Mapenzi Na Khasira Za Allaah Kwa Mtu

Allaah (Ta´ala) Anampenda mtu kunapokuwa na sababu ya kumpenda na Anamchukia kunapokuwa na sababu ya kumchukia. Kutokana na hili, Allaah Anaweza kumpenda mtu siku moja na Akamchukia siku nyingine. Kwa sababu hukumu inategemea sababu. Ama kuhusiana na matendo, Allaah Hupenda daima wema, uadilifu na mfano wa hayo. Ahl-ut-Ta'wiyl wanakanusha Sifa hizi. Wanafasiri mapenzi na radhi kuwa ni thawabu au kutaka kwa thawabu wakati wanafasiri khasira kuwa ni adhabu au kutaka kwa adhabu. Wanasema linatokana na upungufu na kumfananisha na viumbe kumthibitishia sifa hizi. Sahihi ni kwamba zinathibitishwa kwa Allaah ('Azza wa Jalla) kwa njia inayolingana na Yeye kama jinsi tu sifa nyinginezo zote ambazo zimethibitishwa na Ahl-ut-Ta'wiyl. Ni jambo la wajibu kuwa na uhusiano ufuatao kwa Sifa ambazo Allaah Amejithibitishia Yeye Mwenyewe: 1 - Ni lazima kuzithibitisha kama za kweli na za halisi. 2 - Haitakiwi kabisa kuzifananiza wala kuzifikiria. Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn Chanzo: al-Qawl al-Mufiyd (2/122)

Allaah (Ta´ala) Anampenda mtu kunapokuwa na sababu ya kumpenda na Anamchukia kunapokuwa na sababu ya kumchukia. Kutokana na hili, Allaah Anaweza kumpenda mtu siku moja na Akamchukia siku nyingine. Kwa sababu hukumu inategemea sababu. Ama kuhusiana na matendo, Allaah Hupenda daima wema, uadilifu na mfano wa hayo.

Ahl-ut-Ta’wiyl wanakanusha Sifa hizi. Wanafasiri mapenzi na radhi kuwa ni thawabu au kutaka kwa thawabu wakati wanafasiri khasira kuwa ni adhabu au kutaka kwa adhabu. Wanasema linatokana na upungufu na kumfananisha na viumbe kumthibitishia sifa hizi.

Sahihi ni kwamba zinathibitishwa kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) kwa njia inayolingana na Yeye kama jinsi tu sifa nyinginezo zote ambazo zimethibitishwa na Ahl-ut-Ta’wiyl. Ni jambo la wajibu kuwa na uhusiano ufuatao kwa Sifa ambazo Allaah Amejithibitishia Yeye Mwenyewe:

1 – Ni lazima kuzithibitisha kama za kweli na za halisi.
2 – Haitakiwi kabisa kuzifananiza wala kuzifikiria.

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Chanzo: al-Qawl al-Mufiyd (2/122)


  • Kitengo: Uncategorized , Hasira na Ghadhabu za Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013