Mambo Huenda Chap Chap Kwa Jamaa´at-ut-Tabliygh

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Mayahudi wamegawanyika makundi sabini na moja. Manaswara wamegawanyika makundi sabini na mbili. Na Dini hii itakuja kugawanyika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni lipi hilo, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni Jamaa´ah.” Imepokelewa hivo katika Hadiyth ya Mu´aawiyah. Ama kuhusiana na Hadiyth: “Ni lile litakalofuata yale ambayo mimi na Maswahabah wangu waliyomo hivi leo.” ni dhaifu kwa sababu imepokelewa kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Ziyaad bin An´am. al-Haakim, ambaye anajulikana kuwa mlaini, amesema: ”Si hoja yoyote.” Ni lazima kwa Waislamu kuwa mkusanyiko mmoja. Ni nani aliyetupa idhini ya kuwa makundi mengi? al-Ikhwaan al-Muslimuun ni kundi limoja, Jamaa´at-ut-Tabliygh ni kundi limoja. Jamaa´at-ut-Tabliygh imekusanya kati ya Taswawwuf, Bid´ah na ujinga. Mtu akijiunga na wao baada ya ´Aswr wanamlazimisha kutoa darsa Maghrib. Masikini mtu hajui lolote juu ya Dini. Kwa ajili hiyo masikini huyu anaanza kuchanganya mambo. Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy Chanzo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 42-43 Toleo: 13-09-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mayahudi wamegawanyika makundi sabini na moja. Manaswara wamegawanyika makundi sabini na mbili. Na Dini hii itakuja kugawanyika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”
Wakasema: “Ni lipi hilo, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni Jamaa´ah.”

Imepokelewa hivo katika Hadiyth ya Mu´aawiyah. Ama kuhusiana na Hadiyth:

“Ni lile litakalofuata yale ambayo mimi na Maswahabah wangu waliyomo hivi leo.”

ni dhaifu kwa sababu imepokelewa kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Ziyaad bin An´am. al-Haakim, ambaye anajulikana kuwa mlaini, amesema:

”Si hoja yoyote.”

Ni lazima kwa Waislamu kuwa mkusanyiko mmoja. Ni nani aliyetupa idhini ya kuwa makundi mengi? al-Ikhwaan al-Muslimuun ni kundi limoja, Jamaa´at-ut-Tabliygh ni kundi limoja. Jamaa´at-ut-Tabliygh imekusanya kati ya Taswawwuf, Bid´ah na ujinga. Mtu akijiunga na wao baada ya ´Aswr wanamlazimisha kutoa darsa Maghrib. Masikini mtu hajui lolote juu ya Dini. Kwa ajili hiyo masikini huyu anaanza kuchanganya mambo.

Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Chanzo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 42-43
Toleo: 13-09-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Jamaa´at-ut-Tabliygh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 13th, September 2014