Maisha Ya Kinyama Katika Nchi Ya Kikafiri

Hali nyingine ni Muislamu anahama peke yake kwenda Ulaya, ametoka katika nchi za mashariki ili aishi peke yake kati ya makafiri pasina kuweza kuonesha alama za Dini yake. Pengine wakalazimika kila siku kujumuisha kati ya Dhuhr na ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa usiku. Wanaziswali zote usiku. Mchana hawawezi kufanya hivo. Hali ya mambo inaweza kufikia kiasi cha kwamba akaacha Ijumaa kabisa. Mapumziko kwao inakuwa siku ya Jumapili. Ijumaa ni siku ya kazi. Anakuwa ni mwenye kulazimika kumtii mudiri wa kampuni George. ´Abdur-Rahmaan anamtii George! George anasema kumwambia mapumziko kwetu ni siku ya Jumamosi na sio Ijumaa. Ukipenda fanya kazi kwetu na kama hutaki acha. Huko anaishi maisha ya kinyama ambayo yanakuwa kwa kula, kunywa na kuoa. Anakuwa hana jengine zaidi ya haya. Anaacha Dini yake. Mfano wa maisha kama haya hayajuzu. Anahama kwenda kuishi mwenyewe kati ya makafiri hali ya kuwa ni mdhalili na kusahau utukufu wa Uislamu: وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ “Na utukufu ni wa Allaah na wa Rasuli Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawaelewi.” (63:08) Anasahau maana hii. Kwa udhalili na kwa kuinamisha kichwa chini anaishi chini ya uongozi wa George. Anamlaghai kwa maneno “Ee bosi” ili aweze kupata kuswali, George hamruhusu. Mfano wa maisha kama haya ni haramu. Ni haramu kwa Muislamu kuishi maisha kama haya katika nchi ya kikafiri. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 115-116 Toleo la: 26-05-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Hali nyingine ni Muislamu anahama peke yake kwenda Ulaya, ametoka katika nchi za mashariki ili aishi peke yake kati ya makafiri pasina kuweza kuonesha alama za Dini yake. Pengine wakalazimika kila siku kujumuisha kati ya Dhuhr na ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa usiku. Wanaziswali zote usiku. Mchana hawawezi kufanya hivo. Hali ya mambo inaweza kufikia kiasi cha kwamba akaacha Ijumaa kabisa. Mapumziko kwao inakuwa siku ya Jumapili. Ijumaa ni siku ya kazi. Anakuwa ni mwenye kulazimika kumtii mudiri wa kampuni George. ´Abdur-Rahmaan anamtii George! George anasema kumwambia mapumziko kwetu ni siku ya Jumamosi na sio Ijumaa. Ukipenda fanya kazi kwetu na kama hutaki acha.

Huko anaishi maisha ya kinyama ambayo yanakuwa kwa kula, kunywa na kuoa. Anakuwa hana jengine zaidi ya haya. Anaacha Dini yake. Mfano wa maisha kama haya hayajuzu. Anahama kwenda kuishi mwenyewe kati ya makafiri hali ya kuwa ni mdhalili na kusahau utukufu wa Uislamu:

وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ
“Na utukufu ni wa Allaah na wa Rasuli Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawaelewi.” (63:08)

Anasahau maana hii. Kwa udhalili na kwa kuinamisha kichwa chini anaishi chini ya uongozi wa George. Anamlaghai kwa maneno “Ee bosi” ili aweze kupata kuswali, George hamruhusu. Mfano wa maisha kama haya ni haramu. Ni haramu kwa Muislamu kuishi maisha kama haya katika nchi ya kikafiri.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 115-116
Toleo la: 26-05-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 26th, May 2014