Mfikirie Allaah Wakati Unapokula Na Kunywa

Miongoni mwa adabu za chakula ni mtu kutaja jina la Allaah mwanzoni kabla ya kula na kunywa. Aseme: “Bismillaah.” Aseme hivo ili kumfukuza Shaytwaan. Shaytwaan anakula na kunywa na mwanaadamu. Akimtaja Allaah kabla ya kula na kunywa Shaytwaan humkimbia. Ikiwa hamtaji Shaytwaan hula pamoja naye katika chakula na kinywaji chake. Wakati wa kumaliza kula aseme: “Alhamdulillaah.” Anapomaliza kula na kunywa amhimidi Allaah (´Azza wa Jalla) Aliyemruzuku na Kumsahilishia chakula na kinywaji hichi. Yeye ndiye mwenye kukiendesha chakula na kinywaji hichi kwenye tumbo la mwanaadamu na mishipa yake ili kisiweze kumdhuru. Yote haya ni katika fadhila za Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah Anamruzuku mwanaadamu na kuendesha matumizi yake ili asiweze kudhurika kwacho. Matumizi na uendeshaji, yote mawili ni katika neema ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo amhimidi Allaah kwa neema hizi kubwa. Akumbuke wale walio wagonjwa kwa sababu ya kula na kunywa na hali zao. Hivyo amshukuru na amhimidi Allaah kwa hilo. Muislamu asiwe ni mghafilikaji wa kumdhukuru Allaah. Ikiwa hamdhukuru Allaah anapotea na kuangamia na Shaytwaan anamtawala. Kwa ajili hiyo anatakiwa siku zote kumdhukuru Allaah – wakati anapokula, kunywa, kulala, anapokuwa macho, anapokaa na anapotembea. Awe siku zote ni mwenye kumdhukuru Allaah (´Azza wa Jalla) na khaswa Adhkaar zilizowekwa katika nyakati au hali maalum. Ajifunze nazo na kuzisoma daima. Zinamsaidia katika kumuabudu Allaah na kukabiliana na matatizo ya maisha. Zinamkimbiza Shaytwaan kwake. Zinaupa uhai moyo na kuupa mwanga nafsi yake. Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema: الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللَّـهِ ۗ أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ “Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah. Tanabahi! Kwa kumdhukuru Allaah nyoyo hutulia!” (13:28) Mwanaadamu hatakiwi kusahau kumdhukuru Allaah. Anatakiwa kumdhukuru Allaah siku zote kwa ulimi wake, moyo wake na matendo yake pindi anapokuwa amesimama, amekaa, anatembea na amelala.

Miongoni mwa adabu za chakula ni mtu kutaja jina la Allaah mwanzoni kabla ya kula na kunywa. Aseme:

“Bismillaah.”

Aseme hivo ili kumfukuza Shaytwaan. Shaytwaan anakula na kunywa na mwanaadamu. Akimtaja Allaah kabla ya kula na kunywa Shaytwaan humkimbia. Ikiwa hamtaji Shaytwaan hula pamoja naye katika chakula na kinywaji chake. Wakati wa kumaliza kula aseme:

“Alhamdulillaah.”

Anapomaliza kula na kunywa amhimidi Allaah (´Azza wa Jalla) Aliyemruzuku na Kumsahilishia chakula na kinywaji hichi. Yeye ndiye mwenye kukiendesha chakula na kinywaji hichi kwenye tumbo la mwanaadamu na mishipa yake ili kisiweze kumdhuru. Yote haya ni katika fadhila za Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah Anamruzuku mwanaadamu na kuendesha matumizi yake ili asiweze kudhurika kwacho. Matumizi na uendeshaji, yote mawili ni katika neema ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo amhimidi Allaah kwa neema hizi kubwa. Akumbuke wale walio wagonjwa kwa sababu ya kula na kunywa na hali zao. Hivyo amshukuru na amhimidi Allaah kwa hilo. Muislamu asiwe ni mghafilikaji wa kumdhukuru Allaah. Ikiwa hamdhukuru Allaah anapotea na kuangamia na Shaytwaan anamtawala. Kwa ajili hiyo anatakiwa siku zote kumdhukuru Allaah – wakati anapokula, kunywa, kulala, anapokuwa macho, anapokaa na anapotembea. Awe siku zote ni mwenye kumdhukuru Allaah (´Azza wa Jalla) na khaswa Adhkaar zilizowekwa katika nyakati au hali maalum. Ajifunze nazo na kuzisoma daima. Zinamsaidia katika kumuabudu Allaah na kukabiliana na matatizo ya maisha. Zinamkimbiza Shaytwaan kwake. Zinaupa uhai moyo na kuupa mwanga nafsi yake. Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللَّـهِ ۗ أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ
“Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah. Tanabahi! Kwa kumdhukuru Allaah nyoyo hutulia!” (13:28)

Mwanaadamu hatakiwi kusahau kumdhukuru Allaah. Anatakiwa kumdhukuru Allaah siku zote kwa ulimi wake, moyo wake na matendo yake pindi anapokuwa amesimama, amekaa, anatembea na amelala.