Mgawanyiko Wa Imaam ash-Shaafi’iy Wa Bid´ah Hauyasapoti Maadhimisho Ya Maulidi

ar-Rifaa'iy kasema: "Kinachothibitisha ya kwamba tendo hili ni Bid´ah nzuri, ni maneno ya ash-Shaafi'iy yaliyopokelewa na al-Bayhaqiy: "Kuna aina mbili ya Bid´ah. Ya kwanza ni ile inayopingana na Qur-aan, Sunnah, mapokezi au Ijmaa´ . Bid´ah hii ni upotofu. Bid´ah ya pili si ile inayopingana na moja katika hayo tuliyotaja. Bid´ah hii sio yenye kulaumiwa. 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) kasema kuhusu Swalah ya usiku katika Ramadhaan: "Bid´ah nzuri ilioje hii!" Jambo la kwanza, sio maoni ya wanachuoni ndio yenye kuamua yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa, kizuri, haramu na kibaya. Dalili ni Qur-aan, Sunnah, Ijmaa´ au kauli ya Swahabah rafiki maadamu haijulikani ya kwamba kuna Swahabah mwingine ana maoni tofauti. Alichosema ash-Shaafi'iy (Rahimahu Allaah) hakitolei dalili uzushi wa Maulidi, au Bid´ah nyingine kwa jambo hilo, kuwa ni nzuri. Kutokana na maneno yake, mtu anapata kuelewa ya kwamba maadhimisho ya Maulidi yamekatazwa kwa vile yanakwenda kinyume na Qur-aan, Sunnah, mapokezi na matendo ya Salaf taarifa na maimamu. Aidha, maneno ya ash-Shaafi'iy yamepokelewa kwa taarifa nyingine. Abu Nu'aym kapokea katika "al-Hilyah" yake kutoka kwa Ibraahiym bin al-Junayd ambaye kasema: Harmalah bin Yahyaa katueleza ambaye kasema kwamba alimsikia Muhammad bin Idriys ash-Shaafi'iy akisema: "Kuna aina mbili ya Bid´ah. Bid´ah inayosifiwa na Bid´ah ya kulaumiwa. Inayokwenda sambamba na Sunnah inasifiwa na inayokwenda kinyume na Sunnah inalaumiwa. " Kisha akatumia hoja kwa maneno ya 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) kuhusu Swalah ya usiku katika Ramadhan: "Bid´ah nzuri ilioje hii!" Ibn Rajab kasema katika 'Jaami'-ul-'Uluum wal-Hikam": "ash-Shaafi'iy anamaanisha ya kwamba msingi wa Bid´ah ya kulaumiwa ni kuwa ni ile inayokosa msingi katika Shari'ah ambao mtu anaweza kuurejelea. Ndio maana ya Bid´ah kwa mujibu wa Shari'ah. Ama kuhusiana na Bid´ah ya kusifiwa, hiyo inayokwenda sambamba na Sunnah. Ina maana ina msingi ambao mtu anaweza kuurejelea. Kwa njia hii, hii ni Bid´ah tu ya kilugha, na sio ya Dini, hivyo inakwenda sambamba na Sunnah." Jambo la pili, uzushi wa Maulidi hauna msingi katika Shari'ah. Jambo hili linapingana na uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Sunnah. Hivyo ni kitendo cha Bid´ah ya kulaumiwa. Jambo la tatu uzushi wa Maulidi unapingana na Qur-aan, Sunnah, mapokezi na matendo ya Salaf na maimamu. Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy ar-Radd al-Qawiy, uk. 44-45

ar-Rifaa’iy kasema:

“Kinachothibitisha ya kwamba tendo hili ni Bid´ah nzuri, ni maneno ya ash-Shaafi’iy yaliyopokelewa na al-Bayhaqiy: “Kuna aina mbili ya Bid´ah. Ya kwanza ni ile inayopingana na Qur-aan, Sunnah, mapokezi au Ijmaa´ . Bid´ah hii ni upotofu. Bid´ah ya pili si ile inayopingana na moja katika hayo tuliyotaja. Bid´ah hii sio yenye kulaumiwa. ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kasema kuhusu Swalah ya usiku katika Ramadhaan: “Bid´ah nzuri ilioje hii!”

Jambo la kwanza, sio maoni ya wanachuoni ndio yenye kuamua yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa, kizuri, haramu na kibaya. Dalili ni Qur-aan, Sunnah, Ijmaa´ au kauli ya Swahabah rafiki maadamu haijulikani ya kwamba kuna Swahabah mwingine ana maoni tofauti. Alichosema ash-Shaafi’iy (Rahimahu Allaah) hakitolei dalili uzushi wa Maulidi, au Bid´ah nyingine kwa jambo hilo, kuwa ni nzuri. Kutokana na maneno yake, mtu anapata kuelewa ya kwamba maadhimisho ya Maulidi yamekatazwa kwa vile yanakwenda kinyume na Qur-aan, Sunnah, mapokezi na matendo ya Salaf taarifa na maimamu.

Aidha, maneno ya ash-Shaafi’iy yamepokelewa kwa taarifa nyingine. Abu Nu’aym kapokea katika “al-Hilyah” yake kutoka kwa Ibraahiym bin al-Junayd ambaye kasema: Harmalah bin Yahyaa katueleza ambaye kasema kwamba alimsikia Muhammad bin Idriys ash-Shaafi’iy akisema:

“Kuna aina mbili ya Bid´ah. Bid´ah inayosifiwa na Bid´ah ya kulaumiwa. Inayokwenda sambamba na Sunnah inasifiwa na inayokwenda kinyume na Sunnah inalaumiwa. ”

Kisha akatumia hoja kwa maneno ya ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuhusu Swalah ya usiku katika Ramadhan:
“Bid´ah nzuri ilioje hii!”

Ibn Rajab kasema katika ‘Jaami’-ul-‘Uluum wal-Hikam”:

“ash-Shaafi’iy anamaanisha ya kwamba msingi wa Bid´ah ya kulaumiwa ni kuwa ni ile inayokosa msingi katika Shari’ah ambao mtu anaweza kuurejelea. Ndio maana ya Bid´ah kwa mujibu wa Shari’ah. Ama kuhusiana na Bid´ah ya kusifiwa, hiyo inayokwenda sambamba na Sunnah. Ina maana ina msingi ambao mtu anaweza kuurejelea. Kwa njia hii, hii ni Bid´ah tu ya kilugha, na sio ya Dini, hivyo inakwenda sambamba na Sunnah.”
Jambo la pili, uzushi wa Maulidi hauna msingi katika Shari’ah. Jambo hili linapingana na uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na Sunnah. Hivyo ni kitendo cha Bid´ah ya kulaumiwa.

Jambo la tatu uzushi wa Maulidi unapingana na Qur-aan, Sunnah, mapokezi na matendo ya Salaf na maimamu.

Mwandishi: ‘Allaamah Hamuud bin ‘Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 44-45


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013