Milipuko Inayofanywa Haijawapatia Waislamu Faida Yoyote Zaidi Ya Madhara Juu Ya Madhara

Kuhusiana na yale yanayofanywa na baadhi ya watu kujitoa muhanga kwa kujiweka mabomu na kuwaendea makafiri kisha wanajilipua pindi wanapokuwa kati yao, huku inachukuliwa ni kujiua - na tunaomba kinga kwa Allaah. Mwenye kuiua nafsi yake atadumishwa Motoni milele kama ilivyokuja katika Hadiyth yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huyu aliyeiua nafsi yake hakuleta faida yoyote kwa Waislamu hata kwa wasiokuwa Waislamu. Kwa sababu akiua watu kumi, ishirini, mia au mia mbili, Uislamu haufaidiki chochote kwa hilo. Wala hilo haliwafanyi watu kuingia katika Uislamu. Tofauti na kile kisa cha yule kijana, yeye alisababisha watu wote wakaingia katika Uislamu. Hata hivyo haihitajiki kuua adui kumi, ishirini, mia au mia mbili kwa ajili watu waingie katika Uislamu. Kinyume chake huenda maudhi ya maadui ndiyo yakazidi kuwa mengi. Jambo hili ambalo Waislamu hawa wanafanya linapelekea makafiri kuzidisha maudhi yao dhidi ya Waislamu. Mfano wa hili ni kama sasa jinsi mayahudi wanavofanya dhidi ya wapalestina. Mpalestina mmoja anapojilipua na kuua [mayahudi] sita mpaka saba, matokeo yake wanajilipiza kwa kuua wapalestina sitini, sabini au zaidi. Kwa hali hiyo kunakuwa hakuna faida yoyote kwa Waislamu wala hao waliojilipua. Ndio maana naona yeyote atakayefanya kitendo kama hicho atakuwa amejiua bila ya haki. Hili litasababisha yeye kuingia Motoni - na tunaomba kinga kwa Allaah. Aliyefanya hivo sio shahidi. Lakini ikiwa mtu atafanya kitendo hiki kwa ujinga na huku akifikiria kuwa inajuzu, tunatumai kuwa hatopata madhambi. Hata hivyo hatofikia daraja ya aliyekufa shahidi kwa sababu hakufanya kama anayekufa shahidi anavyopaswa kufanya. Lakini hatopama madhambi kwa kuwa amefanya hivo kwa kufahamu makosa. Yule mwenye kujitahidi na akakosea, anapata thawabu moja. Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Muhammad bin ´Uthaymiyn Chanzo: https://www.youtube.com/watch?v=fanzjyIRjXw Toleo la: 07-12-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Kuhusiana na yale yanayofanywa na baadhi ya watu kujitoa muhanga kwa kujiweka mabomu na kuwaendea makafiri kisha wanajilipua pindi wanapokuwa kati yao, huku inachukuliwa ni kujiua – na tunaomba kinga kwa Allaah. Mwenye kuiua nafsi yake atadumishwa Motoni milele kama ilivyokuja katika Hadiyth yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huyu aliyeiua nafsi yake hakuleta faida yoyote kwa Waislamu hata kwa wasiokuwa Waislamu. Kwa sababu akiua watu kumi, ishirini, mia au mia mbili, Uislamu haufaidiki chochote kwa hilo. Wala hilo haliwafanyi watu kuingia katika Uislamu. Tofauti na kile kisa cha yule kijana, yeye alisababisha watu wote wakaingia katika Uislamu. Hata hivyo haihitajiki kuua adui kumi, ishirini, mia au mia mbili kwa ajili watu waingie katika Uislamu. Kinyume chake huenda maudhi ya maadui ndiyo yakazidi kuwa mengi. Jambo hili ambalo Waislamu hawa wanafanya linapelekea makafiri kuzidisha maudhi yao dhidi ya Waislamu. Mfano wa hili ni kama sasa jinsi mayahudi wanavofanya dhidi ya wapalestina. Mpalestina mmoja anapojilipua na kuua [mayahudi] sita mpaka saba, matokeo yake wanajilipiza kwa kuua wapalestina sitini, sabini au zaidi. Kwa hali hiyo kunakuwa hakuna faida yoyote kwa Waislamu wala hao waliojilipua. Ndio maana naona yeyote atakayefanya kitendo kama hicho atakuwa amejiua bila ya haki. Hili litasababisha yeye kuingia Motoni – na tunaomba kinga kwa Allaah. Aliyefanya hivo sio shahidi.
Lakini ikiwa mtu atafanya kitendo hiki kwa ujinga na huku akifikiria kuwa inajuzu, tunatumai kuwa hatopata madhambi. Hata hivyo hatofikia daraja ya aliyekufa shahidi kwa sababu hakufanya kama anayekufa shahidi anavyopaswa kufanya. Lakini hatopama madhambi kwa kuwa amefanya hivo kwa kufahamu makosa. Yule mwenye kujitahidi na akakosea, anapata thawabu moja.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Muhammad bin ´Uthaymiyn
Chanzo: https://www.youtube.com/watch?v=fanzjyIRjXw
Toleo la: 07-12-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 7th, December 2014