Mashairi Si Kama Qaswiydah Zinazoimbwa Hivi Leo

Muulizaji: Ni ipi hukumu ya kuimba Qaswiydah za kidini (Qaswaaid Diyniyyah) kwa sauti ya juu Misikitini wakati wa minasaba ya sikukuu za kidini? al-Albaaniy: Jambo la kwanza ni kuwa katika Uislamu hakuna “Qaswiydah za kidini”. Jambo la pili haijuzu kuwashawishi wenye kuswali Msikitini hata kama itakuwa kwa Aayah za Qur-aan. Mtu asemeje kuhusu Qaswiydah zinazodaiwa kuwa ni za kidini? Zina haki zaidi ya kuwa haijuzu. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Enyi watu! Kila mmoja ana maongezi yake faragha na Mola Wake. Kusiwe yeyote atakayemuudhi mwengine na asiwe yeyote ambaye atanyanyua sauti yake kwa kisomo.” (Ahmad (3/94).) Katika upokezi mwingine imesemwa: “... wakati anaposoma Qur-aan.” Muulizaji: Wanalinganisha hilo na mashairi ya Hassaan bin Thaabit. al-Albaaniy: Mashairi ya Hassaan bin Thaabit? Ni Qaswiydah za kidini? Mimi nimekwambia kwamba Qaswiydah za kidini hakuna katika Uislamu. Ama mashairi ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatetewa, yaseme utakavyo. Lakini usiyaimbe na kuyafanya kuwa ni Dini. Yakasomwa kama jinsi unavyomdhukuru Allaah na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Muulizaji: Vipi katika Uislamu kusiwe Qaswiydah za Kiislamu na za Kidini ikiwa mtu ataimba kuhusu Uislamu na tabia za Kidini? al-Albaaniy: Hayo unayoyasema yaliyokuwepo kwa wema wetu waliotangulia? Aina hii ilikuwepo katika zama za Salaf-us-Swaalih? Muulizaji: Aina ipi? al-Albaaniy: Aina hii ambayo unamaanisha. Kwa nini hamwongei? Muulizaji: Malengo ya mashairi na Qaswiydah za kiarabu... al-Albaaniy: Samahani. Sitaki unirudilie swali lako. Nimefahamu swali lako. Ninachotaka ni wewe kunijibu swali langu kwa kifupi. Je, hili lilikuwa linajulikana kwa wema wetu waliotangulia? Muulizaji: Hapo kabla? Hapana. al-Albaaniy: Hivyo ndivyo! Sasa ndio umeanza kuongea baada ya kukaa kimya. Muulizaji: Hapana, sikuwa kimya. al-Albaaniy: Hakuna neno. Hakuna neno. Hivyo yaliyowatosheleza na sisi vilevile yanatutosheleza.

Muulizaji: Ni ipi hukumu ya kuimba Qaswiydah za kidini (Qaswaaid Diyniyyah) kwa sauti ya juu Misikitini wakati wa minasaba ya sikukuu za kidini?

al-Albaaniy: Jambo la kwanza ni kuwa katika Uislamu hakuna “Qaswiydah za kidini”.

Jambo la pili haijuzu kuwashawishi wenye kuswali Msikitini hata kama itakuwa kwa Aayah za Qur-aan. Mtu asemeje kuhusu Qaswiydah zinazodaiwa kuwa ni za kidini? Zina haki zaidi ya kuwa haijuzu. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Enyi watu! Kila mmoja ana maongezi yake faragha na Mola Wake. Kusiwe yeyote atakayemuudhi mwengine na asiwe yeyote ambaye atanyanyua sauti yake kwa kisomo.” (Ahmad (3/94).)

Katika upokezi mwingine imesemwa:

“… wakati anaposoma Qur-aan.”

Muulizaji: Wanalinganisha hilo na mashairi ya Hassaan bin Thaabit.

al-Albaaniy: Mashairi ya Hassaan bin Thaabit? Ni Qaswiydah za kidini? Mimi nimekwambia kwamba Qaswiydah za kidini hakuna katika Uislamu. Ama mashairi ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatetewa, yaseme utakavyo. Lakini usiyaimbe na kuyafanya kuwa ni Dini. Yakasomwa kama jinsi unavyomdhukuru Allaah na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Muulizaji: Vipi katika Uislamu kusiwe Qaswiydah za Kiislamu na za Kidini ikiwa mtu ataimba kuhusu Uislamu na tabia za Kidini?

al-Albaaniy: Hayo unayoyasema yaliyokuwepo kwa wema wetu waliotangulia? Aina hii ilikuwepo katika zama za Salaf-us-Swaalih?

Muulizaji: Aina ipi?

al-Albaaniy: Aina hii ambayo unamaanisha. Kwa nini hamwongei?

Muulizaji: Malengo ya mashairi na Qaswiydah za kiarabu…

al-Albaaniy: Samahani. Sitaki unirudilie swali lako. Nimefahamu swali lako. Ninachotaka ni wewe kunijibu swali langu kwa kifupi. Je, hili lilikuwa linajulikana kwa wema wetu waliotangulia?

Muulizaji: Hapo kabla? Hapana.

al-Albaaniy: Hivyo ndivyo! Sasa ndio umeanza kuongea baada ya kukaa kimya.

Muulizaji: Hapana, sikuwa kimya.

al-Albaaniy: Hakuna neno. Hakuna neno. Hivyo yaliyowatosheleza na sisi vilevile yanatutosheleza.


  • Author: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (15)
  • Kitengo: Uncategorized , Da´wah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 9th, February 2014