Makatazo Ya Mume Ya Kutomdhuru Mke Wake

Kisha akasema (Rahimahu Allaah): "Na kakataza kuwadhuru na kuwafanyia uadui." Shaykh DMuhammad al-Madkhaliy: Yaani kuwadhuru wanawake. Mume asimdhuru mke wake. Kama Alivyosema (Jalla wa ´Alaa): وَلَا تُضَارُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْهِنَّ ۚ وَإِن كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ "Na wala msiwadhuru ili muwatie dhiki. Na wakiwa ni wenye mimba, basi wagharamieni (matumzi yao) mpaka wazae mimba zao." (65:06) Anasema (Jalla wa ´Alaa): وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ "Na kaeni nao kwa wema." (04:19) وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا "Na wala msiwazuie kuwapa dhara kwa kuvuka mipaka (kuwafanyia uadui)." (02:231) Kumletea madhara hakujuzu. Ima kuishi naye kwa wema au kuachana nae kwa wema. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: "Hakuna madhara wala kudhuriana." Yule atakayemdhuru Muislamu mwenzake, naye Allaah Atamd-huru. Kama Alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hali kadhalika, haijuzu kwa waume kuwafanyia uadui wake zao; kwa kuwapiga na kuwatukana. Na kuchukua haki zoa ambazo ni maalum kwao; katika mali na vitu vyao wanavyomiliki. Haijuzu kuwafanyia uadui, sawa katika nafsi zao wala mali zao ambazo ni maalum kwao. Hili ni jambo la haramu linatolewa dalili na maandiko ya Kishari´ah ambayo mmesikia katika Qur-aan na Sunnah. Na hilo si kwa jengine isipokuwa ni kwa sababu mwananke ni kiumbe dhaifu. Mwanaume jabari, mkandamizaji ambaye dini yake imedhoofika na elimu yake ni ndogo anaweza kumtumia na kufikiria kuwa mwanamke ni kama mnyama kwake. Hili halijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Allaah (´Azza wa Jalla) wamebainisha haki alizo nazo mke na mume. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wasia wake mwisho wa uhai wake ilikuwa ni kuwatendea kheri wanawake: "Ninawausia kuwatendea kheriwanawake." Kausia kuwatendea kheri katika Khutbah ya mwisho ya kuaga siku ya ´Arafah, akasema: "Ninawausia kuwatendea kheri wanawake. Kwani wao ni wafungwa wenu." [Ibn Maajah (1851)] Kawashabihisha na wafungwa kwa kushikamana kwao sana na kukaa nyumbani, hawatoki humo. Kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kawaamrisha hilo. Anasema (Jalla wa ´Alaa) Kuwaambia wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ni wamama wa waumini na ndio wanawake bora: وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ "Na bakieni majumbani mwenu, na wala msionyeshe mapambo na uzuri (kujishaua) kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake majahili wa awali (wakijishaua)." (33:33) Mwanamke kubakia kwake nyumbani kwake amekuwa ni kama mfungwa aliwekwa gerezani. "Kwani wao ni wafungwa wenu." Kitu muhimu ni kuwa, haijuzu kumdhuru mwanamke kwa hali yoyote ile ila kwa yale mambo ambayo Shari´ah imeruhusu, imebainisha katika Qur-aan na katika Sunnah za Mtume Wake.Kumtia adabu kwa njia ya Kishari´ah ni kitu kinajuzu. Lakini pamoja na hivyo, anasema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) kuhusu Mtume: "Hajawahi kumpiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanamke kwa mkono wake wala mtumishi."

Kisha akasema (Rahimahu Allaah):

“Na kakataza kuwadhuru na kuwafanyia uadui.”

Shaykh DMuhammad al-Madkhaliy:

Yaani kuwadhuru wanawake. Mume asimdhuru mke wake. Kama Alivyosema (Jalla wa ´Alaa):

وَلَا تُضَارُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْهِنَّ ۚ وَإِن كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ
“Na wala msiwadhuru ili muwatie dhiki. Na wakiwa ni wenye mimba, basi wagharamieni (matumzi yao) mpaka wazae mimba zao.” (65:06)

Anasema (Jalla wa ´Alaa):

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
“Na kaeni nao kwa wema.” (04:19)

وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا
“Na wala msiwazuie kuwapa dhara kwa kuvuka mipaka (kuwafanyia uadui).” (02:231)

Kumletea madhara hakujuzu. Ima kuishi naye kwa wema au kuachana nae kwa wema. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Hakuna madhara wala kudhuriana.”

Yule atakayemdhuru Muislamu mwenzake, naye Allaah Atamd-huru. Kama Alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hali kadhalika, haijuzu kwa waume kuwafanyia uadui wake zao; kwa kuwapiga na kuwatukana. Na kuchukua haki zoa ambazo ni maalum kwao; katika mali na vitu vyao wanavyomiliki. Haijuzu kuwafanyia uadui, sawa katika nafsi zao wala mali zao ambazo ni maalum kwao. Hili ni jambo la haramu linatolewa dalili na maandiko ya Kishari´ah ambayo mmesikia katika Qur-aan na Sunnah. Na hilo si kwa jengine isipokuwa ni kwa sababu mwananke ni kiumbe dhaifu. Mwanaume jabari, mkandamizaji ambaye dini yake imedhoofika na elimu yake ni ndogo anaweza kumtumia na kufikiria kuwa mwanamke ni kama mnyama kwake. Hili halijuzu.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Allaah (´Azza wa Jalla) wamebainisha haki alizo nazo mke na mume. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wasia wake mwisho wa uhai wake ilikuwa ni kuwatendea kheri wanawake:

“Ninawausia kuwatendea kheriwanawake.”

Kausia kuwatendea kheri katika Khutbah ya mwisho ya kuaga siku ya ´Arafah, akasema:

“Ninawausia kuwatendea kheri wanawake. Kwani wao ni wafungwa wenu.” [Ibn Maajah (1851)]

Kawashabihisha na wafungwa kwa kushikamana kwao sana na kukaa nyumbani, hawatoki humo. Kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kawaamrisha hilo. Anasema (Jalla wa ´Alaa) Kuwaambia wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ni wamama wa waumini na ndio wanawake bora:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ
“Na bakieni majumbani mwenu, na wala msionyeshe mapambo na uzuri (kujishaua) kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake majahili wa awali (wakijishaua).” (33:33)

Mwanamke kubakia kwake nyumbani kwake amekuwa ni kama mfungwa aliwekwa gerezani.

“Kwani wao ni wafungwa wenu.”

Kitu muhimu ni kuwa, haijuzu kumdhuru mwanamke kwa hali yoyote ile ila kwa yale mambo ambayo Shari´ah imeruhusu, imebainisha katika Qur-aan na katika Sunnah za Mtume Wake.Kumtia adabu kwa njia ya Kishari´ah ni kitu kinajuzu. Lakini pamoja na hivyo, anasema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) kuhusu Mtume:

“Hajawahi kumpiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanamke kwa mkono wake wala mtumishi.”