (Jalla wa ´Alaa) Aturuzuku sisi na nyinyi elimu yenye manufaa, matendo mema, ufahamu na baswiyrah katika Dini na uthabiti juu ya haki, Uislamu na Sunnah mpaka pale tutapokutana naye.

Napenda kumkumbusha ndugu yangu, na nyinyi mnasikia, kujiepusha na kusifu. Ninasema haya na wallaahi naapa kwamba sipendi hilo na Allaah Anajua yaliyomo ndani mwangu. Mtu husifiwa kwa matendo yake. Mbele ya Allaah kutajitokeza yote ambayo mtu alikuwa akificha. Mimi sio ´Allaamah. Neno hili limeanza kupewa kila mtu leo.

´Allaamah ni Imaam na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz (Rahimahu Allaah) ambaye ni mwalimu wangu na mwalimu wa baadhi ya waliimu zangu. Allaah Amrahamu. ´Allaamah na Shaykh Muhammad bin Swaalih bin ´Uthyamiyn. Allaah Amrahamu. ´Allaamah na Shaykh Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy. Allaah Amrahamu. Kadhalika Shaykh Swaalih al-Fawzaan, Shaykh Rabiy´ bin Haadiy, Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy na Muftiy [´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh]. Hawa ndio wanaitwa “´Allaamah”.

Ama mimi, mimi ni mwanafunzi tu. Nilisoma na kunufaisha na bado twaendelea kunufaika. Tunamuomba Allaah (Jalla wa ´Alaa) Aturuzuku sisi na nyinyi elimu yenye manufaa, matendo mema, ufahamu na baswiyrah katika Dini na uthabiti juu ya haki, Uislamu na Sunnah mpaka pale tutapokutana naye.