Maimamu Ambao Wamefasiri Uso Wa Allaah Mwelekeo

al-Buutwiy anamnasibishia Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengine ya kwamba wao wamefasiri Uso wa Allaah kama mwelekeo, Qiblah au kiini. Ameona mwenyewe kwamba huku ni kuharibu (kupotosha) Uso ambao ni moja katika Sifa ya Allaah za Dhati. Fikra hii bila ya shaka yoyote ni ya makosa. Maimamu hawa hawakumaanisha hivi anavyoona. Neno Wajh, Uso, linaweza kuwa na maana nyingi. Inaweza kumaanisha kiini cha sifa, Dini, nia, mwelekeo na njia. Ni muktadha wa neno ndio hutoa maamuzi wa nini (neno) linamaanisha. Ikiwa neno Wajh litafasiriwa kwa kuzingatia baadhi ya maana hizi kutokana na muktadha sahihi au nyingine, basi ni sahihi na si kuharibu. Hakika ni kwamba, (haya) ni maelezo tu ya neno hili. Hili linathibitisha kuwa Dr. Kakosea kabisa pindi anaposema kwamba inaruhusiwa kuelewa Aayah na Hadiyth za Sifa za Allaah kama (kwa njia ya) mafumbo na si (kwa njia ya) halisi. Hana hata dalili yoyote ya hilo kutoka kwa Salaf. Aliyoyataja kutoka kwa baadhi yao aidha ni kwamba hayakuthibiti au ni kwamba hayamaanishi kabisa hivyo anavyoona yeye. Mwandishi: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: al-Bayaan li Akhtwaa' Ba´dhw-il-Kuttaab, uk. 144-145

al-Buutwiy anamnasibishia Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengine ya kwamba wao wamefasiri Uso wa Allaah kama mwelekeo, Qiblah au kiini. Ameona mwenyewe kwamba huku ni kuharibu (kupotosha) Uso ambao ni moja katika Sifa ya Allaah za Dhati.

Fikra hii bila ya shaka yoyote ni ya makosa. Maimamu hawa hawakumaanisha hivi anavyoona. Neno Wajh, Uso, linaweza kuwa na maana nyingi. Inaweza kumaanisha kiini cha sifa, Dini, nia, mwelekeo na njia. Ni muktadha wa neno ndio hutoa maamuzi wa nini (neno) linamaanisha. Ikiwa neno Wajh litafasiriwa kwa kuzingatia baadhi ya maana hizi kutokana na muktadha sahihi au nyingine, basi ni sahihi na si kuharibu. Hakika ni kwamba, (haya) ni maelezo tu ya neno hili.

Hili linathibitisha kuwa Dr. Kakosea kabisa pindi anaposema kwamba inaruhusiwa kuelewa Aayah na Hadiyth za Sifa za Allaah kama (kwa njia ya) mafumbo na si (kwa njia ya) halisi. Hana hata dalili yoyote ya hilo kutoka kwa Salaf. Aliyoyataja kutoka kwa baadhi yao aidha ni kwamba hayakuthibiti au ni kwamba hayamaanishi kabisa hivyo anavyoona yeye.

Mwandishi: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: al-Bayaan li Akhtwaa’ Ba´dhw-il-Kuttaab, uk. 144-145


  • Kitengo: Uncategorized , al-Buutwiy, Muhammad Sa´iyd Ramadhaan
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013