Mhubiri Anayewapenda Watu Wote

Usiwadhanie vizuri watu wote. Mfano wa hilo ni maneno ya mhubiri Mmisri mmoja Muhammad Husayn Ya´quub: "Ninaapa kwa Allaah ya kwamba ninawapenda kwa ajili ya Allaah." Subhaana Allaah! Unawapenda wote kwa ajili ya Allaah? Je, huyu ni mhubiri? Huyu ni mhubiri ambaye amevunja kanuni iliyotajwa kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba tunawapenda tu wema na watu waaminifu ambao wanashikamana na Qur-aan na Sunnah kwa ndani na kwa nje. Ama kuhusiana na wanafiki, wafanya madhambi na wafanya makosa ya jinai, tunawachukia kwa ajili ya Allaah. "Kupenda kwa ajili ya Allaah na kuchukia kwa Allaah ni katika fundo gumu la Imani." Ahmad (18524) Shu´ayb al-Arnaa´uut amesema kuwa ni Hasan kupitia mapokezi mengine yanayoishuhudia. al-Albaaniy amesema kuwa ni Hasan katika "Swahiyh-ul-Jaamiy´". Ikiwa mhubiri huyu anaona kanuni hii kwa njia hii pana na kwamba anawapenda wote kwa ajili ya Allaah, ina maana hakusoma ´Aqiydah. Ingelikuwa amesoma ´Aqiydah asingelitamka namna hii.

Usiwadhanie vizuri watu wote. Mfano wa hilo ni maneno ya mhubiri Mmisri mmoja Muhammad Husayn Ya´quub:

“Ninaapa kwa Allaah ya kwamba ninawapenda kwa ajili ya Allaah.”

Subhaana Allaah! Unawapenda wote kwa ajili ya Allaah? Je, huyu ni mhubiri? Huyu ni mhubiri ambaye amevunja kanuni iliyotajwa kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba tunawapenda tu wema na watu waaminifu ambao wanashikamana na Qur-aan na Sunnah kwa ndani na kwa nje. Ama kuhusiana na wanafiki, wafanya madhambi na wafanya makosa ya jinai, tunawachukia kwa ajili ya Allaah.

“Kupenda kwa ajili ya Allaah na kuchukia kwa Allaah ni katika fundo gumu la Imani.” Ahmad (18524)

Shu´ayb al-Arnaa´uut amesema kuwa ni Hasan kupitia mapokezi mengine yanayoishuhudia. al-Albaaniy amesema kuwa ni Hasan katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´”.

Ikiwa mhubiri huyu anaona kanuni hii kwa njia hii pana na kwamba anawapenda wote kwa ajili ya Allaah, ina maana hakusoma ´Aqiydah. Ingelikuwa amesoma ´Aqiydah asingelitamka namna hii.


  • Author: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy. al-Bayaan al-Mubiyn, uk. 39-41
  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 15th, January 2014